Mbunge wa CCM adai kuwa tatizo la umeme ni la kutengenezwa; anao ushahidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge wa CCM adai kuwa tatizo la umeme ni la kutengenezwa; anao ushahidi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Jul 28, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  Na Sharon Sauwa
  28th July 2011

  Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, amesema tatizo la umeme ni la kutengenezwa kwani anao ushahidi unaoonyesha kuwa Wizara ya Nishati na Madini inapinga na haitaki kuendeleza miradi ya Liganga na Mchuchuma kwa ajili ya kuendeleza nishati hiyo.

  "Mhesimiwa Mwenyekiti, tatizo la umeme ni tatizo la kutengenezwa. Viashiria vyote vinaonyesha kuwa kuna watu wachache wananufaika serikalini na hilo tatizo.

  Kwa mfano, kamati yangu ya Hesabu ya Mashirika ya Umma, ina ushahidi kwamba, Wizara ya Nishati na Madini inapinga na haitaki kuendeleza miradi hii ya Liganga na Mchuchuma," alisema.

  Aliongeza: "Kwenye Kamati yangu ya Bunge tumeshamwita Katibu Mkuu aliyepita David Jairo ushahidi wake tunao na barua yake tunayo. Nataka Mheshimiwa Waziri atuthibitishie Bunge Watanzania tumechoka na megawati. Watanzania tunataka umeme."

  Alimtaka athibitishe kuwa wizara yake iko tayari katika kutekeleza miradi ya Liganga na Mchuchuma.

  Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, alisema madai ya Filikunjombe kwamba kamati ina ushahidi kuwa tatizo hilo ni la kutengeneza hayana ukweli.

  "Lakini naomba tuvumiliane tutakapofika kuhitimisha hoja ya wizara tumekubaliana tutakuja kwanza na mpango wa dharura ya kuondokana na tatizo hili katika kipindi kifupi kijacho, halafu na mipango mingine itatekelezwa kwa kadri, ambavyo serikali itashirikiana na wawekezaji na sekta binafsi," alisema.

  Katika swali lake la msingi, alitaka kufahamu serikali ina mkakati gani wa kutumia makaa ya mawe ya Mchuchuma, ambayo yana uwezo wa kuzalisha zaidi ya megawati 600 za umeme utakaoweza kutumiwa na wana Ludewa na Watanzania wote.

  Akijibu swali hilo, Malima alisema serikali kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), imeingia ubia na Kampuni ya Sichuan Hongda ya China kwa ajili ya kuendeleza mradi wa umeme wa Mchuchuma kwa kiwango cha megawati 600.

  Alisema mradi huo utatekelezwa katika awamu mbili; ya kwanza zitazalishwa megawati 300, ambazo zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa na kwamba, unatarajiwa kukamilika mwaka 2014/2015.

  Malima alisema miradi hiyo miwili inaendelezwa kwa pamoja kwa kutambua faida zake kwa uchumi wa nchi.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Officer2009

  Officer2009 JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Yap, hawa ndio wabunge tunao wahitaji. Keep it up!
   
 3. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  huyu si ndio mpuuzi aliyesababisha wenje atolewe nje na kuwafata wapinzani hukohuko nje hadi kidogo achapwe vibao na wenje?????hana akili huyu..kanywa maji ya bendera ya njano na kijani na wala haweki maslshi ya taifa mbele..
   
 4. n

  never JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  muda wote alikuwa wapi?
   
 5. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ndio na yeye leo amejikakamua na kuongea baada ya kuchekwa na wenzake jana...
   
 6. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,084
  Likes Received: 7,312
  Trophy Points: 280

  Wacha umagamba wewe, huyu jamaa baada ya kupewa twisheni jana kua aache kudandia treni kwa mbele, ashughulikie ya jimbo lake ndo anakurupuka kama mtu alietoka usingizini.

  Usijisifie kwa mbio, msifie anaekukimbiza
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  huyo ni chizi baada ya kusutwa kwao huko na kusutwa na akina vijaluba juzi ndio kaamka.... hana ushahidi wala nini..
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kasutwa na wenye akili jana leo kafumbuka macho alete ushahidi si kuleta tetesi tu na kutishia nyau alete data km akina wenje kafulila LEMA LISSU na si ubabaishaji km wa lukuvi
   
 9. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  mdau kachafua mazingira kaona mmeanza kudili nae kaanza kujisafisha kituko chake bado mjadala kwenye umma
   
 10. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145

  Nipashe ya Lini?
   
 11. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Mmmh ila hii wizara ina kashfa mno
   
 12. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,167
  Likes Received: 1,172
  Trophy Points: 280
  Mwisho wa yoooote:- "NAUNGA MKONO HOJA % 100". Ndo ccm walivyo,
   
 13. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Why can't mwananchinewspaper show tht pic where he's on his knees luring school kids with pent up n exhaustic magamba ideologies?
   
 14. only83

  only83 JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Tatizo hawa wabunge wa CCM hawatabiriki...hapa kasema kabisa anaoushahidi wa jambo hili...sasa subiri wakati wa kupitisha hoja,utasikia naunga mkono hoja kwa asilimia 100.Huu ni upuuzi na kuwadanganya watanzania kabisa,kwanini uunge mkono upuuzi?
   
 15. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hoja ni kwamba tatizo la umeme ni la kutengezwa na ushahidi anao mbona hatoi huo ushaidi tuuone na tujui aliye tengeza hili tatizo ni nani Mwenzake alitoa hadi barua na acc number CCM vipi

  " mara ushahidi anao kisha no verification"
   
 16. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  wala sio uongo ni ukweli maana kunaresearch nyingi tu zipo kwenye makararasi hazijafanyiwa kazi kwa mfano research yakuanzisha umeme kwenye mto Rufiji ipo lakini kwa kuwa wachache wanajua wakiwekeza ulaji uatakuwa umeisha kutokana natatizo la umeme hawawezi kukubali mimi naamini kuwa tukiwekeza kwenye mto Rufiji tutakuwa naumeme mpaka vijijini maana maporomoko yake kulingana na research yanatosheleza kuzalisha umeme wa zaidi ya 2500MW kwa hiyo sikitu kidogo lakini kutoka na wehu fulani fulani hawataki leo hii mara umeme wa gas, umeme wa utokanao na upepo, makaa ya mawe ni ukosefu wa uzalendo wala hakuna lingine.
   
 17. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #17
  Jul 29, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Angekuwa mbunge wa CHADEMA kama ilivyozoeleka lazima spika angemwambia naomba ulete huo ushahidi wako na wabunge wengi wa CCM wangeshangilia
   
 18. BILLYZ

  BILLYZ Member

  #18
  Jul 29, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ..........ifikie mahala tujifunze kumpongeza mtu anapofanya vizuri sio kupinga kila kitu itakuwa haileti tija na ndio kinachoendelea mjengoni kati ya pande mbili hata hoja ya msingi akitoa wa cdm wale wa ccm wanaipinga and vise versa tubadilike jamii tukemee uovu na kusaport yale mazuri hata kama yanatoka upande gani
  thanks
   
 19. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #19
  Jul 29, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,393
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Wabunge wengine wanatia huruma!
   
 20. N

  Njaare JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tatizo la hawa wabunge wa CCM ni pale wanapoongea mambo huku wakipuliza. Kama huyu jamaa anatokea jimbo lenye matatizo kibao ila ni bingwa sana wa kuitetea serikali. Ni bingwa wa kuuponda upinzani.

  Kwa hili suala la umeme, ni kweli kuwa ni la kutengeneza. Iweje kuzalisha umeme kutoka Stiglers Gorge kwa ajili ya matumizi ya watanzania kunakuwa na athari za kimazingira lakini kuchimba Uranium Selous na dhahabu mwanza, shinyanga na mara kwa ajili ya wazungu hakuna athari za kimazingira?

  La kushangaza sana ni kuwa serikali yetu bado inafikiria kuzalisha umeme tolka kwenye gas na mafuta na kuondokana na umeme wa maji wakati gas imeshabinafsishwa. Hii ni kwa mujibu wa hotuba ya waziri mkuu wakati akiahirisha kupitishwa kwa bajeti ya nishati na madini. Wakati huo huo tunaambiwa baadhi ya mitambo ya gas imezimwa kwa sababu hamna gas ya kutosha. Hii inamaana solution ya serikali itategemea mafuta ambayo ni ghali.

  Kuna mawili ya kujiuliza, kuachana na umeme wa maji ni suluhisho la matatizo ya umeme au ni kutengeneza ufisadi katika kununua mafuta.

  Mi nafikiri serikali itamk kuwa itapunguza kutegemea mtera na kidatu na kuhamia mito mingine.
   
Loading...