Mbunge amwaga simu kwa wapiga kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge amwaga simu kwa wapiga kura

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibongoto, Sep 13, 2009.

 1. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  MBUNGE wa Jimbo la Biharamulo Magharibi mkoani Kagera Bw. Oscar Mukasa ametoa simu 74 za mezani zitakazotumiwa na wapiga kura wake katika kuwasiliana naye.

  Bw. Mukasa alikabidhi simu hizo wiki iliyopita katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Biharamulo ambapo kila kijiji jimboni humo kitapata simu moja.

  Alisema uamuzi wa kutoa simu hizo ameufikia baada ya kuona wapiga kura wake wakipata ugumu katika kuwasiliana naye hivyo akawataka kuzitumia kueleza matatizo na ushauri utakaohitajika kupatiwa ufumbuzi ndani ya jimbo hilo.

  “Ndugu zangu simu hizi zitusaidia katika mawasiliano ya mara kwa mara nanyi na zina uwezo wa kutumiwa na watu wapatao 15 mpaka 20 kwa wakati mmoja hivyo tunaweza kuendesha majadiliano kupitia simu hizi badala ya kulazimika kuonana ana kwa ana," alisema Bw. Mukasa.

  Mbali na simu hizo, Mbunge huyo alisema anatarajia kuweka mwakilishi wake katika kila kata ili kurahisisha mawasiliano au utatuzi wa kero mbalimbali zinazojitokeza.

  Aliwataka wananchi hao kutumia
  fursa mbalimbali zinazoibuliwa wilayani humo ikiwemo mikopo ya pembejeo za
  kilimo ili kutimiza kauli mbiu ya Kilimo kwanza. Source: http://majira.co.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=1381:mbunge-amwaga-simu-kwa-wapiga-kura&catid=36:mikoani&Itemid=59
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Wananchi wa biharamulo magharibi hawahitaji sana simu kwani ni wengi wana simu za mkononi, wao wanahitaji maji safi, umeme wa uhakika, huduma za afya, elimu n.k.

  Huyo mkasa badala afikirie kuanzisha mfuko wa kusomesha watoto yatima jimboni kwake, anawapelekea simu ambazo hawana hata pesa ya kuziendesha, Mkasa huna jipya.
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama watu wa Biharamulo wanahitaji simu basi ndio hizo lakini Watu wa huko sio muhimu kuwa na simu wakati hali za watu ni Duni sana
   
Loading...