Mbunge wa Mwibara aanza kupoteza sifa ya Ubunge

Mbona shamba halina hata banda la mdudu jamani, tunapoteza fursa!

Ni kweli mkuu! Shamba linaendelezwa kila mwaka kwa kilimo na familia hiyo! Angalia hapa utaona mabua ya ulezi.
 
Attachments

  • 1411416023227.jpg
    1411416023227.jpg
    79.2 KB · Views: 323
Ukiwa mwana siasa jiepushe na migogoro kwa wapiga kura wako yale masilahi binafsi yakatae! Haiwezekani mbunge uishi kwa kuviziavizia kama wananchi hawana uelewa na maswala ya kisheria, wewe utumie huo mwanya kupiga! Watu kwa sasa wameamka sana haibiwi mtu hapa!
 
simjui huyu mbunge, lakini habari hii inaonekana ni ya kizushi-lengo likiwa kuchafua jina la mtu kwa kuwa uchaguzi umekaribia. inaonekana mwandishi anataka kugombea ubunge mwakani katika jimbo hilo.
 
Nampongeza sana Mbunge Kangi Lugola kuisaidia Polisi kukamatwa kwa Mwizi.....

Keep it up Mh Kangi
 
Nampongeza sana Mbunge Kangi Lugola kuisaidia Polisi kukamatwa kwa Mwizi.....

Keep it up Mh Kangi

Mungi tulia! Usije ukushusha ubora wako hapa jukwaani. Hakuna mwizi hapo! Kangi anajenga veta karibu na mpaka wa shamba la watu, sasa eneo lake ni dogo anatamani avamie eneo la huyo uvccm.

Eneo hilo ni eneo halali na kangi hajaingia bado ndani ya shamba hilo ila anapima upepo kupima nguvu ya hiyo familia kama ni legelege ashirikiane na viongizi wenye njaa kali wapore hilo eneo. Tafakari utaelewa. Nampenda kangi hasa kuunga mkono serikali tatu. Lakini namshangaa kwa nini anachukua posho na katiba hakuna!
 
Shika yenu ccm hamtaki mtu anayewapinga au kuwachallenge.Akitokea basi mtamtafutia skendo ili aonekane mbaya.Mbinu zenu tunazijua na kwa taarifa yenu Kangi hamumuwezi maana huwa haogopi akiamua kuwabomoa huwa hapepesi macho au kumumunya maneno.

Kwa hiyo hii habari ya mpaka au shamba umeileta ili iweje?mbona hukuleta habari ya wakazi wa chasimba wanaoonewa na serikali yenu au wale wa kule mvomero au unaona ukileta ya Lugola ndo utakuwa umemmaliza? Ama kweli kuwa na nywele nyingi si kuwa na akili. Na pia unaweza kuwa na akili lakini zisizo na akili
 
simjui huyu mbunge, lakini habari hii inaonekana ni ya kizushi-lengo likiwa kuchafua jina la mtu kwa kuwa uchaguzi umekaribia. inaonekana mwandishi anataka kugombea ubunge mwakani katika jimbo hilo.

Rukiko! Njoo hapa Kibara ujionee madudu ya Kangi! Hakuna kugombea ubunge wala uzushi, haki ndiyo inatafutwa! Kama mbunge akijiepusha na huu mgogoro wa shamba la watu atakuwa amesalimika! Kwenye hicho kichuguu ndio mpaka kwenda juu ni kwake na veta yake.

Kushuka chini ya hicho kichuguu si eneo lake analazimisha aje baadae aingie kwa madai kuwa aliuziwa na Wahuni kinyemela kumbe aliingia choo cha kike! " mkenge"
 
simjui huyu mbunge, lakini habari hii inaonekana ni ya kizushi-lengo likiwa kuchafua jina la mtu kwa kuwa uchaguzi umekaribia. inaonekana mwandishi anataka kugombea ubunge mwakani katika jimbo hilo.

Haya Rukiko mpaka huo hapo kwenye kichuguu
 
Shika yenu ccm hamtaki mtu anayewapinga au kuwachallenge.Akitokea basi mtamtafutia skendo ili aonekane mbaya.Mbinu zenu tunazijua na kwa taarifa yenu Kangi hamumuwezi maana huwa haogopi akiamua kuwabomoa huwa hapepesi macho au kumumunya maneno.

Kwa hiyo hii habari ya mpaka au shamba umeileta ili iweje?mbona hukuleta habari ya wakazi wa chasimba wanaoonewa na serikali yenu au wale wa kule mvomero au unaona ukileta ya Lugola ndo utakuwa umemmaliza? Ama kweli kuwa na nywele nyingi si kuwa na akili. Na pia unaweza kuwa na akili lakini zisizo na akili

Habari imeletwa kwa hisani ya wanakijiji cha Kibara na Namibu! Sasa Chasimba na Mvomero kama nao wanamatatizo kama haya ni vizuri wawakilishi wao wakayaleta hapa jukwaani tujadili.

Niweke wazi hapa hakuna ugomvi wa ccm na kangi, kuna mgogoro wa ardhi kijana wa uvccm kata ya Kibara ni miongoni mwa watoto wa familia wanaomiliki sahamba hilo. Umeanza kuelewa! Kangi anatamani apore hilo shamba kakini mziki uko upande wa pili nao wametegesha rada zao!
 
Kuna msamalia mwema kanitonya hapa kuwa mbunge hilo eneo kangi anasumbuka tu! Kama alitoa mlungura kwa wale wahuni akawambie watapike! Sasa kumekucha ardhi ni mali hakuna mtu atakubali kuachia mali kizembe hivyo!
 
Huyu kijana wa UVCCM ambaye ana mgogoro na mbunge ndo huyu aliyeweka hili bandiko hapa
 
Tubu maana kutukana ni dhambi!!

Kangi ndiye mwenye dhambi! Mnamuona kangi kwa jicho la upofu! Kwa kuwa anamisimamo hasa katiba mpya lakini posho anachukua.

Likini ukija jimboni kwake ni shidaaa!! Mtaamini siku moja na kuheshimu hili bandiko langu! Nakushukuru sana kwa kuanza kuelewa!
 
heshima kwenu wana ukumbi!

Leo nimekutana na wapiga kura wa mh.Kangi Ndege Lugola mbunge wa mwibara wakimlaumu mh.Mbunge kwa kitendo chake cha kiovu alichomfanyia mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kibara tar.02.09.2014!

Wanachama wa ccm walishangazwa kuona mbunge wa jimbo lao; akitoa shinikizo kwa mkuu wa kituo cha polisi kata ya Kibara kuondoka na maaskari wanne wakiwa na bunduki mbili aina ya SMG na kumkamata kiongozi wa chama(jina limehifadhiwa) kwa madai kwamba yeye ni jambazi amevamia veta yake na kukata miti ovyo katika eneo lake. Mwenyekiti aliwekwa maabusu kuanzia saa 11 jioni mpaka kesho yake saa 3 asubuhi ndipo akapata dhamana.

Taarifa za ndani zilionekana mbunge alitoa shinikizo kwa askari polisi kumlazimisha huyo kiongozi wa chama, kuweka maandishi ya kukubali tangu leo; asifanye shughuli yoyote ya maendeleo ndani ya eneo hilo, kitu ambacho hakikuwezekana kabisa na mtuhumiwa alikataa na kudai familia inamiliki hilo eneo tangu Uhuru 1961.

Baada ya kufuatilia kwa wanakijiji; ilithibitika kuwa kiongozi huyo wa chama alikuwa kwenye shamba lao akiliandaa kwa ajili ya msimu wa kilimo, kama desturi yao ya kila mwaka. Shamba hilo lina upana wa mita 70 na urefu wa mita 104 sawa na mita za mraba 7280.

Baada ya kumtafuta kiongozi wa serikali ya kijiji cha Namibu(jina linahifadhiwa) aliyekuwepo wakati anapewa sehemu ya eneo hilo, alithibitisha hilo eneo ni mali ya familia anayotoka mwenyekiti wa UVCCM; na mbunge alipewa sehemu ya juu aliko jenga veta yake. Sehemu ya chini ni eneo halali la familia hiyo.

Kangi analazimisha apole eneo kwa njia za kifisadi; kitu ambacho mimi sikukubaliana nae, na niko tayari kwenda mahakamani kutoa ushahidi.

Wananchi walijaa hofu na kushaangaa silaha nzito za kuwindia majangiri zikipita mtaani; eti kuna majambazi yamevamia veta ya kangi! kumbe uongo mtupu! Kuja kuambiwa jambazi anaye tafutwa kumbe ni mwenyekiti wa UVCCM kijana mpole na mnyenyekevu! wananchi walimtupia lawama mkuu wa kituo cha polisi! na mbunge kwa kitendo cha kihuni alichokifanya.

Taarifa za ndani kutoka kwa katibu wa mbunge Mtesigwa Chikulugu! Zinasema kuwa; yeye ndiye aliyemshauri mbunge kumuachia kiongozi wa uvccm vinginevyo angemfunga amkomeshe alidai mmoja wa kiongozi wa karibu na Kangi.

Chanzo chetu cha habari kinadai huyu mwenyekiti wa UVCCM yuko kambi ya aliyewahi kuwa mbunge wa mwibara mh.Charles Mguta Kajege hivyo kumfanya Kangi kumalizia hasira zake kwa kijana huyo. Hizi ni habari za uhakika na popote alipo mbunge wa mwibara kama anabisha aje akanushe!

Tunaviomba vyombo vyote vya habari hasa ITV na redio one! kumulika huu mgogoro wa ardhi mpakani mwa taasisi ya hospitali ya Kibara.

Chanzo:
Wanakijiji Kibara na Namibu!

Ugomvi wenu unamuondoleaje sifa ya ubunge na kwa katiba ipi
 
Back
Top Bottom