maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Leo hii mbunge wa jimbo la Busanda Lolensia Bukwimba amekumbwa na kizaazaa cha karne baada ya kuzomewa na wapiga kura wake mbele ya waziri mkuu.
Tukio hilo lilitokea baada ya waziri mkuu mheshimiwa Kassim Majaliwa kumuita Lolensia ili aseme neno lakini ghafla liliibuka zogo la wananchi kumzomea na kumtaka ashuke jukwaani atoke mbele yao kwa madai kwamba hakuna anachowafanyia wananchi na ubunge wake ni wa kubaka.
Kilichomwokoa mbunge ni waziri Kalemani na mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Geita Josef Musukuma kwa kuwatuliza wananchi hao vinginevyo leo wangemshusha jukwaani kwa nguvu.