Mbunge Lazaro Nyalandu anavyohujumu watu wake

HIGH VOLTAGE INTELLIGENCE:Mbunge wa Singida kaskazini na waziri wa zamani wa maliasili na utalii katika serikali ya awamu ya nne, Lazaro Nyalandu anatajwa kuhujumu wananchi wake jimboni kwa kujipatia fedha toka kwa wafadhili kwa kigezo cha kusomesha Wanafunzi wa Sekondari jimboni kwake jambo ambalo sio la kweli na hakuna mwanafunzi hata mmoja anayesomeshwa na mbunge huyo.

Hujuma za Mbunge huyo dhidi ya watu wake zimethibitika mapema Wiki iliyopita ambapo Msaidizi wake wa karibu aliyetajwa kwa jina la RUBEN akiambatana na wazungu 4 wa kimarekani walifika Jimboni kwa ajili ya kutembelea shule na kuwaona wanafunzi wanaolipiwa fedha na wafadhili hao ambao wanadaiwa kutoa fedha nyingi kila mwaka ili kusomesha wanafunzi wa O level na A level.

Ilikuwa ni tarehe 5/5/2017 msaidizi wa mbunge huyo alianza kupiga simu kwenye baadhi ya shule akiwapa taarifa kwamba waandae taarifa za wanafunzi wanaosomeshwa na Wamarekani kwa kuwa wapo Singida na wanahitaji kuonana na wanafunzi wanaowafadhili, Ruben ananukuliwa akitoa maelekezo kwa walimu waandae hata taarifa za kupika ili kuwapooza wazungu wale maana mbunge ndio amemtuma awalete jimboni, mambo yalizidi Kuwa magumu baada ya walimu kusimama kidete na kudai hakuna mwanafunzi hata mmoja anayesomeshwa na ofisi ya mbunge hivyo wasingeingia kwenye mtego huo wa Udanganyifu, mfano ni mwalimu wa shule mojawapo alipiga simu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri akimdokezo kuhusu mchezo huo wa mbunge Lazaro Nyalandu, Mkurugenzi aliwaonya walimu wasihusike na Udanganyifu huo.

Ruben akiambatana na wazungu 4 alifika shule ya Sekondari Ilongero mnamo siku ya Ijumaa tarehe 5/5/2017 na alionekana akiingia ofisini kwa walimu na kuzunguka zunguka shule hiyo akiwazuga wale wazungu na baadae waliondoka kuelekea Kijota kwa lengo hilohilo kutembelea wanafunzi hewa wanaosomeshwa kwa ufadhili wa wazungu hao, ni katika shule ya sekondari kijota Mkuu wa shule alipigwaa butwaa kusikia kwamba kuna wanafunzi wa shule yake wanasomeshwa na Mbunge kwa ufadhili wa wamarekani. "Hapa shuleni kwangu hakuna wanafunzi wanaosomeshwa na mbunge na hakuna taarifa za namna hiyo hapa shuleni kwangu " alisema mkuu huyo wa shule.

Kwa taarifa za uhakika toka Idara ya Elimu ni kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja anayesomeshwa na Mbunge huyo wala na wafadhili hao, inawezekana wafadhili wanatoa fedha nyingi lakini haziwafikii walengwa.

Mbunge wa Singida kaskazini kwa muda mrefu amekuwa akilalamikiwa na wananchi kwa kuwadanganya kuwasomesha wanafunzi na amekuwa hafanyi hivyo, kuna kipindi aliorodhesha majina ya wanafunzi ambao wazazi hao hawana uwezo kwa ahadi ya kusomeshwa bure na hakuwahi kutekeleza badala yake wazazi walisubiri kwa matumaini bila mafanikio na baadhi ya wanafunzi walishindwa kuendelea na masomo.

Wale wazungu wa Nyalandu waliondoka Singida siku ya Jumamosi kuelekea Arusha na ndio walewale walionekana kwenye picha za ajali ya wanafunzi wa *Lucky Vicent* waliopata ajali na kupoteza maisha.
KOSA LA NYALANDU NI KUSAIDIA WATOTO MAJERUHI WA LUCKY VICENT HUKU LEMA AKIWA ANALILIA KUONGEA BILA MSAADA WOWOTE- NYALANDU ACHANA NA HAWA CHADEMA WE CHAPA KAZI MUNGU ATAKULIPA
 
Ccm hatuna undugu nanyi fanyeni kazi msitegemee mwanaccm au chadema atawajali
 
Hapa ni polisi? Kama hoja zako Zina mashiko chukua hatua za kisheria, vinginevyo unachafua jina la mtu.
 
Sasahivi mheshimiwa anasafirisha wanafunzi waliopata ajali kwenda kutibiwa Marekani, yeye ameshikilia bango na amekuwa msemaji wa watoto hao.
Unajua uhusiano wake na wafadhili hawa?
 
Unaongea na nani mkuu.... mimi sio mtu wa mahaba kama wewe....penye sifa nasema na kasoro natoa vile vile....Kaa kwenye post acha kutoka nje ya mada....au toka kaanzishe yako....kazushiwa kipi kwa mfano kwenye post hii......acha upuuzi wewe kama unakula kwa mgongo wao shauri yako na njaa zako...
Wewe ndo una mahaba ya dhati ndugu, maana umepanic mbaya! Usipende kitonga Mzee, chapa kazi, acha umbea.
 
Mbunge muongo muongo hivi. .wanasingida wenyewe wamelala fofofo hawana hili wala lile ukija uchaguzi anatusua. Acha awakomeshe wataelewa tu.
 
Mbunge Lazaro Nyalandu anasomesha Watoto kwa pesa za wafadhili toka Marekani hilo liko wazi kabisa kwa zile familia ambazo hawajiwezi kabisa kiuchumi na wamefaulu kwenda secondary.

Mtoa mada anaweza kuwa ameamua kuanzisha mada ya uchokozi kwa mheshimiwa huyu kwasababu mahususi.
 
Elimu ya sekondari ni bure siku hizi!
 
Jimbo la sgd kaskazini halina mtu na wananchi wake wanampenda kwa umaskini wao wa fikra na uchumi. Huu mtindo wake miaka mingi alishawahi kumtelekeza mwanafunzi mtc alikuwa anamsomesha ftc mwaka 2000 au 2001 akafukuzwa chuo kwa kukosa ada. Tokea hapo nikajua huyu ni tapeli tu
Ukiwa nje ya hili jimbo n rahis kuongea ila tunaoishi hapa ndo tunajua shida zilizopo ila wananchi wameziba masikio nyalandu anawaendesha atakavyo.inakela jimbo maskini hatari.
 
Kawaida yao. Siyo yeye tu wapo wengi
 
Hii ni sawa na kwenda kuzima moto kwa jirani yako wakati nyumbani kwako unawaka pia, kama hizi tuhuma zimekuwepo toka muda wote huo halafu magufuli anang'ang'ania kuwafukuza watumishi wa umma wenye vyeti vya kugushi wakati wabunge wake ni matapeli wa kutupwa, ni aibu isiyo na kifani
 
Mleta mada acha wivu wa mbwa kumzuia mbuzi kula majani. Hao wazungu kawaleta nani kama sio yeye.
 
Mbunge Lazaro Nyalandu anasomesha Watoto kwa pesa za wafadhili toka Marekani hilo liko wazi kabisa kwa zile familia ambazo hawajiwezi kabisa kiuchumi na wamefaulu kwenda secondary.

Mtoa mada anaweza kuwa ameamua kuanzisha mada ya uchokozi kwa mheshimiwa huyu kwasababu mahususi.
Wewe nae ni jangili kama jangili mwenzio
 
Back
Top Bottom