Madam Lauwrencia Masele Bukwimba, madam nakuheshimu sana ndio maana nikaamua kuandika kukukumbusha kuwa barabara katika jimbo lako ni mbovu .
Mfano barabara ya Kutoka Nyarugusu kwenda kwenu Nyabulolo kupitia s/msingi Kanyalu ni mbovu kabisa, magari yanakwama njiani kwa makorongo na mchanga uliojaa bara barani.
Fanya hima itengenezwe, pia umeme umeletwa lakini hauja pitishwa kwenda s/msingi Kanyalu kwenda Nyabulolo umekomea Nyarugusu mjini, kumbuka CCM inatekeleza mradi wa UMEME VIJIJINI (REA).
Unapocheza faulo kama hii ndio unawapa fursa wapinzani kufunga magoli maana haya matatizo ya maji,barabara na umeme ni kero kubwa kwa wananchi wa jimbo lako la Busanda. Bado unayo fursa jipange utatue kero hizi mbunge wangu.
Ningekuwa na e-mail yako ninge kutumia ila sikuwa na njia mbadala zaidi ya kutumia mtandao wa kijamii.
Kama viongozi wa kata na jimbo wanakuambia mambo safi wanakudanganya dada yangu mambo si shwari nenda ukajionee, toka Dar es salaan utaniamini ninachosema.