Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Msigwa akamatwa na Jeshi la Polisi na kupelekwa mahabusu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Jioni hii Mbunge wa Iringa Mjini REV.Msigwa amekamatwa na Polisi akiwa Iringa Mjini na mpaka sasa yupo Mahabusu, na huenda akalala Mahabusu.

=======

JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa kwa mahojiano kutokana na matukio ya kiuharifu yanayotokea mjini Iringa .

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa (RPC) Julius Mjengi ameuthibitishia mtandao huu usiku huu baada ya kupigiwa simu kuhusiana na kuzagaa kwa taarifa za kukamatwa kwa mbunge Msigwa katika mitandao ya kijamii .

Kamanda huyo amesema kuwa ni kweli hadi majira ya saa8.25 usiku huu alikuwa akihojiwa juu ya matukio ya uvunjwaji wa nyumba ya aliyekuwa diwani wa kata ya Mwangata kupitia chadema aliyejiuzulu na kujiunga na CCM pamoja na tukio la kuchomwa moto kwa nyumba aliyokuwa akiishi katibu wa UVCCM Iringa mjini .

" Bado tunaendelea kumhoji na ni kweli amekamatwa tupo naye tunaendelea kumhoji "

Chanzo: Mtandao ya Kijamii

UPDATES:

Mbunge wa Iringa Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mch. Peter Msigwa ambaye alikamatwa na Polisi tarehe 22/01/2018 na kushikiliwa kwenye kituo cha Polisi Kati Iringa Mjini, ameachiwa kwa dhamana usiku baada ya kukaa mahabusu kwa masaa kadhaa.
 
Leo Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za uchochezi katika mahakama ya Mkoa wa Mbeya na amenyimwa tena dhamana pamoja na ukweli kuwa kosa analotuhumiwa nalo lina dhaminika kwa mujibu wa sheria zetu, hivyo atalala tena Magereza leo.

Jioni hii Mbunge wa Iringa Mjini REV.Msigwa amekamatwa na Polisi akiwa Iringa Mjini na mpaka sasa yupo Mahabusu, na huenda akalala Mahabusu.
Hizi taarifa zinauzi na kuumiza sana, zinataka kuleta taswira kwamba kuwa mpinzani kwenye nchi hii ni sawa na kuwa mhaini, heshima na utu wako wote unakuwa mashakani. Ila yanamwisho.
 
Hizi taarifa zinauzi na kuumiza sana, zinataka kuleta taswira kwamba kuwa mpinzani kwenye nchi hii ni sawa na kuwa mhaini, heshima na utu wako wote unakuwa mashakani. Ila yanamwisho.

Mwisho wa hayo ya kulala Mahabusu ni kubadilika

Tangu Lema kuacha Matusi kalala Tena Mahabusu ?
 
Back
Top Bottom