Kanyunyu
JF-Expert Member
- May 2, 2012
- 335
- 495
HIGH VOLTAGE INTELLIGENCE:Mbunge wa Singida kaskazini na waziri wa zamani wa maliasili na utalii katika serikali ya awamu ya nne, Lazaro Nyalandu anatajwa kuhujumu wananchi wake jimboni kwa kujipatia fedha toka kwa wafadhili kwa kigezo cha kusomesha Wanafunzi wa Sekondari jimboni kwake jambo ambalo sio la kweli na hakuna mwanafunzi hata mmoja anayesomeshwa na mbunge huyo.
Hujuma za Mbunge huyo dhidi ya watu wake zimethibitika mapema Wiki iliyopita ambapo Msaidizi wake wa karibu aliyetajwa kwa jina la RUBEN akiambatana na wazungu 4 wa kimarekani walifika Jimboni kwa ajili ya kutembelea shule na kuwaona wanafunzi wanaolipiwa fedha na wafadhili hao ambao wanadaiwa kutoa fedha nyingi kila mwaka ili kusomesha wanafunzi wa O level na A level.
Ilikuwa ni tarehe 5/5/2017 msaidizi wa mbunge huyo alianza kupiga simu kwenye baadhi ya shule akiwapa taarifa kwamba waandae taarifa za wanafunzi wanaosomeshwa na Wamarekani kwa kuwa wapo Singida na wanahitaji kuonana na wanafunzi wanaowafadhili, Ruben ananukuliwa akitoa maelekezo kwa walimu waandae hata taarifa za kupika ili kuwapooza wazungu wale maana mbunge ndio amemtuma awalete jimboni, mambo yalizidi Kuwa magumu baada ya walimu kusimama kidete na kudai hakuna mwanafunzi hata mmoja anayesomeshwa na ofisi ya mbunge hivyo wasingeingia kwenye mtego huo wa Udanganyifu, mfano ni mwalimu wa shule mojawapo alipiga simu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri akimdokezo kuhusu mchezo huo wa mbunge Lazaro Nyalandu, Mkurugenzi aliwaonya walimu wasihusike na Udanganyifu huo.
Ruben akiambatana na wazungu 4 alifika shule ya Sekondari Ilongero mnamo siku ya Ijumaa tarehe 5/5/2017 na alionekana akiingia ofisini kwa walimu na kuzunguka zunguka shule hiyo akiwazuga wale wazungu na baadae waliondoka kuelekea Kijota kwa lengo hilohilo kutembelea wanafunzi hewa wanaosomeshwa kwa ufadhili wa wazungu hao, ni katika shule ya sekondari kijota Mkuu wa shule alipigwaa butwaa kusikia kwamba kuna wanafunzi wa shule yake wanasomeshwa na Mbunge kwa ufadhili wa wamarekani. "Hapa shuleni kwangu hakuna wanafunzi wanaosomeshwa na mbunge na hakuna taarifa za namna hiyo hapa shuleni kwangu " alisema mkuu huyo wa shule.
Kwa taarifa za uhakika toka Idara ya Elimu ni kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja anayesomeshwa na Mbunge huyo wala na wafadhili hao, inawezekana wafadhili wanatoa fedha nyingi lakini haziwafikii walengwa.
Mbunge wa Singida kaskazini kwa muda mrefu amekuwa akilalamikiwa na wananchi kwa kuwadanganya kuwasomesha wanafunzi na amekuwa hafanyi hivyo, kuna kipindi aliorodhesha majina ya wanafunzi ambao wazazi hao hawana uwezo kwa ahadi ya kusomeshwa bure na hakuwahi kutekeleza badala yake wazazi walisubiri kwa matumaini bila mafanikio na baadhi ya wanafunzi walishindwa kuendelea na masomo.
Wale wazungu wa Nyalandu waliondoka Singida siku ya Jumamosi kuelekea Arusha na ndio walewale walionekana kwenye picha za ajali ya wanafunzi wa *Lucky Vicent* waliopata ajali na kupoteza maisha.