Mbunge wa Arumeru mashariki mbona hasomeki?(Sumari)

Aliupata ubunge kwa njia isivyo halali, kwani kila mmoja anajua kua matokeo yalitangazwa baada ya mamvi kwenda kumsaidia, kwani mtoto wake kamuoa mtoto wa mamvi. Sasa Mungu anafanyia kazi fitna na sasa anakaribia faili lake, siku sii nyingi tutaimba. ''Siii mbaliiiii''
 
Ugonjwa hauna mwenyewe, tusishangilie, tusiwaumize zaidi ndugu zake ambao wanateseka bila shaka kumhangaikia ili apone na kuendelea kuihudumia familia yake. Tusishabikie ugonjwa wa mtu kisiasa. Ilikuwa kosa la magamba kung'ang'ania kuchukua jimbo hata kwa njia ya wizi wa kura ilhali wakijua mgombea wao alikuwa mgonjwa. Tumwombee Jerry apone maradhi hayo kama ni mapenzi yake Mola ili atumikie wana Arumeru. Ikidhihirika kinyume chake, basi achaguliwe mbadala, hapo twaweza kushangilia kwani Mgombea Chadema aliyedhulumiwa haki yake, njia ya ushindi itakuwa nyeupe. Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki wape uvumilivu wana Arumeru. Mungu mpe afya Jerry S.
Hapa swala si ugonjwa wa Jerry Solomon. Hoja za wadau ni je sheria inasemaje pale mbunge mteule anaposhindwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa mwaka mzima. On top of that mbunge huyo hajaapishwa. Je nini kingetokea kama mbunge huyo angekuwa wa upinzani?
 
Hapa swala si ugonjwa wa Jerry Solomon. Hoja za wadau ni je sheria inasemaje pale mbunge mteule anaposhindwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa mwaka mzima. On top of that mbunge huyo hajaapishwa. Je nini kingetokea kama mbunge huyo angekuwa wa upinzani?

Mkuu you are very right, lakini nadhani hoja ya Dopas inakuja kutokana na mtiririko wa majadiliano.
 
Tatizo lililojitokeza huko Meru ni kina EL na nec. Wameru waliona aliyekuwa mbunge wao si tu alishindwa kutekeleza ahadi zake bali hawezi tena kuwatumikia. Wakamchagua kijana Nasar Joshua awapeleke "kaanan". NEC na EL wakalazimisha kumtangaza Jerry ambaye hata kabla ya kupiga kura, tayari alikuwa icu akipambana na "israel" mtoa roho! Kwa kuwa mpambano kati yao bado unaendelea, wameru wanaendelea kukosa uwakilishi bungeni kwasababu sheria yoyote inayomaanisha ccm kulikosa jimbo haitapewa nafasi. Maana ccm imeshatoka viungo vyote kimebaki kichwa. Kupoteza hata udiwani kwenye kata ni sawa na kung'ofoa jicho kwenye kichwa kilichobaki. Likiguswa jimbo si ndio ubongo kabisa!?
 
Ni kweli huyu Mh. alikuwa anaumwa kabla hata ya uchaguzi ilitumika pesa mingi kufanya akubalike eti kisa alikuwa naibu waziri basi wakajua wakimchagua atakuwa waziri wa fedha.Ushauri wangu angekuwa muungwana kwa wananchi wake na kodi zao akadeclare tu kuwa afya yake haimruhusu kuendelea kuwatumikia hataheshimika sana kuliko hili ambalo linaendelea.Jimbo la Arumeru mashariki kukosa mwakilishi katika bunge.
Wana Arumeru Mashariki pia muwe makini wakati mnapo chagua kwa kipindi kirefu sana mmekosa maendeleo sababu ya watu mnaowachagua ni kianzia na Major Ndosi,Prof Talala Mbise, mpaka huyu wa sasa.
 
CCM wawe waungwana hata kidogo kwa hili, maana afya ya Mzee Sumari kwa kweli ni mbaya,
wafanye utaratibu Mzee Sumari ajiuzuru, ngoma ianze upya!!
 
Mheshimiwa JSS. MB wa Arumeru anaendelea vizuri lakini kuendelea na siasa itakuwa ngumu, anahitaji mapumziko zaidi. Cha muhimu ni kuitisha uchaguzi mdogo kama Igunga na anayefaa aongoze jimbo.
 
Hapa swala si ugonjwa wa Jerry Solomon. Hoja za wadau ni je sheria inasemaje pale mbunge mteule anaposhindwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa mwaka mzima. On top of that mbunge huyo hajaapishwa. Je nini kingetokea kama mbunge huyo angekuwa wa upinzani?

Na pamoja na kutoapa unaweza kuta ameendelea kuvuta mshahara na marupurupu yote ya ubunge hadi leo! We surely don't need these thugs.
 
Ama kwel hata mimi nilishawah kujiulza maswal kama hayo! Huyu jamaa nasikia huwa haishi huku tz(arumeru) sasa cjui anaish wapi! Mi nadhani Wana arumeru(Wameru) wameshashikwa,na wajifunze kutokana na makosa. 2015 ndo hyo inakuja,je wananchi bado mtaendelea kumpa kula???

Mi nafikiri wana arumeru hawana makosa. Makosa yako kwenye katiba yetu ambayo haisemi mbunge anatakiwa kuapishwa baada ya muda gani na ukipita huo uchaguzi urudiwe. Kuna nchi raisi akiugua kiasi kushindwa kutimiza majukumu yake basi anakabidhi kwa mwingine au uchaguzi unafanyika mwingine.
 
Yani naaaajuuuuta...!kwanini nilimnyima kamanda nassari kura yangu.bt wananchi 2najifunza kwa makosa.
 
Tupeni kiundani,huyu jamaa anumwa ugonjwa upi!!!Inasikitisha sana mtu kuugua mwaka mzima na hakuna ufafanuzi kiundani kuhusiana na ugonjwa wake!!!MBONA HAPELEKWI INDIA KWA MATIBABU ZAIDI?????
 
Back
Top Bottom