MBUNGE CCM ahukumiwa kifungo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MBUNGE CCM ahukumiwa kifungo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngoshwe, Nov 13, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mbeya imemhukumu Mbunge wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya (CCM) Dickson Kilufi kutumikia kifungo cha miezi 10 au kulipa faini ya sh 500,000.  [​IMG]
  Mh. Mbunge wa Mbarali Modestus Dickson mwenye kaunda suti katikati.  Hukumu hiyo imetolewa jana na Hakimu Mkazi Michael Mteite baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mawakili wa serikali mahakamani hapo.

  Hakimu huyo alisema kuwa kutokana na maelezo yaliyotolewa na mlalamikaji wa kesi hiyo, Jordan Masweve, ambaye ni ofisa mtendaji wa kata ya Ruiwa, wilayani Mbarali, mkoani hapa kwa kuzingatia taarifa alizoziwasilisha kituo cha polisi juu ya kutishiwa kuuawa pamoja na shahidi wake unaonyesha mshtakiwa alitenda kosa hilo.

  alisema Hakimu Mteite.Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mawakili wa upande wa mashitaka walimwomba Hakimu Mteite kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa, ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

  Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, hakimu huyo alisema mbali na kesi hiyo, mahakama iligundua kuwa mlalamikaji na mshtakiwa wana uhasama wa muda mrefu ambapo mpaka sasa bado kuna kesi nyingine ambayo inaendelea mahakamani.

  Wakili wa serikali Apimark Mabrouk aliiambia mahakama hiyo kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ambao haukuacha mashaka yoyote dhidi ya mshtakiwa, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kwa kutenda kosa hilo.Naye wakili wa Mbunge huyo Edson Mbogoro kwa upande wake aliiomba mahakama kuangalia jinsi ya kumpunguzia adhabu mteja wake kwa kuwa ni mwakilishi wa wananchi katika jimbo lake la Mbarali na pia ni mbunge anayestahili kuwa bungeni kwa sasa.

  Baada ya hukumu hiyo mbunge huyo aliwaambia waandishi wa habari nje ya eneo la mahakama kuwa mahakama imefanya kazi yake kwa mujibu wa sheria, lakini bado anayo nafasi ya kuendelea na kesi katika mahakama nyingine ya juu ili kujua hatima ya kesi yake.Wakati mbunge huyo akitoa kauli hiyo, wakili wa mbunge huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa kosa hilo lililomtia hatiani mteja wake, halimwondolei nafasi yake ya ubunge kisheria kutokana na adhabu iliyotolewa dhidi yake.

  Wakili huyo aliongeza kuwa kwa sasa anaangalia uwezekano wa kukata rufaa mapema iwezekanavyo ili kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo.Kwa upande wake Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Verena Shimbusho ambaye alihudhuria mahakamani hapo aliwaambia waandishi wa habari kuwa ni wazi ifahamike kuwa kabla ya hukumu hiyo kulikuwa hakuna kikao chochote cha chama hicho kilichoketi kwa lengo la kumjadili mbunge huyo kama ana makosa yoyote ndani ya chama ili aweze kuondolewa.

  Alisema asingeweza kuzungumzia lolote juu ya sheria na taratibu za chama chake kuhusiana na hukumu iliyotolewa na mahakama na kuwa mahakama imefanya kazi yake kwa mujibu wa sheria na chama kitaangalia kwa upande wake juu ya hukumu hiyo. Mbunge huyu wa Mbarali alikamatwa na polisi mapema Oktoba 7 mwaka huu saa 9 alasiri akiwa maeneo ya ofisi zake wilayani humo na kusafirishwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kuelekea mkoani Mbeya.

  Baada ya kusomewa hukumu, Mbunge huyo alilipa Sh 500,000 na kuachiwa huru.


  http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=36234

  http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=23141
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi kutoshia kuua siyo kosa la jinai kweli?
   
Loading...