Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Msigwa akamatwa na Jeshi la Polisi na kupelekwa mahabusu

Msigwa ni Maarufu tu lakini mpaka sasa watu zaidi ya kumi wako mahabusu kwa zaidi ya wiki sasa bila ya kupelekwa mahakamani.

Sasa naelewa ni kwa nini Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi.
Safi sana kila mara mnadai polisi wachunguze tukio la Lissu kupigwa risasi naona umeshapata majibu. Waambie polisi waache kuhangaika na dereva waje kwako maana ni verified user.
cc kamanda Sirro.
 
Jimbo la Katalonya kule Spain nao Viongozi wao wamewekwa ndani kwa Muda mrefu, ukifanya Demokrasia bila ya adabu lazima ufundishwe Siasa za kistaarabu
Katalonya walihadaiwa na uhuni wa kisiasa, waungwana wakatibua mbinu chafu hizo...muda haupo mbali tutashuhudia utitiri wa mende kumalizika kwa kuukosa uchafu
 
Mwisho wa hayo ya kulala Mahabusu ni kubadilika

Tangu Lema kuacha Matusi kalala Tena Mahabusu ?
Kuna movie hapa naangalia, kuna jinga lina kichwa kikubwa linajipendekeza kila sehemu bila kujali, ndo wewe?
 
Jimbo la Katalonya kule Spain nao Viongozi wao wamewekwa ndani kwa Muda mrefu, ukifanya Demokrasia bila ya adabu lazima ufundishwe Siasa za kistaarabu
Acha uongo mjomba. .ishu ya uhispania tofauti na haya mambo yetu ya bongo.
 
Acha uongo mjomba. .ishu ya uhispania tofauti na haya mambo yetu ya bongo.

Uongo uko wapi?
Mmesahau waliokuwa wanataka kujitenga Zanzibar mlikuwa mnasema waachwe ni haki Yao ya kidemokrasia Mbona Catalonya wanawasweka ndani au mnajisahaulisha?
 
Jioni hii Mbunge wa Iringa Mjini REV.Msigwa amekamatwa na Polisi akiwa Iringa Mjini na mpaka sasa yupo Mahabusu, na huenda akalala Mahabusu.

=======

JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa kwa mahojiano kutokana na matukio ya kiuharifu yanayotokea mjini Iringa .

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa (RPC) Julius Mjengi ameuthibitishia mtandao huu usiku huu baada ya kupigiwa simu kuhusiana na kuzagaa kwa taarifa za kukamatwa kwa mbunge Msigwa katika mitandao ya kijamii .

Kamanda huyo amesema kuwa ni kweli hadi majira ya saa8.25 usiku huu alikuwa akihojiwa juu ya matukio ya uvunjwaji wa nyumba ya aliyekuwa diwani wa kata ya Mwangata kupitia chadema aliyejiuzulu na kujiunga na CCM pamoja na tukio la kuchomwa moto kwa nyumba aliyokuwa akiishi katibu wa UVCCM Iringa mjini .

" Bado tunaendelea kumhoji na ni kweli amekamatwa tupo naye tunaendelea kumhoji "
Mbona Chadema wanakubali kunyanyaswa kijinga namna hii ?
 
Polisi hawakamati mtu tu bila sababu maana kama hivyo tusinge lala na wakezetu nyubani maana ingekuwa ukikutana na polisi tu unakamatwa, mleta mada sema kafanya nini?
Mleta mada kasema amekamatwa kwa matukio mawili yaliyotokea wiki za nyuma ya kuchomewa na kuvunjiwa nyuma kwa kiongozi wa ccm na huyo aliyehamia ccm kutoka chadema. Kumbuka kuna watu walikamatwa wakihusishwa na matukio hayo na bado wanashikiliwa kwa upelelezi zaidi, sasa huwezi jua labda Msigwa ametajwa na watuhumiwa hao. Jeshi la polisi sio wajinga wamkamate tu mtu bila sababu ya msingi
 
Jioni hii Mbunge wa Iringa Mjini REV.Msigwa amekamatwa na Polisi akiwa Iringa Mjini na mpaka sasa yupo Mahabusu, na huenda akalala Mahabusu.

=======

JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa kwa mahojiano kutokana na matukio ya kiuharifu yanayotokea mjini Iringa .

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa (RPC) Julius Mjengi ameuthibitishia mtandao huu usiku huu baada ya kupigiwa simu kuhusiana na kuzagaa kwa taarifa za kukamatwa kwa mbunge Msigwa katika mitandao ya kijamii .

Kamanda huyo amesema kuwa ni kweli hadi majira ya saa8.25 usiku huu alikuwa akihojiwa juu ya matukio ya uvunjwaji wa nyumba ya aliyekuwa diwani wa kata ya Mwangata kupitia chadema aliyejiuzulu na kujiunga na CCM pamoja na tukio la kuchomwa moto kwa nyumba aliyokuwa akiishi katibu wa UVCCM Iringa mjini .

" Bado tunaendelea kumhoji na ni kweli amekamatwa tupo naye tunaendelea kumhoji "
Hii kali! Mbona wauwaji wa Alohonce Mawazo hawajakamatwa?

Na yale mauwaji ya viongozi wa chadema huko Arusha?

Wamethibitisha kwamba kiongozi wa chadema akipata madhara, ni ccm na serikali yake wako responsible
 
Back
Top Bottom