MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Mmarekani Margaret J. Wheatley alisema ‘’Without reflection, we go blindly on our way, creating more unintended consequences, and failing to achieve anything useful’’.
Baada ya Uchaguzi Mkuu huwa ni muda wa kuyatazama mafanikio na mapungufu yaliyojitokeza katika kulifikia lengo la uwepo wa chama katika uwanja wa siasa. Kama ilivyo ada, mwisho wa Uchaguzi ni mwanzo wa uchaguzi mwingine.
Ikumbukwe kuwa, baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Freeman Mbowe walianza harakati nyingine za kisiasa katika lengo la kuondoa mapungufu ya Uchaguzi uliopita ili CHADEMA ipewe ridhaa ya kuingia Ikulu katika Uchaguzi Mkuu 2015. Harakati hizo ziliambatana na ahadi nyingi kwa Watanzania.
Moja ya ahadi aliyoitoa Mbowe wakati akuhutubia wananchi wa Masasi mwaka 2012 ni kutueleza kuwa atajiuzulu uenyekiti wa chama na siasa kama CHADEMA haitapewa ridhaa ya kuingia Ikulu.
Maelezo ya Mbowe kuhusu ahadi hiyo yanapatikana katika Thread/Mada hii;
Hakuna mtu au taasisi iliyomuwekea Mbowe bunduki kichwani ili kumshinikiza kutoa ahadi hiyo. Alitoa ahadi kwa utashi wake huku akiwa hana mgandamizo kifikra(undue influence) au matatizo ya akili(insane).
Mwanafilosofia wa Marekani aitwaye William James alisema pia’’Acceptance of what has happened is the first step to overcoming the consequences of any misfortune’’.
Kama viongozi CHADEMA wanataka/wanapenda wawe wanaaminiwa kwa kile wanachokisema ni lazima waanze kuyaishi maneno yao (walk the talk). Kuendelea kuona kauli ya Mbowe ni suala la kawaida ni kujenga mazingira ya kuendelea kutokuaminiwa kwa kile wanachokiahidi au kukisema kwa Watanzania.
Ahadi ni deni! Ikumbukwe, it’s very difficult to regain trust and reputation once you toss away!

Katika Mkutano huo, Mbowe alikaririwa akisema,
Tunatambua Uchaguzi Mkuu 2015 umepita na CHADEMA haikupata ridhaa ya kuingia Ikulu. Kwa mantiki na maana hii, huu ni wakati wa Mbowe kutimiza ahadi yake na kujiuzulu.Ndugu zangu ngojeni niwaulize swali, wakati wa utawala wa Mwinyi na Mkapa (marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa), ni kipindi gani maisha yalikuwa mazuri? Wananchi wakajibu (kipindi cha Mwinyi). Miaka 10 ya uongozi wa Mkapa na miaka saba ya Kikwete, ni kipindi gani maisha yamekuwa magumu zaidi?" Wakajibu (Kikwete); Je, 2015 wanakuja tena kutuomba kura huyo atakayekuja si ndiyo itakuwa mbaya zaidi, Chadema hatuwezi kukubali na moto huu tuliowasha utaendelea nchi nzima hadi Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kama CCM itasalimika nitajiuzulu siasa.