Tumeambiwa tufyatue.Kinachoelezwa na wanasiasa ni tofauti na maelekezo yanayotolewa nyuma ya pazia kwa hospital zetu....
Rekebisha usemi wako.Ni aibu kwa mume kusubiri mke ajifungue kwa hisani ya watu wa marekani.
Bima ya CHF ni Tsh 30,000 kwa mwaka yaani mume,mke na wategemezi wanne.
kwa kuwa na bima hii utakuwa umeokoa mengi.
Wakati Serikali ikisisitiza matibabu bure kwa makundi ya wanawake wajawazito, watoto chini ya miaka mitano na wazee kulingana na Sera ya Afya inavyosema, Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Emmanuel Mwakasaka amesema Hospitali ya Kitete mkoani Tabora wamekuwa wakiwatoza wajawazito Sh 30,000 hadi 50,000 wakati wa kujifungua.
Akiuliza swali bungeni leo Ijumaa Februari 5, 2020, Mwakasaka alihoji “Hospitali ya Kitete Tabora bado inatoza fedha kwa akina mama waliojifungua kwa njia ya kawaida na wanaoshindwa kutoa hizo fedha huwa wanazuiliwa. Je, serikali ina msimamo gani kwa akina mama wanaozuiliwa kutoka na watoto wao wachanga hadi walipe?"-
Fedha wanazotozwa wajawazito ni gharama ya vifaa vyote walivyotumia wakati wa kujifungua ndio hiyo 30,000 hadi 50,000Huyu naye alitakiwa kuuliza hao wanaotoza hizo fedha wanatoa risiti ya EFD? na kama hawatoi amekwenda PCCB kutoa taarifa? Bungeni angekwenda kutoa taarifa ya idadi ya waliokamatwa kutokana na kukiuka taratiu za serikali na hatua zingine, kwa kufanya hivyo angewaokoa wengi
Fedha wanazotozwa wajawazito ni gharama ya vifaa vyote walivyotumia wakati wa kujifungua ndio hiyo 30,000 hadi 50,000
Akina mama wanaoenda kujifingua na vifaavyao hawatozwi hizo hela(wanao jifungua kawaida).
Serikali yetu ni utopolo kupaza sauti kujifungua ni bure huku vifaa vinanunuliwa.
Mpe mtu mimba akajifungue ndo utaelewa nilichokuambai.Mbona huwa anasema "ninaposema bure nina maana bure kwelikweli"