Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,428
Mbunge wa Jimbo la Busokelo, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete leo tarehe 29 Aprili, 2025 Amechangia Bungeni wakati Bunge likijadili Hotuba ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 ikiendelea kujadiliwa Bungeni Dodoma.
Mhe. Atupele Fredy Mwakibete ameiomba Wizara ya Nishati kuwalipa fidia zao wananchi wa Jimbo la Busokelo waliopisha miradi ya umeme na pia ameomba kuwekwa nguzo za umeme za zege kutokana na uwepo wa Mvua za mara kwa mara.
Aidha, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete ametangaza fursa ya uwekezaji wa umeme wa joto ardhi unaopatikana kwa wingi kwenye jimbo la Busokelo ili kuchochea maendeleo ya Busokelo kwa kasi.