Mbunge wa CCM azomewa Igunga

Duh hii kali naona wananchi wakireact watawala husingizia cdm. Nadhani hawataamini macho yao pale watakapo fanya kweli. Naomba MUNGU niwepo siku hiyo.
 
Atakuwa na wakati mgumu sana wa kuwatumikia wananchi wake kama hakubaliki namshauri afanyie kazi PR yake, kwa kuanzia nakushari uhamishie maisha yako igunga, kumbuka 2015 mwigulu mchemba hatakuwepo utakufa peke yako. KAZI KWAKO
 
Anapata mshahara wa wizi.
Kama ni hasira za kushindwa basi asubiri aitakapowaishia.
Sijui ni lini.
 
kuzomewa kwa wana wa magamba ni jambo la kawaida.Wakati wananchi wa Shinyanga walipofanya maandamano ya kupinga ongezeko la mfumuko wa bei wanamagamba walikuwa na kikao kwenye ukumbi maarufu mkoani humo hujulikanao kama NSSF,wajumbe wa mkutano huo walificha magwanda yao ya kijani kwa aibu na kwenda kuyavalia ukumbini.Si hapo tu hata wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa kata ya Masekelo mama Kilango Marecela naye aliingia aibu ya mwaka kwa kukimbiwa kwenye mkutano na kundi kubwa la wakazi wa kata hiyo na kulazimika mkutano wake kufungwa muda wa saa kumi na moja.Hali hiyo ilipelekea mh.Ole Sendeka naye kuvunja ratiba ya kuja kukisaidia chama chake kwa kusoma alama za nyakati na kuacha kuja kama ratiba ilivyokwisha kutajwa hapo awali,Shame on them scars
 
na Abdallah Ramadhan, Igunga | Tanzania Daima

MBUNGE wa Igunga, Dk. Dallali Kafumu, alisababisha kuvunjika kwa vikao viwili vya kujadili muswada wa upatikanaji wa Katiba mpya baada ya kuzomewa na wakazi wa jimbo lake kila alipozungumza. Kwa mara ya kwanza Januari 9 mwaka huu Dk. Kafumu alishindwa kuendelea kuchangia muswada wa Katiba mpya baada ya kupanda jukwaani kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mahali ambapo wananchi walikusanyika ili kutoa maoni yao.

Muda mfupi baada ya kupanda jukwaani na kujitambulisha kuwa ni mbunge wao, wananchi hao waliaza kunong’ona wakisema hawamtambui huku wakimzomea na kuondoka uwanjani hapo hali iliyosababisha kuvunjika kwa mkutano huo.

Dk. Kafumu alikumbwa na zomeazomea nyingine Januari 14, 2012 kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya St. Margreth ambapo wananchi zaidi ya robo tatu waliohudhuria mkutano huo waliondoka huku wakizomea na kuonyesha vidole viwili alama inayotumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

“Huo mkutano utausikiliza mwenyewe sisi hatukutambui, umechaguliwa na nani? Sio mbunge wetu wewe,” zilisikiza sauti za wananchi hao sambamba na kuzomea huku wakitoka nje ya ukumbi huo wa shule.

Mkutano huo ulioongozwa na Adam Robert kutoka Dar es Salaam ulivunjika tena baada ya mbunge huyo aliyechaguliwa Oktoba 2 mwaka jana kuchukua kipaza sauti na kujitambulisha kuwa ni mbunge wao.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano Dar es Salaam jana Dk. Kafumu alikiri kutokea na zomeazomea hizo akidai kuwa ni vijana waliotumwa na CHADEMA ili kufanya fujo kwenye mikutano yake huku akisisitiza kwamba jambo hilo ni hasira za kisiasa.

“Niliitwa kama mbunge wa Igunga kwenda kushiriki mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba mpya…kwa vile ni mwakilishi wao; nilikubali kuahirisha mikutano yangu ya vijijini nikaenda kushiriki.

“Ni vijana wa CHADEMA walikuwa kama robo tu ya waliohudhuria mkutano ule wakaamua kususia wakatoka nje; naona bado wana hasira ya kushindwa… nilipopewa nafasi ya kujitambulisha kwa ajili ya kufunga mkutano huo wakainuka vijana wakionyesha alama ya CHADEMA wakatoka nje lakini mkutano uliendelea.

“…Nikawaambia wana Igunga mambo ya kisiasa yamekwisha uchaguzi umeisha mbunge amepatikana tufanye kazi kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa sababu shughuli za maendeleo kwa jimbo letu hazina chama, rika wala jinsia na wananchi wamepewa nafasi ya kuchangia muswada wa Katiba, wafanye hivyo bila kuangalia itikadi za kisiasa,” alisema mbunge huyo aliyevaa viatu vya Rostam Aziz.

Baadhi ya wananchi walikuwepo kwenye mkutano huo waliliambia gazeti hili kwamba ushindi wa Dk. Kafumu uligubikwa na hila hivyo sio mbunge halali na kwamba hawataki kuongozwa naye.

Kabla ya kuvunjika kwa mikutano hiyo, wananchi wa Igunga walitaka kipengele cha madaraka ya Rais kipunguzwe kwa kuwa ni mkuu wa nchi anaweza kutoa uamuzi kwa upendeleo na kuleta mgawanyiko.

Hata hivyo zipo taarifa kwamba mbunge huyo alitoa fedha kwa baadhi ya waandishi waliokuwepo uwanjani hapo ili kuwazuia wasiandike habari ya kuzomewa kwa maelezo kwamba itamchafulia sifa na heshima yake kwa jamii.

May take: Makupe humng'ang'ania mpaka machinjioni! Mwaka huu magamba mnalo tutajenga majosho ya kuogeshea ng'ombe kwa wingi (yaani wananchi mnaowachakachua kura zao kuwazomea na kuwakataa).

Mwanjerwa kazowewa cdm kafumu nk cdm. Kesho watasema cdm imewatuma mafisadi wa lichimondi,epa,kagoda,kiwila nk kuiba ccm wakifanya kosa watasema cdm wamesababisha tufanye makosa hayo yote yanaonye uchovu wa ccm
 
si kuna sheria inakataza kujadili katiba nje ya tume ya katibai?
je rais ameshateua tume ya katiba?
je ni wangapi wameshatiwa hatiani na hiyo sheria?
au haijaanza kutumika?


Ccm haijui ifanye nini iache nini, watakoma kuringa!
Labda Sheria hiyo haiwahusu wao, na pengine inawalenga watu fulani kama vile jukwaa la katiba, au Wazee wa magwanda ambao watakapo jaribu tu
kuhamasisha wananchi utaona ile sheria inavyotumika.
Mi sijasikia kama rais ameshatangaza tume ya kukusanya maoni juu ya katiba mpya.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom