Mbunge wa jimbo la Tanga kwa tiketi ya CUF akamatwa tena na Polisi kwa kutoa maneno ya uchochezi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
tanga22.jpg

Mbunge wa jimbo la Tanga kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF chini ya umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) Mheshimiwa Mussa Mbaruk amekamatwa na jeshi la polisi kisha kufikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tanga kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi na chuki kwa jamii.

Akisoma shtaka linalomkabili Mheshimiwa Mbaruk mwanasheria wa serikali Saraji Iboru amedai mahakamani hapo mbele ya kaimu hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Hilda Lyatuu kuwa Agosti 13 mwaka huu katika eneo la madina lililopo kata ya Msambweni jijini Tanga Mussa Mbaruk alitamka maneno ya uchochezi na chuki kwa jamii hatua ambayo ingeweza kuhamasisha vitendo vya uvunjifu wa amani.

Akinukuu vipengele vya sheria kuhusu shtaka hilo mwanasheria wa mtuhumiwa Warehema Kibaha aliiomba mahakama hiyo impe dhamana mteja wake huku shauri hilo likiendelea kusikilizwa.

Kwa kuzingatia ombi hilo kaimu hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Hilda Lyatuu amemtaka mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja awe na shilingi milioni 3 na mmoja wapo kati ya hao awe ni mtumishi wa umma masharti ambayo yalitekelezwa na kuachiwa huru hadi shtaka lake litakapo tajwa tena kesho Agosti 23 mwaka huu.

Chanzo: ITV

=========

UPDATES:

Mbunge kizimbani kwa maneno ya uchochezi

MBUNGE wa Jimbo la Tanga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mussa Mbarouk amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tanga kujibu shitaka la kutoa maneno ya uchochezi.

Mbunge huyo alifikishwa mahakamani hapo saa 8.30 alasiri jana akiambatana na jopo la mawakili wake wakiongozwa na Warehema Kibaha.

Mbele ya Kaimu Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Hilda Lyatuu Wakili wa Serikali, Saraji Iboru alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 13, mwaka huu.

Iboru alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kutoa maneno ya uchochezi wakati akiwa katika mtaa wa Madina jijini Tanga majira ya saa 10 jioni alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara.

Wakili Siraji akiwa na mwanasheria mwenzake wa Serikali, Shose Naiman aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa katika mkutano huo, Mbunge huyo alisema Mapango ya Amboni yanatumika kwenda kuwaua vijana.

Mshitakiwa huyo alikana shitaka hilo na mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi leo ili kutoa nafasi kwa upande wa mashtaka na mshitakiwa kukamilisha taratibu za kupata watu watakaokidhi masharti ya dhamana ambayo yamewekwa na mahakama.

Hata hivyo, Mbunge Mbarouk pamoja na mambo mengine leo atatakiwa kuripoti mahakamani hapo akiwa ameambatana na watu wawili ambao ni watumishi wa serikali ambao ndio watakuwa na sifa ya kumdhamini katika shitaka hilo.
 
Mbunge wa jimbo la Tanga kwa tiketi ya CUF akamatwa na polisi kwa kutoa maneno ya uchochezi.

Mbunge wa jimbo la Tanga kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF chini ya umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) Mheshimiwa Mussa Mbaruk amekamatwa na jeshi la polisi kisha kufikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tanga kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi na chuki kwa jamii.
Akisoma shtaka linalomkabili Mheshimiwa Mbaruk mwanasheria wa serikali Saraji Iboru amedai mahakamani hapo mbele ya kaimu hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Hilda Lyatuu kuwa Agosti 13 mwaka huu katika eneo la madina lililopo kata ya Msambweni jijini Tanga Mussa Mbaruk alitamka maneno ya uchochezi na chuki kwa jamii hatua ambayo ingeweza kuhamasisha vitendo vya uvunjifu wa amani.

Akinukuu vipengele vya sheria kuhusu shtaka hilo mwanasheria wa mtuhumiwa Warehema Kibaha aliiomba mahakama hiyo impe dhamana mteja wake huku shauri hilo likiendelea kusikilizwa.

Kwa kuzingatia ombi hilo kaimu hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Hilda Lyatuu amemtaka mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja awe na shilingi milioni 3 na mmoja wapo kati ya hao awe ni mtumishi wa umma masharti ambayo yalitekelezwa na kuachiwa huru hadi shtaka lake litakapo tajwa tena kesho Agosti 23 mwaka huu.
 
Sijapata kuona kiongozi mwoga asiyependa kukosolewa kama mtukufu baba jesca.

Tutaupinga udikteta uchwara kila mahali
 
Shida ni Lowassa,wamwachie mbunge wa watu.
Wanamwogopa Lowassa kwa madhila waliyomfanyia.
 
Serikali itoe kitabu chenye misamiati yote yenye maana ya uchochezi ili wananchi wayafahau, wawe salama na mkono wa sheria.
 
Mbunge kizimbani kwa maneno ya uchochezi

MBUNGE wa Jimbo la Tanga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mussa Mbarouk amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tanga kujibu shitaka la kutoa maneno ya uchochezi.

Mbunge huyo alifikishwa mahakamani hapo saa 8.30 alasiri jana akiambatana na jopo la mawakili wake wakiongozwa na Warehema Kibaha.

Mbele ya Kaimu Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Hilda Lyatuu Wakili wa Serikali, Saraji Iboru alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 13, mwaka huu.

Iboru alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kutoa maneno ya uchochezi wakati akiwa katika mtaa wa Madina jijini Tanga majira ya saa 10 jioni alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara.

Wakili Siraji akiwa na mwanasheria mwenzake wa Serikali, Shose Naiman aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa katika mkutano huo, Mbunge huyo alisema Mapango ya Amboni yanatumika kwenda kuwaua vijana.

Mshitakiwa huyo alikana shitaka hilo na mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi leo ili kutoa nafasi kwa upande wa mashtaka na mshitakiwa kukamilisha taratibu za kupata watu watakaokidhi masharti ya dhamana ambayo yamewekwa na mahakama.

Hata hivyo, Mbunge Mbarouk pamoja na mambo mengine leo atatakiwa kuripoti mahakamani hapo akiwa ameambatana na watu wawili ambao ni watumishi wa serikali ambao ndio watakuwa na sifa ya kumdhamini katika shitaka hilo.
 
Mimi lazima niandamane tarehe 1 sep na lazima nimpasue mtu mjinga mjinga hasa hasa namtaka yule RPC na RC
 
Back
Top Bottom