Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Bakari Shingo, amejiondoa katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi za uwakilishi wa Tanzania kwenye taasisi muhimu za kimataifa za mabunge baada ya kushindwa kukidhi kigezo cha umahiri wa lugha ya Kiingereza wakati wa mchakato wa uteuzi.
Uchaguzi huo ulifanyika ili kupata wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika (Pan-African Parliament), Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) pamoja na Jukwaa la Mabunge ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Nafasi hizo zilikuwa wazi kufuatia kumalizika kwa muda wa Bunge la 12, hivyo kulazimu kufanyika kwa kura mpya za kuteua wajumbe wapya.
Hata hivyo, Mbunge huyo wa Ukonga alishindwa kuendelea na mchakato wa kuwania nafasi hizo baada ya tathmini ya lugha kuthibitisha kuwa hakukidhi kiwango kinachohitajika cha umahiri wa Kiingereza, ambacho ni sharti muhimu kwa ushiriki katika vikao na shughuli za mabunge hayo ya kimataifa.