Mbunge wa Arusha Lema amwomba Magufuli avunje Halmashauri ya jiji la Arusha

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
'
SAKATA la madalali kuendelea kukusanya kodi za Halmashauri ya Jiji la Arusha kutoka kwa wapangaji wa vibanda vinavyomilikiwa na jiji hilo, limezidi kuchukua sura mpya huku, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), akimwomba Rais Dk. John Magufuli kuunda tume ya uchunguzi au avunje halmashauri.

Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya hivi karibuni kikao cha Baraza la Madiwani katika Jiji la Arusha kupitisha azimio la kodi za vibanda vilivyojengwa stendi ndogo mjini Arusha kutakiwa kulipia halmashauri moja kwa moja na si kupitia madalali.

Akizungumza jana baada ya MTANZANIA kutaka kujua msimamo wa mbunge huyo kuhusu hali hiyo, Lema alisema kwa muda mrefu kumekuwa na hali ya kutoheshimiwa kwa maazimio yanayotolewa na Baraza la Madiwani jambo ambalo halileti picha nzuri kwa jamii.

Alisema jiji liliingia mkataba wa miaka 10 na waliojenga vibanda hivyo tangu mwaka 1994 na baada ya hapo vitarudi chini ya umiliki wa halmashauri ya jiji lakini tangu wakati huo hadi sasa kumekuwa na kutoelewana na Serikali imekuwa ikikosa mapato yake.

“Tunajua huenda ni mkakati maalumu unaofanywa na Mkurugenzi wa Jiji (Athuman Kihamia) kupitia Mkuu wa Mkoa wa Arusha (Mrisho Gambo).

“Ni wazi huu ni mkakati wa kudhoofisha halmashauri ambazo zipo chini ya upinzani hasa Chadema ili zionekane zimeshindwa kusimamia rasilimali ikiwemo ukusanyaji wa mapato.

“Kutokana na hali hii ninamwomba sana Rais Dk. John Magufuli, kama aliweza kuunda tume na ikachunguza suala la mchanga wa dhahabu na akawafukuza kina Acacia basi afanye hivyo na kwa jiji la Arusha na kama itaonekana vinginevyo avunje Baraza la Madiwani nasi tutarudi mtaani na kuwa madiwania wa wananchi kuliko kutoheshimiwa maamuzi ya vikao.

“Mtu amejenga kibanda miguu mitatu kwa mitano tangu mwaka 1994 anakusanya kodi je hadi leo hajarudisha fedha zake? Kuna nini kinachoendelea na kwanini madiwani wanadharauliwa? Nakuombas Rais Magufuli tupia jicho lako Arusha,” alisema Lema

Mbunge huyo alikwenda mbali na kudai kwamba wapo baadhi ya viongozi wa Serikali wamekuwa wakiandaa mikakati kwa kushirikiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yenye lengo la kudhofisha maeneo yanaongozwa na wapinzani.

“Tunaona wazi huu huenda ni mkakati wa kudhofisha upinzani kwani hata kauli ya CCM kupitia kwa Katibu Mwenezi wake, Humphrey Polepole kwamba viongozi wa Serikali kupelekwa kwenye maeneo ya upinzani. Kauli hii aliitoa akiwa Arusha na kilio chetu hiki tumekifikisha hadi kwa Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene naye anajua kila kitu,” alisema

Alisema suala la malipo hayo awali wafanyabiashara walikubaliana na uamuzi wa jiji lakini baada ya kuteuliwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Arusha ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa, Mrisho Gambo aliingia suala hilo na kumpa maagizo kwa kuwakingia kifua watu waliojenga vibanda hivyo.

Alipotafutwa Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro, ili kujua hasara walioyoitapa kutokana na kukosekana kwa kodi hiyo, aliomba atumiewe ujumbe mfupi wa simu na baada ya muda alijibu yupo kwenye kikao cha Kamati Kuu.
 
Hapo ndipo upinzani wanapofungwa kila siku. Huu ni mfano wa kujilengeshea balaa ambalo tunaona hawa Upinzani wakifanya kola siku na mwisho wake ni CCM kufanye kweli bila ajizi. Kitachotokea sasa ni kwa CCM kukubali ombi hilo la kuvunja halmashauri na kusema kuwa CDM wMeomba hivyo baada ya kushindwa kuongoza jiji kubwa kama Arusha. Itasemwa kuwa kushindwA huko ni kutokana na uchanga wa CDM.
 
Kutokana na hali hii ninamwomba sana Rais Dk. John Magufuli, kama aliweza kuunda tume na ikachunguza suala la mchanga wa dhahabu na akawafukuza kina Acacia basi afanye hivyo na kwa jiji la Arusha na kama itaonekana vinginevyo avunje Baraza la Madiwani nasi tutarudi mtaani na kuwa madiwania wa wananchi kuliko kutoheshimiwa maamuzi ya vikao.Godbless Lema
 
Inawezekana pia anategwa na upinzani kama kweli anaupiga vita ufisadi au lah.Maana akikubali kuvunja baraza la madiwani maana yake ana bariki wizi unaofanywa na wanachama wa CCM na wafanyakazi wa Halmashauri upo?
 
Hapo ndipo upinzani wanapofungwa kila siku. Huu ni mfano wa kujilengeshea balaa ambalo tunaona hawa Upinzani wakifanya kola siku na mwisho wake ni CCM kufanye kweli bila ajizi. Kitachotokea sasa ni kwa CCM kukubali ombi hilo la kuvunja halmashauri na kusema kuwa CDM wMeomba hivyo baada ya kushindwa kuongoza jiji kubwa kama Arusha. Itasemwa kuwa kushindwA huko ni kutokana na uchanga wa CDM.

Inawezekana pia anategwa na upinzani kama kweli anaupiga vita ufisadi au lah.Maana akikubali kuvunja baraza la madiwani maana yake ana bariki wizi unaofanywa na wanachama wa CCM na wafanyakazi wa Halmashauri upo?
 
IMG_20170529_152239_049.jpg
 
“Kutokana na hali hii ninamwomba sana Rais Dk. John Magufuli, kama aliweza kuunda tume na ikachunguza suala la mchanga wa dhahabu na akawafukuza kina Acacia basi afanye hivyo na kwa jiji la Arusha na kama itaonekana vinginevyo avunje Baraza la Madiwani nasi tutarudi mtaani na kuwa madiwania wa wananchi kuliko kutoheshimiwa maamuzi ya vikao.
 
SAKATA la madalali kuendelea kukusanya kodi za Halmashauri ya Jiji la Arusha kutoka kwa wapangaji wa vibanda vinavyomilikiwa na jiji hilo, limezidi kuchukua sura mpya huku, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), akimwomba Rais Dk. John Magufuli kuunda tume ya uchunguzi au avunje halmashauri.

Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya hivi karibuni kikao cha Baraza la Madiwani katika Jiji la Arusha kupitisha azimio la kodi za vibanda vilivyojengwa stendi ndogo mjini Arusha kutakiwa kulipia halmashauri moja kwa moja na si kupitia madalali.

Akizungumza jana baada ya MTANZANIA kutaka kujua msimamo wa mbunge huyo kuhusu hali hiyo, Lema alisema kwa muda mrefu kumekuwa na hali ya kutoheshimiwa kwa maazimio yanayotolewa na Baraza la Madiwani jambo ambalo halileti picha nzuri kwa jamii.

Alisema jiji liliingia mkataba wa miaka 10 na waliojenga vibanda hivyo tangu mwaka 1994 na baada ya hapo vitarudi chini ya umiliki wa halmashauri ya jiji lakini tangu wakati huo hadi sasa kumekuwa na kutoelewana na Serikali imekuwa ikikosa mapato yake.

“Tunajua huenda ni mkakati maalumu unaofanywa na Mkurugenzi wa Jiji (Athuman Kihamia) kupitia Mkuu wa Mkoa wa Arusha (Mrisho Gambo).

“Ni wazi huu ni mkakati wa kudhoofisha halmashauri ambazo zipo chini ya upinzani hasa Chadema ili zionekane zimeshindwa kusimamia rasilimali ikiwemo ukusanyaji wa mapato.

“Kutokana na hali hii ninamwomba sana Rais Dk. John Magufuli, kama aliweza kuunda tume na ikachunguza suala la mchanga wa dhahabu na akawafukuza kina Acacia basi afanye hivyo na kwa jiji la Arusha na kama itaonekana vinginevyo avunje Baraza la Madiwani nasi tutarudi mtaani na kuwa madiwania wa wananchi kuliko kutoheshimiwa maamuzi ya vikao.

“Mtu amejenga kibanda miguu mitatu kwa mitano tangu mwaka 1994 anakusanya kodi je hadi leo hajarudisha fedha zake? Kuna nini kinachoendelea na kwanini madiwani wanadharauliwa? Nakuombas Rais Magufuli tupia jicho lako Arusha,” alisema Lema

Mbunge huyo alikwenda mbali na kudai kwamba wapo baadhi ya viongozi wa Serikali wamekuwa wakiandaa mikakati kwa kushirikiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yenye lengo la kudhofisha maeneo yanaongozwa na wapinzani.

“Tunaona wazi huu huenda ni mkakati wa kudhofisha upinzani kwani hata kauli ya CCM kupitia kwa Katibu Mwenezi wake, Humphrey Polepole kwamba viongozi wa Serikali kupelekwa kwenye maeneo ya upinzani. Kauli hii aliitoa akiwa Arusha na kilio chetu hiki tumekifikisha hadi kwa Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene naye anajua kila kitu,” alisema

Alisema suala la malipo hayo awali wafanyabiashara walikubaliana na uamuzi wa jiji lakini baada ya kuteuliwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Arusha ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa, Mrisho Gambo aliingia suala hilo na kumpa maagizo kwa kuwakingia kifua watu waliojenga vibanda hivyo.

Alipotafutwa Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro, ili kujua hasara walioyoitapa kutokana na kukosekana kwa kodi hiyo, aliomba atumiewe ujumbe mfupi wa simu na baada ya muda alijibu yupo kwenye kikao cha Kamati Kuu.

Hapa ndipo nitakapoona kama kweli JPM ana nia njema na Tanzania,na kama anayo basi ataunda Tume huru kuangalia ukiukwaji wa kupokea pesa za umma,akifanya vinginevyo nitajua issue ya kupinga ulaji wa raslimali za Taifa ni changa la macho,ikija kwa wapendwa wake anawakumbatia hata pale wanapothibitika wanakula rushwa.

Na kama kweli mnaongelea umoja basi hapa ndipo nitakapoona uzalendo wako wewe rafiki yangu.Tusiangalie kwa sababu Halmashauri ni ya Chadema bali tuangalie HAKI za RAIA wetu.

Lisije la ACACIA likatokea mnaanza kuwalaumu CHADEMA
 
Kwemye mikataba ya madini mambo yalikuwa hivi pia, wapinzania walikuwa na mbinu ya kudhibiti wizi lakini watawala wakapuuza na leo hii tunaingia kwenye matatizo! Hata hili watapuuza kujionyesha eti 'ndio vidume' but time will tell!
 
Hapo ndipo upinzani wanapofungwa kila siku. Huu ni mfano wa kujilengeshea balaa ambalo tunaona hawa Upinzani wakifanya kola siku na mwisho wake ni CCM kufanye kweli bila ajizi. Kitachotokea sasa ni kwa CCM kukubali ombi hilo la kuvunja halmashauri na kusema kuwa CDM wMeomba hivyo baada ya kushindwa kuongoza jiji kubwa kama Arusha. Itasemwa kuwa kushindwA huko ni kutokana na uchanga wa CDM.
Unawashauri nini katika hilo ili wasifungwe?
 
'
SAKATA la madalali kuendelea kukusanya kodi za Halmashauri ya Jiji la Arusha kutoka kwa wapangaji wa vibanda vinavyomilikiwa na jiji hilo, limezidi kuchukua sura mpya huku, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), akimwomba Rais Dk. John Magufuli kuunda tume ya uchunguzi au avunje halmashauri.

Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya hivi karibuni kikao cha Baraza la Madiwani katika Jiji la Arusha kupitisha azimio la kodi za vibanda vilivyojengwa stendi ndogo mjini Arusha kutakiwa kulipia halmashauri moja kwa moja na si kupitia madalali.

Akizungumza jana baada ya MTANZANIA kutaka kujua msimamo wa mbunge huyo kuhusu hali hiyo, Lema alisema kwa muda mrefu kumekuwa na hali ya kutoheshimiwa kwa maazimio yanayotolewa na Baraza la Madiwani jambo ambalo halileti picha nzuri kwa jamii.

Alisema jiji liliingia mkataba wa miaka 10 na waliojenga vibanda hivyo tangu mwaka 1994 na baada ya hapo vitarudi chini ya umiliki wa halmashauri ya jiji lakini tangu wakati huo hadi sasa kumekuwa na kutoelewana na Serikali imekuwa ikikosa mapato yake.

“Tunajua huenda ni mkakati maalumu unaofanywa na Mkurugenzi wa Jiji (Athuman Kihamia) kupitia Mkuu wa Mkoa wa Arusha (Mrisho Gambo).

“Ni wazi huu ni mkakati wa kudhoofisha halmashauri ambazo zipo chini ya upinzani hasa Chadema ili zionekane zimeshindwa kusimamia rasilimali ikiwemo ukusanyaji wa mapato.

“Kutokana na hali hii ninamwomba sana Rais Dk. John Magufuli, kama aliweza kuunda tume na ikachunguza suala la mchanga wa dhahabu na akawafukuza kina Acacia basi afanye hivyo na kwa jiji la Arusha na kama itaonekana vinginevyo avunje Baraza la Madiwani nasi tutarudi mtaani na kuwa madiwania wa wananchi kuliko kutoheshimiwa maamuzi ya vikao.

“Mtu amejenga kibanda miguu mitatu kwa mitano tangu mwaka 1994 anakusanya kodi je hadi leo hajarudisha fedha zake? Kuna nini kinachoendelea na kwanini madiwani wanadharauliwa? Nakuombas Rais Magufuli tupia jicho lako Arusha,” alisema Lema

Mbunge huyo alikwenda mbali na kudai kwamba wapo baadhi ya viongozi wa Serikali wamekuwa wakiandaa mikakati kwa kushirikiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yenye lengo la kudhofisha maeneo yanaongozwa na wapinzani.

“Tunaona wazi huu huenda ni mkakati wa kudhofisha upinzani kwani hata kauli ya CCM kupitia kwa Katibu Mwenezi wake, Humphrey Polepole kwamba viongozi wa Serikali kupelekwa kwenye maeneo ya upinzani. Kauli hii aliitoa akiwa Arusha na kilio chetu hiki tumekifikisha hadi kwa Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene naye anajua kila kitu,” alisema

Alisema suala la malipo hayo awali wafanyabiashara walikubaliana na uamuzi wa jiji lakini baada ya kuteuliwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Arusha ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa, Mrisho Gambo aliingia suala hilo na kumpa maagizo kwa kuwakingia kifua watu waliojenga vibanda hivyo.

Alipotafutwa Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro, ili kujua hasara walioyoitapa kutokana na kukosekana kwa kodi hiyo, aliomba atumiewe ujumbe mfupi wa simu na baada ya muda alijibu yupo kwenye kikao cha Kamati Kuu.

Mhe Lema na Mstahiki Meya Kalisti Lazaro nawashauri itisheni baraza la madiwani la dharura na mwiteni Mkuu wa Mkoa na mwambieni Mkurugenzi mbele yake atekeleze maazimio ya baraza na akikataa pigeni kura ya kutokuwa na imani naye. Hapo uwezekano wa halmashauri kuvunjwa utakuwepo iwapo serikali itakataa kumwondoa kwani mnaweza kupitisha azimio lingine mjiuzulu wote kwani hakuna sababu ya kuwa na madiwani ambao wako kisheria lakini hawatumii nguvu walizo nazo kisheria. Tumechoka kuwa nchi ya walalamishi.
Nadhani mna ujasiri huo.
 
'
SAKATA la madalali kuendelea kukusanya kodi za Halmashauri ya Jiji la Arusha kutoka kwa wapangaji wa vibanda vinavyomilikiwa na jiji hilo, limezidi kuchukua sura mpya huku, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), akimwomba Rais Dk. John Magufuli kuunda tume ya uchunguzi au avunje halmashauri.

Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya hivi karibuni kikao cha Baraza la Madiwani katika Jiji la Arusha kupitisha azimio la kodi za vibanda vilivyojengwa stendi ndogo mjini Arusha kutakiwa kulipia halmashauri moja kwa moja na si kupitia madalali.

Akizungumza jana baada ya MTANZANIA kutaka kujua msimamo wa mbunge huyo kuhusu hali hiyo, Lema alisema kwa muda mrefu kumekuwa na hali ya kutoheshimiwa kwa maazimio yanayotolewa na Baraza la Madiwani jambo ambalo halileti picha nzuri kwa jamii.

Alisema jiji liliingia mkataba wa miaka 10 na waliojenga vibanda hivyo tangu mwaka 1994 na baada ya hapo vitarudi chini ya umiliki wa halmashauri ya jiji lakini tangu wakati huo hadi sasa kumekuwa na kutoelewana na Serikali imekuwa ikikosa mapato yake.

“Tunajua huenda ni mkakati maalumu unaofanywa na Mkurugenzi wa Jiji (Athuman Kihamia) kupitia Mkuu wa Mkoa wa Arusha (Mrisho Gambo).

“Ni wazi huu ni mkakati wa kudhoofisha halmashauri ambazo zipo chini ya upinzani hasa Chadema ili zionekane zimeshindwa kusimamia rasilimali ikiwemo ukusanyaji wa mapato.

“Kutokana na hali hii ninamwomba sana Rais Dk. John Magufuli, kama aliweza kuunda tume na ikachunguza suala la mchanga wa dhahabu na akawafukuza kina Acacia basi afanye hivyo na kwa jiji la Arusha na kama itaonekana vinginevyo avunje Baraza la Madiwani nasi tutarudi mtaani na kuwa madiwania wa wananchi kuliko kutoheshimiwa maamuzi ya vikao.

“Mtu amejenga kibanda miguu mitatu kwa mitano tangu mwaka 1994 anakusanya kodi je hadi leo hajarudisha fedha zake? Kuna nini kinachoendelea na kwanini madiwani wanadharauliwa? Nakuombas Rais Magufuli tupia jicho lako Arusha,” alisema Lema

Mbunge huyo alikwenda mbali na kudai kwamba wapo baadhi ya viongozi wa Serikali wamekuwa wakiandaa mikakati kwa kushirikiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yenye lengo la kudhofisha maeneo yanaongozwa na wapinzani.

“Tunaona wazi huu huenda ni mkakati wa kudhofisha upinzani kwani hata kauli ya CCM kupitia kwa Katibu Mwenezi wake, Humphrey Polepole kwamba viongozi wa Serikali kupelekwa kwenye maeneo ya upinzani. Kauli hii aliitoa akiwa Arusha na kilio chetu hiki tumekifikisha hadi kwa Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene naye anajua kila kitu,” alisema

Alisema suala la malipo hayo awali wafanyabiashara walikubaliana na uamuzi wa jiji lakini baada ya kuteuliwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Arusha ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa, Mrisho Gambo aliingia suala hilo na kumpa maagizo kwa kuwakingia kifua watu waliojenga vibanda hivyo.

Alipotafutwa Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro, ili kujua hasara walioyoitapa kutokana na kukosekana kwa kodi hiyo, aliomba atumiewe ujumbe mfupi wa simu na baada ya muda alijibu yupo kwenye kikao cha Kamati Kuu.
Akivunja ni cdm mmepwaya. Tatua kero aache majibu ya mkato
 
Back
Top Bottom