Mbunge wa Chadema afungua Matawi

Mbunge wa Chadema afungua Matawi

KITANGE

Senior Member
Joined
Apr 12, 2013
Posts
138
Reaction score
42
Mbunge wa Viti Maalum Mh. Conchesta Rwamulaza - CHADEMA leo hii jioni amefungua matawi ya chama hicho kwenye Kata za Rubafu na Kishanje zilizopo jimbo la uchaguzi Bukoba Vijijini
Pamoja na mvua kubwa iliyonyesha kuanzia asubuhi wanachama wa CHADEMA wa kijiji Katale kilichoko Kata Rubafu walihudhuria kwa wingi na kuwapongeza viongozi walioambatana na Mbunge, Kamanda IKENGYA na viongozi wa chama wa Kata hizo kwa kuvunja mwiko wa CCM ambayo kwa miaka 50 haijawahi kuwa na ofisi rasmi ya Tawi.
Katika Kijiji cha Kishanje mkutano mkubwa zaidi ya wanachama na wananchi mia sita walijitokeza kwenye mkutano huo ambapo ofisi ya Tawi ilifunguliwa na viongozi Mbunge pia viongozi walihutubia.
Kwa miaka yote ya utawala wa CCM kati ya vijiji 16 vilivyopo kwenye Tarafa Bugabo ni vijiji viwili vyenye ofisi za CCM za matawi vijiji vingine ofisi za watendaji ndizo hugeuzwa ofisi za CCM.
CHADEMA wameonyesha njia na kukubaliwa kwa wananchi wanyonge wa vijijini, wamechoka na CCM wanataka ukombolewa, mkombozi wao ni CHADEMA.
Kata za Kishanje na Rubafu zimekamilisha zoezi la ufunguzi wa matawi kwenye Vijiji vyao, vijiji vyote sita vimefungua matawi Kyamalange, Katale na Rubafu (Kata Rubafu) Bushasha, Bumai na Kishanje (Kata Kishanje)

Muda huu tupo njiani tunarudi mjini Bukoba.
 
huyo mama ni mchapa kazi na kumbuka harakati zake kabla hajawa mbunge mwaka.2008 katika uchaguzi mdogo tulikuwa nae bihalamro kwa dk.mbasa huyo ni kamanda wa ukweli namkubali
 
...mchakamchaka mpaka walie machozi,tunapiga mahakamani,tumewachapa kwenye katiba,na tunawachapa majimboni...
 
Tutafika tulikolenga tu, kikubwa kumtanguliza Mungu
 
wakati wao wanahangaika na warioba , sisi tunasonga mbele .
 
Hiyo ndiyo dawa tunawahitaji na huku Kata ya Kyengege, Kinampanda na Ulemo. CDM mnapendwa na watu wako tayari kuwaunga mkono hoja zenu zinatija. Ng'oa mizizi ya CCM zama hadi wanayoita mashina samabaratisha kabisa.

HOJA ZENYE TIJA ZA CHADEMA + ONGEZEKO LA UELEWA WA WANANCHI + MGOMEA WA CCM LOWASSA= CHADEMA CHAMA TAWALA
 
Back
Top Bottom