Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,936
Shule hizo ni 4. MARIANI GIRLS, 5. MARIANI BOYS na 6. ST ALOYSIUS GIRLS. Shule hizi zipo zinamilikiwa na KANISA KATOLIKI ambapo zinatoza ada kubwa sana kiasi kwamba wazazi wengi wa Chalinze na Pwani kwa ujumla hawawezi kusomesha watoto wao pale.
Aloshiba hamjui mwenye njaa. Sidhani kama Ridhiwani anaweza kumpeleka mtoto wake shule yoyote ya kata, masikini watoto wetu hatujui mbele yao.
Kufeli kwa shule za kata ilibidi iwe changamoto kwa mbunge huyo ili ajipange cha kuongea kwenye bunge lililoanza leo.
Ameshindwa kuonesha uzalendo hata kwa shule ya VIPAJI MAALUM Kibaha Boys ambayo inakufa kutokana na sera mbovu ya elimu. Nakumbuka mtoto wa Kikwete wakati huo ni RAIS alipelekwa Kibaha kwa mbwembwe lakini akahamishwa na kupelekwa shule ya mamilioni.
Haya bhana, Juzi Kigwangallah katutusi, leo nawe tumetusiwa sie watoto wa masikini ambao ndio wapiga kura wakubwa.