Malaria Sugu
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 2,653
- 270
Mheshimiwa BuLJi kutogombea Ubunge 2015!
Mheshimiwa Mbunge Shah(Bulji) amefunguka na kusema kwamba hatogombea tena nafasi hiyo kwa kipindi cha nne mfululizo! Ameamua hivyo ili kupisha wadau wengine wajitokeze na kutoa mchango wao katika kuleta maendeleo zaidi kisiwani humo! Hata hivyo ameeleza masikitiko yake ya kushindwa kuleta mabadiliko makubwa kwa mda mrefu tangu aingie madarakani miaka 12 sasa!
Kati ya mambo ambayo mbunge yamemhuzunisha ni juu ya kutoweza kufanikiwa kukamilika hata mradi mmoja kati ya ile aliyoiahidi tangu kipindi chake cha kwanza alipokuwa anaingia kuchukua nafasi hiyo!
Miradi hiyo ni pamoja na, kutokuwepo kwa usafiri wa uhakika wa majini kwa wakazi wa kisiwa hicho, kutokamilika na kutokuwa na majibu ya uhakika juu ya mradi wa gati, kutojulikana kwa uhakika ni lini bara bara za mafia zitajengwa, kutokamilia kwa mradi wa Uwanja wa ndege kama ilivyoahidiwa kwa mara ya kwanza mradi ambao unafadhiliwa na MCA, kushindwa kusimamia Ilani ya ccm kutekeleza miradi mbali mbali kisiwani humo kwa vipindi vyake vyote vya uongozi, ikiwepo ile ya kujengwa kwa Chuo cha ufundi kwa kila wilaya, na shule angalau moja yenye A-Level, na mengine mengi
Kutangaza Mapema kwa mh bulj kujiondoa ktk kinyanganyiro hichi kunatokana na vijana kadhaa wasomi kuonyesha mwelekeo wa kugombea ubunge kupitia vyama mbali mbali. tayari mijadala mikali kupitia face book imeanza kumuweka pabya Mh Bulj
SOURCE: Kisiwa chetu cha Mafia face book