Mbunge wa CCM adai kuwa tatizo la umeme ni la kutengenezwa; anao ushahidi

Namuunga mkono mbunge Deo.Mimi sina ushahidi wowote wa maandishi,lakini jinsi tatizo hili lilivyo, inaonyesha kuna conspiracy! I AM SURE THE FREEMASONS ARE INVOLVED.THESE GUYS ARE SADISTS.
Na Sharon Sauwa
28th July 2011

Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, amesema tatizo la umeme ni la kutengenezwa kwani anao ushahidi unaoonyesha kuwa Wizara ya Nishati na Madini inapinga na haitaki kuendeleza miradi ya Liganga na Mchuchuma kwa ajili ya kuendeleza nishati hiyo.

“Mhesimiwa Mwenyekiti, tatizo la umeme ni tatizo la kutengenezwa. Viashiria vyote vinaonyesha kuwa kuna watu wachache wananufaika serikalini na hilo tatizo.

Kwa mfano, kamati yangu ya Hesabu ya Mashirika ya Umma, ina ushahidi kwamba, Wizara ya Nishati na Madini inapinga na haitaki kuendeleza miradi hii ya Liganga na Mchuchuma,” alisema.

Aliongeza: “Kwenye Kamati yangu ya Bunge tumeshamwita Katibu Mkuu aliyepita David Jairo ushahidi wake tunao na barua yake tunayo. Nataka Mheshimiwa Waziri atuthibitishie Bunge Watanzania tumechoka na megawati. Watanzania tunataka umeme.”

Alimtaka athibitishe kuwa wizara yake iko tayari katika kutekeleza miradi ya Liganga na Mchuchuma.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, alisema madai ya Filikunjombe kwamba kamati ina ushahidi kuwa tatizo hilo ni la kutengeneza hayana ukweli.

“Lakini naomba tuvumiliane tutakapofika kuhitimisha hoja ya wizara tumekubaliana tutakuja kwanza na mpango wa dharura ya kuondokana na tatizo hili katika kipindi kifupi kijacho, halafu na mipango mingine itatekelezwa kwa kadri, ambavyo serikali itashirikiana na wawekezaji na sekta binafsi,” alisema.

Katika swali lake la msingi, alitaka kufahamu serikali ina mkakati gani wa kutumia makaa ya mawe ya Mchuchuma, ambayo yana uwezo wa kuzalisha zaidi ya megawati 600 za umeme utakaoweza kutumiwa na wana Ludewa na Watanzania wote.

Akijibu swali hilo, Malima alisema serikali kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), imeingia ubia na Kampuni ya Sichuan Hongda ya China kwa ajili ya kuendeleza mradi wa umeme wa Mchuchuma kwa kiwango cha megawati 600.

Alisema mradi huo utatekelezwa katika awamu mbili; ya kwanza zitazalishwa megawati 300, ambazo zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa na kwamba, unatarajiwa kukamilika mwaka 2014/2015.

Malima alisema miradi hiyo miwili inaendelezwa kwa pamoja kwa kutambua faida zake kwa uchumi wa nchi.


CHANZO: NIPASHE
 
Taarifa, huyu si mbunge wa Ludewa ila ni mbunge wa tume ya uchaguzi na mwenyekiti wa tume, hakuna mwananchi wa ludewa aliyemchagua
 
Back
Top Bottom