Mbowe: Rais Magufuli ndiye rais wa pekee Tanzania atakaekaa madarakani kwa kipindi kimoja

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Mhe Rais Magufuli ndiye rais wa pekee Tanzania atakaekaa madarakani kwa kipindi kimoja cha utawala wake kutokana na kuendesha nchi kibabe bila kufuata sheria, uonevu, upendeleo na hali ngumu ya maisha inayawakabili wananchi tofauti na kipindi kilichopita.

Mbowe ametoa kauli hiyo wakati akizindua tawi jipya la Chadema katika kijiji cha Mpakani Kata ya Kwakifua Wilaya ya Muheza mkoani Tanga leo Jumamosi.

Freeman Mbowe
M/kiti Chadema-Taifa.
Muheza leo
25.03.2017
tmp_30533-FB_IMG_1490450997916-1257937617.jpg


FREEMAN Aikaeli Mbowe, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni miongoni mwa waasisi wa chama hicho amesema atajiuzulu kufanya siasa iwapo Rais John Magufuli atashinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, anaandika Charles William.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ametoa kauli hiyo mbele ya wanachama wa Chadema wilayani Muheza Tanga ambapo yupo katika ziara ya kukagua uhai wa chama.

“Huyu atakuwa rais wa kwanza kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano tu. Na kama Magufuli akishinda tena uchaguzi mwaka 2020 mimi nitajiuzulu siasa,” amesema Mbowe.

Kiongozi huyo aliorodhesha madudu kadhaa ya utawala wa awamu ya tano ikiwemo upendeleo wa kugawa madaraka na kulinda waovu wasio na sifa ya kuwa viongozi akitolea mfano wa Paul Makonda mwenye tuhuma mbaya ya kufoji vyeti vya elimu na mtu aliyeongoza uhalifu wa kuvamia kituo cha Habari cha Clouds.

Pia Mbowe aliutuhumu utawala wa sasa wa kunyanyasa wananchi na kuonyesha ubabe huku ukiminya uhuru wa vyombo vya habari na ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya nchi.

Amesisitiza kuwa chama chake tayari kimeanza kujiandaa na uchaguzi wa 2020 kwani kumalizika kwa uchaguzi mmoja ni maandalizi ya uchaguzi mwingine.

Mbowe yupo ziarani mkoani Tanga, akifungua matawi ya chama hicho na kukagua uhai wa chama.

Ameambatana pia na Julius Mwita, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha).
Mbowe ndiye mwanasiasa pekee ambaye bado anafanya siasa miongoni mwa waasisi wa mwanzo kabisa wa Chadema.
Wengi wamekufa na wengine ni wazee kiasi cha kutoweza kumudu mikimiki ya siasa za majukwaani.

Hii ni ahadi ya pili ya Mbowe kujiuzulu siasa.
Mara ya kwanza, mwaka 2014 aliahidi kujiuzulu siasa mwaka 2015 iwapo chama chake kingepata idadi ndogo ya kura za Urais na wabunge kuliko kilichopata mwaka 2010.

Hata hivyo Chadema kiliongeza Wabunge kutoka 49 mpaka 71 huku kura za urais zikipanda kutoka asilimia 26 kwa mwaka 2010 mpaka asilimia 40 kwa mwaka 2015.
 
Nikifikiria Ile tofauti ya kura mil 2 miaka 2 imepita nawaza tu zile 2m hazihamia upande wa pili? Kikichopo mpaka sasa upinzani wapiga kura wake hawajapungua ila kwa watawala naamini nusu ya wapiga kura wao wamehamia upande wa pili
 
Mhe Rais Magufuli ndiye rais wa pekee Tanzania atakaekaa madarakani kwa kipindi kimoja cha utawala wake kutokana na kuendesha nchi kibabe bila kufuata sheria, uonevu, upendeleo na hali ngumu ya maisha inayawakabili wananchi tofauti na kipindi kilichopita.

Freeman Mbowe
M/kiti Chadema-Taifa.
Muheza leo
25.03.2017


ILE NAFASI ALIYOIACHA WAZI MZEE WA MAONO PALE HOTELINI KISONGO IPO WAZI ,NAONA DJ UNAJAZA FOMU ILI UKAKAE, HAYA KAZI KWAKO.
 
Mhe Rais Magufuli ndiye rais wa pekee Tanzania atakaekaa madarakani kwa kipindi kimoja cha utawala wake kutokana na kuendesha nchi kibabe bila kufuata sheria, uonevu, upendeleo na hali ngumu ya maisha inayawakabili wananchi tofauti na kipindi kilichopita.Mbowe ametoa kauli hiyo wakati akizindua tawi jipya la Chadema katika kijiji cha Mpakani Kata ya Kwakifua Wilaya ya Muheza mkoani Tanga leo Jumamosi
Freeman Mbowe
M/kiti Chadema-Taifa.
Muheza leo
25.03.2017
View attachment 486862
View attachment 486863
NONSENSE: KUOTA NI HAKI YENU. Subirini hadi 2025
 
Back
Top Bottom