Mbunge adaiwa kuwatapeli kina mama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge adaiwa kuwatapeli kina mama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Sep 6, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [h=3]
  [/h][​IMG]


  Na Danson Kaijage, Dodoma


  MBUNGE wa Babati Mjini, Kisyeri Chambiri (CCM), analalamikiwa na kina mama ambao wanajishughulisha na kazi ya ufundi rangi kwa kitendo cha kutowalipa sh 750,000 baada ya kupaka rangi katika Msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma.

  Chambiri anadaiwa kuwa kati ya wasimamizi wa kampuni ya Wine Source ambaye alihusika kusimamia mradi wa ujenzi wa Msikiti wa Gaddafi na kushindwa kuwalipa wanawake hao ambao mpaka sasa wanadai kuwa wanasumbuliwa na vibarua wao waliowasaidia.


  Mmoja wa mafundi hao,Mwajuma Issa, aliliambia gazeti hili mjini hapa jana kuwa akiwa na mwenzake, Hawa Jumanne, walipewa kazi na mbunge huyo na baada ya kuimaliza hawakulipwa ujira wao kama makubaliano yalivyokuwa.


  Mwajuma alisema katika kazi ya kupiga rangi msikiti huo ambao ulifadhiliwa na aliyekuwa Rais wa Libya, Muammar Gaddafi na kusimamiwa na baadhi ya makandarasi akiwamo Chambiri, waliahidiwa kulipwa kiasi hicho cha fedha baada ya kumalizika kwa kazi hiyo.


  Aliongeza kuwa makubaliano yote yalikuwa sh milioni moja lakini walilipwa sh 250,000 kama malipo ya awali.


  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Shaaba Rajabu, alipoulizwa juu ya jambo hilo, alikiri kuwatambua wanawake hao mafundi rangi akisema kuwa wamekuwa wakidai kiasi hicho kwa muda mrefu.


  “Ni kweli najua mafundi hao walikuwa wakidai fedha zao kutokana na kazi yao ya kupaka rangi jengo, lakini mimi niliwashauri waende Idara ya Kazi ili mhusika aweze kuandikiwa barua ya kuitwa mahakamani ili waweze kulipwa haki zao badala ya kukimbilia katika vyombo vya habari,” alisema.


  Alisema mafundi hao walikuwa wakifanya kazi chini ya Kampuni ya Wine Source na baada ya mmojawapo wa wenye kampuni hiyo kufariki dunia, Chambiri ndiye alibakia akisimamia shughuli hizo na kimsingi anatakiwa kuwalipa mafundi hao.


  Chambiri alipopigiwa simu yake ya kiganjani ili kutolea ufafanuzi madai hayo, hakuipokea na hata alipoandikiwa ujumbe mfupi (sms) hakujibu.


  Chanzo: Tanzania Daima
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Mh. Chambiri yaani Umeshindwa kuiba ndani ya BUNGE kama Wenzako? Mpaka kuwaingilia kina Mama wasio na sauti?
   
 3. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ndio ccm walivyo wamejaa ujambazi kila sehemu
   
 4. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kisyeri, dawa ya deni ni kulipa si maelezo marefu yasiyo na tija.
   
Loading...