Mbunge wa Nkasi Ally Kessy avunja rekodi kwa kuongea pointi katika hali ya mzaha

Mndengereko

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
7,280
3,345
Mbunge wa Nkasi, Ally Keissy, June 18 2013 alivunja rekodi ya kuwa mbunge aliyechekesha watu wengi wakiwemo wabunge bungeni, sio tu kwa sababu ya kutoa vichekesho lakini pia ni kwa namna alivyokua akieleza mambo pamoja na kuikosoa Serikali.

Anakwambia ‘Twende Kigoma, Mwanza, Tabora, Mpanda, Shinyanga tuwaulize watu mnataka reli au viwanja vya ndege… mtashangaa wenyewe, vipaumbele gani mnapeleka viwanja vya ndege? mtu gani wa Tabora anapanda ndege kama sio Mbunge, DC na Mkuu wa mkoa… ? ni Treni…… hawataki viwanja vya ndege, viwanja vya ndege baadae…. kwanza ndege zenyewe zikowapi? mna ndege nyie???? mabilioni ya hela mnajenga viwanja vya ndege… ndege hatuna, wapanda ndege ni nyie wenyewe Wabunge na Mawaziri… jamani tutulie tuweke vipaumbele ambavyo vinaweza kusaidia Wananchi na uchumi wa nchi, mtapakia mizigo, madebe ya mawese kwenye ndege? migebuka kwenye ndege? acheni mambo ya kurukiakurukia ndege zenyewe hamna"

"Mmefilisi shirika la ndege tunawaambia tuwakamate wale waliofilisi tuwafunge pingu zao, sasa sheria mpya kama wamekufa tuwafufue tuwasage mifupa yao… mi nashangaa baadhi ya Wabunge hapa wanakuja tuondoe hela hii tuondoe hela hii… utapata wapi hela ya kuiendeleza nchi yako? leo Uingereza kodi ya TV unalipia, ukiwa nazo tatu utalipia kila moja… wewe una TV mpaka 10 mpaka chooni, umekaa hulipii chochote… nani akudai? " – Keissy

"Mafisadi wanajulikana, hata mzee Sitta nimemsikia siku moja akisema hawa dawa yao kuwanyonga….. mimi Mbunge hapa, baada ya mwaka nina gorofa 10 nimepata wapi hela? sijakwenda benki sijakwenda popote, hapohapo ndio pa kunibana… na hizi pesa zinazochangiwa kwenye maharusi mabilioni ya hela, michango ya kanisa na Misikiti zikatwe kodi 30% palepale… wauza dawa za kulevya kama hawajakamatwa lakini wana majumba, wakatwe kodi.. shida yetu kodi sisi hatujui dawa zako umepeleka wapi huko tumeshindwa kukukamata lakini tulipe kodi" – Mbunge Keissy

"Tukipata maafa kidogo… kelele misaada, tukisema kodi mnapiga kelele nyie Wabunge… Ebooooo? itakuaje? nani ameoa Mwanamke nyumbani kwake anakwenda kuomba msaada kwa jirani? watakuchukulia mke wako… JITEGEMEE!!!!!"
 
Mchango wa Mhe. Kessy sio vichekesho wala vituko bali ni 'facts' nenda kwenye mikoa aliyoitaja wakazi hawana uwezo wa kupanda ndege kwa sh.437,000 kwa trip lakini ukiwapelekea train watapanda kwa sh.19,000/- mpaka Dar huku wakiwaletea zawadi za migebuka, mawaese, sato, sangara na matoborwa ndugu zao waliopo Dar. TRain kwanza ndege baadae. Mimi nipenda mchango wa huyu jamaa
 
Mchango wa Mhe. Kessy sio vichekesho wala vituko bali ni 'facts' nenda kwenye mikoa aliyoitaja wakazi hawana uwezo wa kupanda ndege kwa sh.437,000 kwa trip lakini ukiwapelekea train watapanda kwa sh.19,000/- mpaka Dar huku wakiwaletea zawadi za migebuka, mawaese, sato, sangara na matoborwa ndugu zao waliopo Dar. TRain kwanza ndege baadae. Mimi nipenda mchango wa huyu jamaa
ndio maana nimesema kaongea pointi ningesema kaongea kichekesho peke yake ungekuwa na haki ya kunicriticize,binafsi nakubaliana na alichokisema ila sikubaliani na kuunga kwake mkono hoja.(budget)
 
Hizi ni point tupu, kwa kweli JK anatuuza hivi hivi na omba omba yake. Unafuga mbwa unategemea mavi ya walevi.
 
Amenena ukweli mtupu, nampongeza kwa kuwasemea wanyonge wa Mwanza,Tabora,Kigoma n.k Reli kwanza, viwanja vya ndege baadaye!
 
tunamshukuru sana Mwakyembe kwa kuturudishia train,hope itaendelea kuwepo
 
Huyu Mbunge si ndumilakuwili
Nadhani kajizatiti unajua 2015
kuna mgombea binafsi Ccm
wammwaga anaweza rudi kwa
njia nyingine.

Ila aliongea ukweli mtupu km vile
hayuko Ccm.
 
katika wabunge wa CCM wasema kweli na wanaojua kuibana serikali huyu ni mmoja wapo wengine ni Deo Filikunjombe,Mpina Luhaga na Esther Bulaya.Safi sana mh Ally Kessy.
 
jamaa kaongea kweli tupup kama serikali ilnashindwa kuwakamata wanauza madawa ya ku;evya na wa wanajulikana basi bora tuanze kuitoza kodi tu ili serikali ifaidike!!!!
 
Wabunge wa ccm kama wamelogwa, kwa zile point kali namna ile then anaunga mkono hoja aiingii hata kidogo

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wanashindwa kuchukua kodi kwa wenye fedha, wanaendelea kuwakamua maskini. Wenye fedha wanakwepa kodi na wanalindwa na mihimiri ya serikali.
Nchi ilishakufa long time tangu 2005.
 
Huyu Jamaa namkubali sana, ni mzalendo na mkweli...huwa anaongea "facts" na hajui kujikomba.
 
kuna mahali nimesoma huku kachekesha sana......eti "au gesi ni ya kujamba?"
 
hapo angekuwa yule mchumia tumbo aka mgeni, Mgeni au Mzee wa Lulu angesema tunataka ndege nyingi kial wilaya na kata zime na ndege, kama alivyo wai kusema kuwa" Kma nchi yetu ingelingana na Kenya kwa ukubwa, basi lami zilizojengwa na serikali ya ccm zingefika hadi chooni " bila kujua kuwa hazina ubora na ni za zima moto
 
wabunge wetu wanataka kutujengea viwanja vya ndege,je ni watanzania wangapi wanapanda ndege?je mkulima wa moshi vijijini atapeleka mazao yake sokoni kwa kutumia ndege?2015 tuchague viongozi watakao tatua matatizo ya watanzanzia masikini
 
Back
Top Bottom