Akifungua kikao cha Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amesema wananchi watajadili Katiba kadiri wanavyotaka na siyo kama anavyotaka Rais Jakaya Kikwete na kwamba hata suala la Muungano litajadiliwa kwa vile ni haki yao.
Source: Tanzania Daima.
nini cha kujadili kwenye muungano??
Ivi ssi watanganyika tunapata nni ndani ya huu muungano?
...Kila kitu kilichokuwemo ndani ya katiba ya sasa na vile ambavyo havimo lakini vinahusu nchi zote mbili lazima vijadiliwe. Kama Watanganyika tutaamua kuwepo kwa Serikali tatu ya Tanganyika, Zenj na Muungano basi iwe hivyo ila kwa maoni yangu kutakuwa na gharama kubwa sana za uendeshaji. Serikali moja tu inatosha ila Wazenj hatakubali Serikali yao imezwe ndani ya Serikali moja ya Tanzania.
nini cha kujadili kwenye muungano??
Ivi ssi watanganyika tunapata nni ndani ya huu muungano?
...Kila kitu kilichokuwemo ndani ya katiba ya sasa na vile ambavyo havimo lakini vinahusu nchi zote mbili lazima vijadiliwe. Kama Watanganyika tutaamua kuwepo kwa Serikali tatu ya Tanganyika, Zenj na Muungano basi iwe hivyo ila kwa maoni yangu kutakuwa na gharama kubwa sana za uendeshaji. Serikali moja tu inatosha ila Wazenj hatakubali Serikali yao imezwe ndani ya Serikali moja ya Tanzania.
Mbowe na misukule yake msipoteze umma hakuna mahali Kikwete ameseme Muungano usijadiliwe, kinachosemwa ni si kujadili kuuvunja muungano ni kujadili kuuboresha. Kuweni wa kweli kwenye nafsi zenu. Kama hauutaki muungano unajadili nini? si unasema tu "hatuutaki". Kwisha.?????
Kama unataka muungano basi kuujadili ni vipi utauboresha ruksa, hakuna aliyekatazwa.
Kwanini hakusema hilo bungeni?
nini cha kujadili kwenye muungano??
Wewe huoni tatizo?
Mheshimiwa nampa mkono wa hongera 100%. Mambo hayo lazima yajadiliwe na wanachi maana matatizo makubwa yamo kwenye suala tete la muungano. Mh. Mbowe kura yangu nimekupa tayari.
Kitendo cha kusema hauutaki muungano tayari utakuwa umejadili huwezi kusemea chumbani 'siutaki muungano' lazima uje kwa wananchi uwa-convince. Hata hivyo unaposema Kikwete kasema tuujadili lakini tusiuvunje kwani yeye ni nani si kabakiza miaka miwili tu aondoke madarakani, je baada ya hapo amri yake itaendelea ku-hold? Nafikiri Kikwete asiingilie sana suala hili historia isije ikamhukumu yeye awaachie wananchi waamue.Mbowe na misukule yake msipoteze umma hakuna mahali Kikwete ameseme Muungano usijadiliwe, kinachosemwa ni si kujadili kuuvunja muungano ni kujadili kuuboresha. Kuweni wa kweli kwenye nafsi zenu. Kama hauutaki muungano unajadili nini? si unasema tu "hatuutaki". Kwisha.
Kama unataka muungano basi kuujadili ni vipi utauboresha ruksa, hakuna aliyekatazwa.
Nyie mnaosema tusijadili kuvunja au kutovunja lazima mtuambie kwanini tusivunje, tuambieni faida zake tuzione. Tumeishi na muungano kwa miongo mitano sasa, partner mwenzetu Zanzibar anaona kama tunamkera, sasa nyie including Kikwete ambao hamtaki uvunjike mnatakiwa muende kwa wazanzibari na watanganyika muwaeleze faida zake na sio kuwalazimisha kuwemo kwenye chumba wasichotaka. Tofauti ya hapo hata kama katiba mpya itaandikwa manung'uniko yatakuwepo na labda yatazidi kuwa mabaya zaidi. Leo wazanzibari wanadai nchi yao kwa amani kabisa itafikia wakati wataidai kwa nguvu.Ndiyo hata mimi sioni tatizo kwavile maelezo yako ni ya jumla jumla!! Hakuna aliyesema muungano hautajadiliwa....jambo la msingi nini cha kujadili kama alivyokuuliza mtotowamjini!! Kitu ambacho hakitajadiliwa ni kuvunjwa au kutovunjwa kwa muungano.....ima faima, lazima muungano uwepo, issue ni muungano wa namna gani! Suala la kujadili ni muungano wa aina gani, litajadiliwa lakini kuwepo au kutowepo, NO!!!!! Hivyo basi, Mbowe au mtoa mada mlitakiwa kuwa wazi.....ni cha kujadili!! Tujadili suala la kuendelea na muungano au kuvunjwa kwako!!
gharama zipi jamani mnasema gharama tuuu!...Kila kitu kilichokuwemo ndani ya katiba ya sasa na vile ambavyo havimo lakini vinahusu nchi zote mbili lazima vijadiliwe. Kama Watanganyika tutaamua kuwepo kwa Serikali tatu ya Tanganyika, Zenj na Muungano basi iwe hivyo ila kwa maoni yangu kutakuwa na gharama kubwa sana za uendeshaji. Serikali moja tu inatosha ila Wazenj hatakubali Serikali yao imezwe ndani ya Serikali moja ya Tanzania.
Kitendo cha kusema hauutaki muungano tayari utakuwa umejadili huwezi kusemea chumbani 'siutaki muungano' lazima uje kwa wananchi uwa-convince. Hata hivyo unaposema Kikwete kasema tuujadili lakini tusiuvunje kwani yeye ni nani si kabakiza miaka miwili tu aondoke madarakani, je baada ya hapo amri yake itaendelea ku-hold? Nafikiri Kikwete asiingilie sana suala hili historia isije ikamhukumu yeye awaachie wananchi waamue.