Mbunge Mnyaa aishangaa serikali kuhusu maagizo ya Richmond

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,150
Mbunge Mnyaa aishangaa serikali kuhusu maagizo ya Richmond
Na Kizitto Noya, Bukoba

MJUMBE wa Kamati ya Bunge iliyochunguza zabuni ya kufua umeme wa dharura iliyoipa ushindi Kampuni ya Richmond, Habib Mnyaa, amesema haridhiki na kasi ya serikali katika kutekeleza mapendekezo ya Bunge kuhusu suala la Richmond


Mnyaa ambaye ni Mbunge wa Mkanyageni (CUF) aliliambia gazeti hili katika mahojiano maalum kwamba, kinachomkera zaidi ni serikali kukwepa kutekeleza pendekezo namba tatu la Bunge lililoitaka ipitie upya mikataba ya makampuni ya IPTL, Songas, Aggreko na Alston, ili kupunguza mzigo wa kuyalipa makampuni hayo zaidi ya Sh244bilioni kila mwaka, kama gharama za uwezo wa mitambo (Capacity charge).


Alisema tangu kutolewa pendekezo hilo Februari mwaka huu, serikali bado inaendelea kuyalipa makampuni hayo kiasi hicho cha fedha jambo ambalo ni hatari kwa uchumi wa taifa.


"Mimi kama mmoja wa wajumbe wa kamati ya Richmond, siridhiki na jinsi serikali inavyoshughulikia maagizo ya Bunge kuhusu Richmond kwa sababu baadhi ya vipengele muhimu havijatekelezwa," alisema.


ALisema mbali na serikali kushindwa kutekeleza pendekezo hilo pia imekwama kutekeleza pendekezo namba 20 linaloitaka kuendesha uchunguzi wenye lengo la kubaini ukweli kwamba, taarifa ya awali ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu suala hilo ilichezewa ili kuficha ukweli.


"Bunge lilipendekezo utekelezaji wa suala hilo ufanyike ndani ya miezi mitatu kuanzia Februari mwaka huu, lakini serikali ilianza kuzungumzia utekelezaji Agosti na imeanza utekelezaji kwa kuchagua vipengele rahisi na kuacha vipengele vigumu ambavyo ndivyo msingi wa matatizo," alisema.


Alisema uzembe huo wa serikali ndio unaochochea umaskini katika jamii hasa baada ya taifa kuendelea kupoteza mabilioni ya shilingi kuyalipa makampuni yanayozalisha umeme wa dharura, badala ya fedha hizo kutumika katika nyanja zingine za maendeleo.


Akichambua malipo ya kampuni moja hadi nyingine, Mnyaa alisema: "Richomond ilikuwa inalipwa Sh54.8bilioni kwa mwaka, IPTL inaendelea kulipwa Sh40.5 bilioni, Songas Sh99.6, Aggreko Sh 21.8 na kampuni ya Alston inalipwa Sh27.4," alisema.


ALisema fedha hizo ambazo jumla yake ni Sh244.1bilioni zingeweza kutumika katika mambo mengine ya maendeleo ili kulinusuru taifa na umaskini.


Akichambua matumizi mbadala ya fedha hizo aliyosema kuwa ndiyo yangechangia maendeleo, Mnyaa alisema Sh244.1bilioni zingiweza kununua matrekta 5424 na kuyagawa katika kila jimbo la uchaguzi matrekta 23.
 
Back
Top Bottom