Mbunge CCM ampinga RC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge CCM ampinga RC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Dec 19, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]

  na Jumbe Ismailly, Singida


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  MBUNGE wa Iramba Mashariki (CCM), Salome Mwambu, ameonesha kupingana na mtazamo wa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, wa kupiga marufuku kilimo cha mahindi kwa wakulima mkoani hapa.

  Mwambu alionesha msimamo wake huo hivi karibuni alipokuwa akichangia mada ya kutolimwa kwa zao hilo kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa.

  Katika mchango wake baada ya kuruhusiwa na mwenyekiti wa kikao hicho, mkuu wa mkoa, Mwambu alisisitiza kutokubaliana na tamko hilo kwamba ni maamuzi ya mkoa huo.

  “Sikubaliani na msimamo wa mkoa na kwanza huu si msimamo wa wananchi wote kwani kwa miaka mingi wananchi wamekuwa wakilima zao hili, hivyo nashauri serikali iachane na msimamo huo, labda pengine iseme kuwa wananchi washauriwe kulima angalau ekari mbili za mazao ya kinga ya njaa,” alisisitiza Mwambu.

  Kwa mujibu wa Mwambu, wakati tamko hilo likitoka hakuna hata kiongozi mmoja wa ngazi ya mkoa au wilaya aliyediriki kuwashirikisha wananchi kwenye maamuzi hayo, jambo ambalo alisema ni dhana iliyojengeka ya kutokuwapo ushirikishwaji.


  Kuhusu pembejeo za kilimo, mbunge huyo alisema kuwa wakati wananchi wakitembea umbali mrefu kwenda kutafuta mbegu mji mdogo wa Haydom, wilayani Mbulu, anashangaa kusikia kauli ya mkuu wa mkoa kwamba mbegu zilizoletwa mkoani hapa zimerudishwa wizarani.


  Pamoja na kwamba Mkoa wa Singida ni moja ya mikoa sita nchini inayopata mvua zake mara moja kwa mwaka, Mwamba alisema hiyo isiwe sababu ya kuwakataza wananchi wote kuendeleza kilimo cha zao la mahindi.


  Hata hivyo, alisikitishwa na kitendo cha mkuu wa mkoa kuutangazia umma wa kwamba amemweleza waziri mwenye dhamana ya maendeleo ya kilimo kuwa asiuletee mkoa huo mbegu ya mahindi na badala yake mbegu zinayohitajika ni mtama na uwele.


  Alifafanua kuwa pembejeo za kilimo hazina budi kuletwa kwa wingi badala ya kurudishwa wizarani, ila cha msingi ni kuhakikisha pembejeo hizo zinafikishwa kwa wakati unaotakiwa na si vinginevyo.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Wakuu wa mikoa huwa kama miungu watu flani,sitashangaa mbunge huyo akikabiliana na kash kash zisizo kichwa wala miguu labda vile wote wanatoka magambas
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ubaya ya wakuu wa Wilaya yawa Baraka za Rais hawaisomi hiyo Mikoa wanayoteuliwa kwenda kujua Mazuri na Mabaya ya Mikoa hiyo au Yanayotakiwa kuendeleza mikoa hiyo wanakwenda na ubabe tu wa kuwa na ukaribu na rais
   
 4. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,741
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mkuu wa mkoa anadhani bado tuko kwenye ukomunist ambapo anaweza kuwaamilia na kuwalazimisha wananchi walime au wasilime nini. Hivi hawa viongozi wa ccm watabadilika lini waelewe kwamba wananchi wanauwezo wa kufikiri na kujiamulia wao wenyewe?
   
 5. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 4,935
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Huyu mkuu wa mkoa wa Singida ana tatizo yani yupo kama roboti vile, huwa hataki kusikiliza hata ushauri wa wataalamu, siku zote amekuwa na msimamo mkali katika kukataza wananchi wasilime mahindi na tumbaku wakati ni mazao ambayo watu wanalima kwa muda mrefu na wanavuna vizuri tu. Kwa kweli si sehemu zote za mkoa wa singida zinafaa kulima mahindi, kwa mfano ukanda wote wa bonde la ufa kilimo cha mahindi hakina uhakika sana so upande wa bonde la ufa wanatakiwa kulima mtama ila sehemu nyingine zinakubali kulimwa mahindi.
   
 6. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  huku ndio kukua kwa demokrasia!
   
Loading...