Mbunge: CCM WANATAKA KUNIUA

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
MBUNGE wa Ilemela, mkoani Mwanza, Bw. Highness Kiwia (CHADEMA), amefichua mpango wa kutaka kumuua unaofanywa na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), jimboni humo.

Kiwia alisema huo ni mpango wa muda mrefu ambao ulipangwa na kusisitiza kuwa, mabadiliko katika jiji la Mwanza hayawezi kuzimwa kwa kumuua yeye

"Hata nikifa leo, wananchi wa Mwanza wataendeleza harakati za kudai mabadiliko, mimi sio kuku wa Krismasi ambao huchinjwa hovyo," alisema Bw. Kiwia bungeni jana.

"Nipo tayari kutoa ushahidi wote na majina ya watu wanaotaka kuniua, nitayawasilisha bungeni kwa muda niliopewa," alisema.

SOURCE: GAZETI LA MAJIRA
 
duh,kweli magamba noma.
mh.mbunge wala hawawezi,wataishia kutaka tu.
mabadiliko haya ni mpango wa mungu ndiyo maana hata walivyokukata mapanga hawakukuua,dr ulimboka nae hawajamuua.wanapigwa upofu hawa wapuuzi.
 
Hao CCM mbona wanaua kila siku ,kule Zanzibar si mnaona wakiwapiga watu kama ngedele ,au kwenu wale sio watu ?
 
Hizo ndio dalili za mwisho za anguko kuu la CCM! wameshindwa kushawishi kisiasa sasa wamebadilika kuwa Mafia wanaua bila kificho na kwa kuacha alama dhahiri kuwa ndio wameua!!
 
Back
Top Bottom