Mbunge atoa rambirambi milioni 2/- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge atoa rambirambi milioni 2/-

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amemkabidhi Balozi mdogo wa Kenya, Robert Mathenge, Sh milioni 2 za Tanzania, kwa ajili ya kuwezesha kusafirisha mwili wa Paul Njuguna Kaiyehe (26), kwenda Nakuru, kwa maziko.

  Akitoa ubani huo jana, Mbunge alisema Chadema iliona ni vema kutoa rambirambi japo kidogo, kwa ajili ya kusafirisha mwili huo.

  “Mnajua ndugu zangu nawapa pole sana, huu msiba umetufika wote, baada ya ndugu yetu kupigwa risasi eneo la Jogoo House stendi, akiwa katika shughuli zake na si kama alikuwa kwenye maandamano ya Chadema,” alisema Lema.

  Naye Mathenge, akipokea rambi rambi hizo na kumkabidhi kaka wa marehemu, Timoth Gitau Kaiyehe.

  Akipokea fedha hizo, Timoth alimshukuru Lema, kwa kuwasaidia kuwezesha kupeleka mwili wa ndugu yao kwao, akazikwe.

  Aliiomba Serikali ya Tanzania, kuchunguza kwa kina tukio hilo na kuchukua hatua ili kujenga uhusiano uliopo, ambao unaimarishwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Naye Oscar Job anaripoti kwamba, Chama cha Sauti ya Umma (SAU), kimewataka wananchi kuacha kudanganyika na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini wanaowashawishi kufanya maandamano bila ya kuwa na kibali cha Polisi, huku kikidai kuwa hali hiyo inachangiwa na njama za viongozi hao wanaotaka kujijenga kwa ukaidi.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na SAU ikiwa imesainiwa na Mwenyekiti wake, Paul Kyara, kilichosababisha vurugu za Arusha ni matokeo ya wananchi `kudanganywa’.

  Taarifa ilisema Chadema ingeweza kuepusha maafa ya Januari 5 Arusha yaliyosababisha kumwagika kwa damu, kama viongozi wake wangekuwa wavumilivu na kusubiri siku ambayo Polisi ingeruhusu maandamano yao.

  Alisema anaamini amani haiwezi kulindwa kwa ukaidi na kiburi dhidi ya amri halali ya vyombo vya Dola, huku akisisitiza kuwa Chadema walikosa hekima, busara na uvumilivu, ili kuepusha maafa na wakashikilia falsafa yao ya kuonewa huruma.

  “Serikali kama ingekuwa inajifunza ingeacha kabisa Chadema waandamane na pengine kulindwa na kupokewa vizuri, sidhani kama ingepata lawama inazozipata sasa na pia kama watu kuuawa kama walivyouawa,” alisisitiza Kyara.

  Alisema tatizo analoliona kutokana na maafa hayo ni kwa Serikali kushindwa kujifunza na hata jamii pia CCM na Chadema, kukosa kuwa na busara na hekima kwa kile alichoeleza kuwa watu wanapolilia kufanya jambo wanalokatazwa, inahitaji kuwa na viongozi wenye hekima na uelewa wa falsafa na saikolojia ya mtoto anayelilia moto au wembe.

  Kyara aliwapa pole wafiwa na wana-Arusha kwa jumla, huku akiwasihi kutodanganyika hata kukubali kuandamana yasiyozingatia taratibu.

  HabariLeo | Mbunge atoa rambirambi milioni 2/-
   
 2. Marunde

  Marunde JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Jun 9, 2008
  Messages: 253
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 60
  SAU hivi kumbe bado kipi du! mi nilijua kilishazikwa.Naona wanajipendekeza ccm wapate chochote.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  safari njema
   
Loading...