PreGE2025 Mbunge wa Busega Simon Lesengekile ataka Kariakoo Dabi ibadilishwe jina na kuitwa Samia Dabi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,439
Reaction score
6,692
Wakuu,

Wale wapenzi wa soka la Tanzania, mna salamu zenu huku!

Akiwa anazungumza bungeni leo, Mbunge wa Busega, Simon Lusengekile ametaka mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Simba maarufu kama Kariakoo Dabi iliyopangwa kupigwa Juni 15, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam kuitwa “Samia Dabi”.

Soma pia: Simiyu: CCM Busega wachanga pesa kwaajili Rais Samia na Mbunge kuchukua fomu ya kugombea 2025, wengine watoa ng'ombe

“La mwisho mheshimiwa mwenyekiti ni kwamba nimemuona hapa Kaimu Waziri Mkuu Mheshimiwa Mkuchika (Kapt. George Mkuchika-anayekaimu nafasi ya Waziri Mkuu bungeni), ninaomba msimamizi wa shughuli za serikali hapa bungeni siku ya tarehe 15, 6, 2025 Dabi ya Simba na Yanga tuiite jina la Samia Dabi Kampeni,” amesema mbunge huyo.

Awali dabi hiyo ilikuwa imepangwa kufanyika Machi 8, 2025 lakini muda mchache kabla ya mchezo huo, Bodi ya Ligi Kuu Bara iliahirisha mchezo huo kwa madai kuwa Simba ilizuiwa na wanaodaiwa kuwa makomandoo wa Yanga siku moja kabla ya mchezo huo wasifanye mazoezi ya mwisho.

Huyu mpumbavu amshukuru magufuli kura za maoni alikuwa wa mwisho hapo busega..
Sasa hivi ajiandae kurudi Shirati Hospital Rorya alipokuwa mfanyakazi.
 
Back
Top Bottom