Mbunge Upendo Peneza(CHADEMA) akamatwa Geita mjini, aachiwa kwa dhamana

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
Mh. Upendo Peneza mbunge wa Geita viti maalum, na Diwani wa Kata ya Kasamwa wamekamatwa jioni hii....

Wako kituo cha polisi Geita Mjini...

Sababu bado hazijajulikana. Nitawajuza kitakachojiri

=======
UPDATE:
=======

JamiiForums imefanikiwa kumpata Mhe. Upendo Peneza na amethibitisha kukamatwa na Jeshi la Polisi na amesema anatuhumiwa kutoa maneno ya uchochezi/kashfa.

Mhe. Peneza anadai alisema kuna baa la njaa na Rais ameshasema hatatoa chakula kwa watakaokumbwa na njaa.

Aidha, amesema ameambiwa kosa jingine ni kulikashifu Jeshi la Polisi kwa kudai linaonea wananchi.
 
Police state

Hivi kwa nini ccm wasiwaachie makada wao wafanye siasa pia?

Yaani wanawafungia ndani wasifanye siasa,badala yake nafasi ya makada inachukuliwa na geshi

Wawaache makada wakasimulie bombadia zilivyokuja,wakahimize kilimo na kazi za maendeleo vijijini,wafuatilie mambo ya mbolea,viwanda vidogo,sio kuwafungia ndani
 
CCM wameishiwa hoja na uwongo wa kuwaambia watu.... waliaminisha watu huyu ndo masihi alosubiriwa kwa karne kuja ibadili TZ... matokeo yamekuja kinyume... wamejawa na aibu na sidhani kama kuna mwenye uthubutu wa kuitisha mkutano wa hadhara.... wamebakia kutumia nguvu ya dola!! CCM imeishiwa pumzi.....
 
Lakini yana MWISHO!! hata HITLER alikuwa na MWISHO!!! hata utwala wa RUMI ulifika MWISHO....

MWAMBIENI MAGUFULI KUWA HAYA YOTE YANA MWISHO!!!

Hilo kila mtu analijua. hakuna kisicho na mwisho. ni Mwenyezi Mungu tuu aliyetuumba ndio hana mwisho.

Lakini hii haimaanishi tuwaache wahuni wachache wafanye wanavyotaka , eti tuu kwa sababu kuna mwisho.

UKAWA sasa hivi mmeanza tabia ya kufanya makosa halafu mnaanza kujilizaliza. Lazima muwajibike mnapoharibu. Hakuna atakayewavumilia mkiharibu. Mkumbuke mwenye dhamana ya Dola kwa sasa ni CCM, ifike sehemu muheshimu hilo.

Zizi haliwezi kuwa na mafahali wawili. huo ndio UKWELI japo mchungu.
 
Kwa hiyo kupeperusha Bendera ya CDM ni kosa??Mbona nyie mnapeperusha hizo za kwenu!Mnakera sana nyie
 
Hilo kila mtu analijua. hakuna kisicho na mwisho. ni Mwenyezi Mungu tuu aliyetuumba ndio hana mwisho.

Lakini hii haimaanishi tuwaache wahuni wachache wafanye wanavyotaka , eti tuu kwa sababu kuna mwisho.

UKAWA sasa hivi mmeanza tabia ya kufanya makosa halafu mnaanza kujilizaliza. Lazima muwajibike mnapoharibu. Hakuna atakayewavumilia mkiharibu. Mkumbuke mwenye dhamana ya Dola kwa sasa ni CCM, ifike sehemu muheshimu hilo.

Zizi haliwezi kuwa na mafahali wawili. huo ndio UKWELI japo mchungu.
Lakini yana MWISHO...... fanyeni udhalimu kwa kadiri mpendavyo ila mwisho wenu waja YU wapi GADAFI?
 
Mh. Upendo Peneza mbunge wa Geita viti maalum, na Diwani wa kata ya Kasamwa wamekamatwa jioni hii.... Wako kituo cha polisi Geita Mjini...

Sababu bado hazijajulikana. Nitawajuza kitakachojiri

Meshaambiwa fanyeni siasa za kistaarabu nyie bado mnatafuta kick za kijinga mtapiga kolabo na lema .
 
Acha kujitoa akili basi. Kwani we humjui mwenye mji ni nani.? acha wivu wa kishamba, CCM ndio wenye nchi, na hilo unalifahamu. Anayetawala Tanzania kwa sasa ni CCM, tatizo lenu UKAWA hamna adabu na hamtaki kuheshimu hilo.

Nyie mnata kila siku muonekane kana kwamba nyie ndio watawala, HAKUNA KITU KAMA HICHO. Tuacheni CCM tufanye yetu, na nyie siku mkishika nchi mtajinafasi. mbona hili ni simpo tuu wala hata halihitaji nguvu kulielewa jamani.

Kwa hulka ya binadamu hakuna Baba anayependa baba mwingine kujinafasi kwenye himaya yake. huo ni wivu wa kiasili, UKAWA msitutie majaribuni bure. Mtakuja matulaumu bila sababu.
Hakuna kwenye Katiba palipoandikwa wanayotakiwa kupeperusha Bendera ni Chama kimoja tu .Badikisheni katiba.Shida ukiona Bendera tu ya Chadema akili zinaenda kwapwani zote.
Hakuna mahali kwenye Katiba walipiandika Wapinzani siyo watanzania. Mmejaza ubongo wenye na fitina,chuki,visasi na ubaguzi.Nasema.tena Acheni upumbavu wenye usio na tija na.msidhani Tanzania ni ya wanaccm tu.Mwambie ni na Mwenyekiti wenu kwamba Tanzania haina Chama.Watanzania wote this mahali sawa sawa za kuishi na kutembea.Hakuna mahali palipoandikwa kwenye katiba wenye haki.ni CCM.

Mnajifanya kutumbua Majipu kumbe nyie wenyewe ndiyo watengeneza majipu
 
Back
Top Bottom