Mbunge Kiteto alia na mfuko wa jimbo

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
449
60
Huwa najiuliza kwa sauti, hivi mfuko wa Jimbo nani anakuwa nao, wanapotaka ufanye kazi, nani anasema nini ili wananchi waweze kujua kuwa wameungwa mkono miradi yao na mfuko wa jimbo?

Maswali haya yatabaki kama yalivyo ila sasa nisemee kijisehemu tu hapa, kumbe unapoutumika visivyo, hatua zinatakiwa kuchukuliwa.

Nimpongeze Mhe Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian, umekuwa Jemedari baada ya kuona kuna ubadhirifu kwenye fedha za mfuko wa Jimbo umeamua kupambana na kutounga mkono ubadhirifu na kuomba mamlaka ziingilie kati.

Iko hivii pale Shule ya Sekondari Engusero, mfuko wa Jimbo ulitumika kutengeneza madawati na meza zake jumla 100 kwa thamani ya mil 6.5 lakini madawati na viti yako chini ya kiwango.

Papiani anasema hawezi kuwa sehemu ya wachakachuaji hao,"Naomba nieleweke, Mimi sio sehemu yao siungi wala sipokei taarifa ya haya madawati na viti nimeona, baadhi ya viongozi nao wameona, kwakuwa hizi in fedha za wananchi tuungane kukataa vije tulivyokubaliana".

Mamlaka za Serikali naomba zitusaidie huenda hatuoni sisi huku tukidhani tupo sahihi, hapana Mimi nimeyaona madawati na meza yako chini ya kiwango.

Hongera Papian huko ndiko kipigania haki za wananchi.
 
Back
Top Bottom