Mbunge wa Rombo Joseph Selasini Kusherehekea Mwaka Mpya Kwa Kupanda Miti na Wananchi Wake

Kitu Kizito

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
242
250
Mbunge wa Rombo Mh Joseph Selasini (CHADEMA) ataongoza mamia ya vijana na wanajamii wengine katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti jimboni humo kesho January 1, 2017 katika eneo la Mamsera.
1483158836608.jpg

Zaidi ya miche 1000 ya miti imeandaliwa kuoteshwa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Rombo katika jitihada za kukabiliana na uharibifu wa mazingira kutokana na ukame uliotokana na tabia ya wananchi kukata miti bila kuotesha miti mbafala.

Zoezi hilo linatarajiwa kuhitimishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh Agnes Hokororo eneo la Mkuu yalipo makao makuu ya kiutawala ya Wilaya ya Rombo.

Wilaya ya Rombo ambayo kijiografia ndiko ulipo mlima Kilimanjaro imeathirika sana na mabadiliko ya tabia nchi kiasi cha kufikia kukauka kwa vijito na chemchemi nyingi na kupelekea adha kubwa ya upatikanaji maji tofauti na zamani.

Wenyeji wameiekeza blogu hii kuwa joto limeongezeka sana na mvua hazitabiriki tena huku theluji mlimani ambayo husababishwa na unyevu nyevu wa miti kwenda mlimani inayeyuka.

Mh Mbunge anawakaribisha watu wote kushiriki kampeni hii muhimu kwa ajili ya faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Source: Mbunge wa Rombo Joseph Selasini Kusherehekea Mwaka Mpya Kwa Kupanda Miti na Wananchi Wake | PolitiksiFactTrack ''ARUSHA255''
 

laki si pesa.

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
10,020
2,000
Ben alimfanyia sana fitina Selasini hata hilo dili lake na Mbowe la kujiteka ni laana za Selasini hizo
 

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
15,650
2,000
Safi sana ndugu Selasini....japo watu wanataka jimbo kwa mbinu ya kujiteka sisi tunatambua kazi yako.
 

Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,423
2,000
ingekuwa vema angefanya hiyo shughuli tarehe 2 kwa kuwa 1 imeangukia j2 siku ya mapumziko
 

future mind

Senior Member
Dec 13, 2016
151
250
Mnapanda miti pia mkumbuke kuimwagilia sio mnapanda afu mnapotea mazima kuwe na utaratibu wa kuimwagilia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom