Mbunge wa Musoma Nimrodi Mkono kuhama CCM

Mbunge wa Musoma Nimrodi Mkono kuhama CCM

Eghorohe

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2011
Posts
220
Reaction score
79
Wadau naomba kupata uhakika na ukweli kuhusu habari hii! Habari zisizo rasmi zinasema mbunge wa Musoma vijijini Nimrodi Mkono ameamua kuihama CCM na ana mpango wa wa kujiunga na UKAWA japo alishashinda kwenye kura za maoni za CCM!

Kwamba muda huu vigogo wa CCM akina mzee Msekwa wanamsihi asitekeleze maamuzi hayo,pia amegoma kuongea na mwenyekiti wa CCM,sababu ya msingi ni kwamba amechoshwa kuongozwa na watu wajinga wenye majungu muda wote! .

Nilimwuuliza mnenaji kwamba itakuwaje kuhusu ubunge ukizingatia muda wa kura za maoni za ubunge zimekwisha? Akasema ubunge sio kitu kwake!! Bali anataka heshima!

Naomba mwenye uhakika juu ya jambo hili.
 
Jua yule ni CCM na wala haami ng'ooooo. Kapita jimbo jipya la butiama.
 
mwambiae karibu kwenye meli ya nuhu ya ukombozi
 
Nasikia amepigiwa Simu aende ikulu kachomoa wazee wanahaha na mpaka sasa wanaendelea kumshawishi asifanye hivo!
 
Hakuna hapa km vip endelea kuchunguza ulete mzigo hapa
 
Simu zinapigwa hapokei nasikia kuna waziri mmoja rafiki yake wako manyara lodge wanamikakati yao sijui ni nini.


swissme
 
Habari bado iko ndani kwa ndani wanajaribu kukaba kabla haija erupt kama volkano!
 
mbunge wangu huyu ni mtu wa vitendo sana....akiwa kwenye movement ya ukawa watafika mbali sana....karibu nimrod mkono kijana wa busegwe
 
Wadau naomba kupata uhakika na ukweli kuhusu habari hii! Habari zisizo rasmi zinasema mbunge wa Musoma vijijini Nimrodi Mkono ameamua kuihama CCM na ana mpango wa wa kujiunga na UKAWA japo alishashinda kwenye kura za maoni za CCM! Kwamba muda huu vigogo wa CCM akina mzee Msekwa wanamsihi asitekeleze maamuzi hayo,pia amegoma kuongea na mwenyekiti wa CCM,sababu ya msingi ni kwamba amechoshwa kuongozwa na watu wajinga wenye majungu muda wote! . Nilimwuuliza mnenaji kwamba itakuwaje kuhusu ubunge ukizingatia muda wa kura za maoni za ubunge zimekwisha? Akasema ubunge sio kitu kwake!! Naomba mwenye uhakika juu ya jambo hili.
akihama its good riddance. matajiri fisadi wenye kutaka uongozi ndio wanayumbisha ccm. magamba yanajibandua mmoja baada ya mwingine kama habari hii ikiwa kweli. ccm irejee kua chama cha wavuja jasho badala ya pango la walanguzi.
 
Kwani kulikuwa na tetesi za kukatwa maana mwenye chama chake Nape amesema walioongoza wameongoza huko huko maamuzi bado, kama mganga wake amemwambia atakatwa asepe kungali mchana maana kuna giza mbele
 
Back
Top Bottom