Ta Kamugisha
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 3,536
- 2,187
Uyu mama kinachomponza ni mikopo aliyotoa kwa kina mama ya VIKOBA, wakina mama waliichukua hii mikopo wakishangilia ila kwa sasa imewatokea puani, wanadaiwa na wameshindwa kuirudisha, wanasakwa kila kona na wengine wamekimbia nyumba zao. Hii kitu imepelekea vijana wengi kumchukia uyu mama maana mama zao wanashindwa hata kulima kisa MIKOPO. Hawataki hata kumwona huyu mama. Nakwambia kwasasa hata akisimama mpiga debe anachukua hili jimbo. MISENYI ndo HOME KWETU, tunajuta kumchagua uyu mama ingawa kula zote alizipata toka kwa akina MAMA ambao hivi sasa wamemgeuka.