Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,908
- 945
WANAKIJIJI WAMEAMUA KUFUFUA MRADI WA UJENZI WA ZAHANATI YAO - MBUNGE ACHANGIA SARUJI MIFUKO MIA MBILI (200)
Kijiji cha Chimati cha Musoma Vijijini ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Makojo. Vijiji vingine ni Chitare na Makojo
Kwa muda wa miaka mingi, Kata hii yenye vijiji vitatu ilikuwa inahudumiwa na Zahanati moja tu ya Kijijini Chitare.
Utoaji wa Huduma za Afya kwenye Kata ya Makojo inaenda kubadilika kwa maboresho makubwa. Kituo cha Afya cha Kata hii kimejengwa Kijijini Makojo. Kijiji cha Chimati kimeamua kufufua mradi wa ujenzi wa Zahanati yao ulioanza Mwaka 2018 na kusimama hadi leo.
Harambee ya Mbunge wa Jimbo:
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameungana tena na Wana-Chimati kuendelea na ujenzi wa Zahanati ya Kijiji chao.
Ujenzi ulipoanza Mwaka 2018, Mbunge huyo alianza kutoa michango yake kwa kuchangia Saruji Mifuko 50.
Juzi Jumatano, 10.8.2023, Mbunge huyo, akiambatana na Kamati ya Siasa ya CCM ya Wilaya ya Musoma Vijijini, aliendesha HARAMBEE kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho.
Matokeo ya HARAMBEE ya Kijijini Chimati:
*Wanakijiji & Wazaliwa wa hapo
Saruji Mifuko 123
*Kamati ya Siasa (CCM) ya Wilaya
Saruji Mifuko 25
*Mbunge wa Jimbo
Saruji Mifuko 200
Kero na matatizo yaliyowasilishwa na wananchi wa Kata ya Makojo:
*Mbunge wa Jimbo alipokea kero na matatizo yanayowakabili wananchi, na kuyatolea majibu.
*Mwenyekiti wa Chama Wilaya, Ndugu Denis Ekwabi, na Katibu wa Chama Wilaya (CCM), Ndugu Valentine Maganga walijibu maswali yaliyoelekezwa kwenye Chama. Vlevile, walitoa elimu na ufafanuzi kwa masuala mengine yaliyoulizwa.
Jimbo la Musoma Vijijini linaendelea kuboresha utoaji wa Huduma za Afya na takwimu za sasa ni hizi hapa:
*Hospitali ya hadhi ya Wilaya:
1 (moja), imeanza kutoa huduma
*Vituo vya Afya (6)
2 vinatoa huduma
2 vinatoa huduma kwa hadhi ya Zahanati
2 ni vipya vinasubiri kufunguliwa
*Zahanati 42
24 zinatoa huduma (za Serikali)
14 zinajengwa (Wananchi & Serikali, baadhi)
4 ni za Binafsi
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha matukio mbalimbali ya tarehe 10.8.2023 ya Harambee ya Kijijini Chimati.
Tenki la maji la ujazo wa lita 75,000 (pichani) linakamilishwa ujenzi Kijijini Chimati kwa ajili ya maji ya bomba ya Kijiji hicho.
SHUKRANI:
Wananchi na Viongozi wote wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuishuruku Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupatia fedha za miradi mbalimbali ikiwemo ya Sekta ya Afya - ahsanteni sana!
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumamosi, 12.8.2023
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-08-12 at 18.10.57(2).jpeg78.8 KB · Views: 5
-
WhatsApp Image 2023-08-12 at 18.10.57(1).jpeg94.6 KB · Views: 4
-
WhatsApp Image 2023-08-12 at 18.10.57.jpeg106.5 KB · Views: 4
-
WhatsApp Image 2023-08-12 at 18.10.56(1).jpeg109.1 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-08-12 at 18.10.56.jpeg110.5 KB · Views: 2