Mbunge Chadema matatani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Chadema matatani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 11, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMAMOSI, AGOSTI 11, 2012 08:43 NA MAREGESI PAUL, DODOMA

  NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai , ameagiza Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa, akajadiliwe katika Kamati ya Bunge ya Maadili.

  Naibu Spika amefikia hatua hiyo jana jioni, baada ya Mchungaji Msigwa ambaye ni Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), kuliambia Bunge, kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Karatu, aliyemtaja kwa jina la Mzee Lazaro ni jangili na anamiliki bunduki aina ya Riffle 375, kwa ajili ya kuulia tembo.

  Kabla Naibu Spika hajatoa agizo hilo, awali Mnadhimu Mkuu wa Serikali Bungeni ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, aliomba Mwongozo wa Spika akitaka kukanusha kauli ya Mchungaji Msigwa aliyemtuhumu kiongozi huyo wa CCM alipokuwa akisoma hotuba ya kambi yake kuhusu bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013.

  Akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma hizo, Lukuvi alisema kilichosemwa na Mchungaji Msigwa hakikuwa sahihi kwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Karatu ni John Zacharia Tipa badala ya Mzee Lazaro aliyekuwa ametajwa na Mchungaji Msigwa. Kwa mujibu wa Lukuvi, Mzee Lazaro ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kupitia CHADEMA.

  Pamoja na hayo, Lukuvi alisema CCM haikumbatii majangili kama ilivyoelezwa na kambi ya upinzani kwa kuwa Februari 12 mwaka 2010 watu saba walikamatwa katika Kijiji cha Marang kilichopo jirani na Hifadhi ya Ngorongoro wakiwa na gari la Serikali lenye namba SM 4117.

  Katika tukio hilo, alikuwamo Diwani wa Kata ya Lotya pamoja na ofisa mmoja wa Idara ya Wanyama, wakiwa na bunduki moja aina ya Riffle 5287 ikiwa na risasi saba.

  Pia, alisema watuhumiwa hao walikamatwa na bunduki aina ya Shortgun yenye namba 400 ikiwa na risasi sita.

  Kutokana na maelezo hayo, Lukuvi aliomba mwongozo wa Spika akitaka Mchungaji Msigwa aombe radhi na afute shutuma dhidi ya kiongozi huyo wa CCM na chama hicho kwa ujumla.

  Hata hivyo, Naibu Spika hakumruhusu Mchungaji Msigwa kujibu chochote badala yake, aliamua kulipeleka suala hilo katika Kamati ya Maadili ili likajadiliwe na kupatiwa ufumbuzi.

  Awali, akisoma hotuba ya kambi yake, Mchungaji Msigwa alisema Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha ni Mzee Lazaro na kwamba ni jangili.

  Alisema Lazaro, amekuwa akitumia bunduki aina ya Riffle 375 na kwamba amekuwa akishirikiana na majangili wegine katika kazi hiyo.

  “Kuna taarifa za kuwepo majangili wa utafutaji wa masoko ya nyara za Serikali, wasambazaji wa silaha za kivita, wafadhili wa ujangili wenye wawakilishi wao na kufanya kazi ya kusambaza sumu ya kuulia wanyama, bunduki na risasi.

  “Kambi Rasmi ya Upinzaini, inahoji pamoja na taarifa hizi kuwapo serikalini na watuhumiwa kutambuliwa kwa majina na aina ya silaha walizonazo watuhumiwa hao, bado Serikali haitaki kuwachukulia hatua zozote za kisheria.

  “Usalama wa tembo uko hatarini kutokana na Serikali kutochukua hatua dhidi ya ujangili wa tembo kwani pamoja na taarifa za ujangili kuwapo serikalini ambapo viongozi wa CCM wanashiriki katika ujangili, Serikali imeendelea kuwalinda.

  “Mfano halisi wa viongozi hao wa CCM, mzee Lazaro ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Karatu ambaye anamiliki silaha aina ya Riffle 375 na huyu ni mshirika wa mtandao wa ujangili.

  “Katika mtandao huu, Lazaro anashirikiana na Bryson Baloshingwa ambaye naye Serikali imeendelea kumlinda.

  “Kwa maana hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kwa kupitia waziri husika, kuwaeleza Watanzania kama ni sera ya Serikali ya CCM kufumbia macho masuala yanayotishia ustawi wa taifa kwa kuwalinda majangili wakiwamo viongozi wa chama chao,” alisema Mchungaji Msigwa.

  Pamoja na Lazaro, Mchungaji Msigwa alimtaja kiongozi wa ujangili Bryson Baloshingwa ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Busunzu, Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Kigoma, kwamba licha ya kutambuliwa kuwa ni jangili, bado hajachukuliwa hatua zinazostahili.

  Kwa mujibu wa Mchungaji Msigwa, Baloshingwa amekuwa akiendesha ujangili wa kuua tembo katika Hifadhi za Taifa za Serengeti, Katavi, Tarangile, Ziwa Manyara, Ngorongoro na katika Mapori ya Akiba ya Ugalla, Rungwe, Moyowosi na Maswa.

  Pia Mchungaji Msigwa, aliwashutumu askari polisi, kwamba wanatumia magari ya Serikali na magari yao binafsi kusindikiza misafara iliyobeba nyara za Serikali.

  “Kuna taarifa baadhi ya watumishi wa Serikali, wanahusika na matukio ya ujangili katika hifadhi za taifa na taarifa hizi ziko katika mamlaka za Serikali ingawa haitaki kuzifanyia kazi.

  Wakati Mchungaji Msigwa akisoma hotuba hiyo jana asubuhi, Lukuvi alisimama kwa kutumia Kanuni ya 64 (1) na kuomba Mwongozo wa Spika akitaka Mchungaji Msigwa alithibitishie Bunge jinsi kiongozi wa CCM alivyo jangili.

  Hata hivyo, kabla Mchungaji Msigwa hajasema chochote, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), alisimama na kutumia Kanuni ya 63 (4).

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hii inashangaza CCM inatumia NGUVU zake ni ajabu; kama ametumia jina kimakosa halafu CCM haina Majangili?
   
 3. w

  why JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 203
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa ccm vipi?????// mbona inajulikana na ushahidi umewasilishwa leo kwa spika pamoja na marekebisho kufanyika mbona haya hayasemwiiiiiiiiiiii? Na kuishia kudanganya kuwa chadema waongo? Huu sii uungwana kama ndio tunakuza uongo na kuficha ukweli kila anaesema kweli anaambiwa muongo na mwongo anautangaza uongo wake hapa haki hakunaaaaaaaaaaa
   
Loading...