Mbowe: Kikwete amehalalisha rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe: Kikwete amehalalisha rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PELE, May 17, 2010.

 1. P

  PELE JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 229
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mbowe adai Kikwete amehalalisha rushwa


  [​IMG]Monday, 17 May 2010 06:18  • Ni kwa kutetea takrima katika uchaguzi
  • Pia kwa CCM kupanga kutumia bilioni 50/-

  Na Tumaini Makene


  KAULI ya Rais Jakaya Kikwete kuwa takrima haiepukiki katika uchaguzi imezidi kuzua mjadala na sasa imeelezwa kuwa analivuruga taifa kwa kutoa kauli zinazohalalisha rushwa hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.

  Imeelezwa kuwa kauli hiyo ya Rais Kikwete, uamuzi wa CCM kupanga kutumia takribani sh. bilioni 50 katika uchaguzi na kutunga sheria ya matumizi ya fedha bila umakini, ni ushahidi kuwa serikali ya CCM haina dhamira ya dhati ya kupunguza gharama za uchaguzi, kupambana na rushwa wala kuleta maendeleo kwa Watanzania.

  Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe alipozungumza na Majira juu ya kauli ya Rais Kikwete kuunga mkono matumizi ya takrima katika mchakato wa uchaguzi, ilihali Mahakama Kuu ya Tanzania ilikwishatoa hukumu kuwa kitendo hicho ni rushwa.

  Mwishoni mwa juma lililopita, akizungumza na viongozi wa dini mbalimbali nchini katika semina iliyoitishwa na serikali kwa ajili ya kuwapatia elimu ya uchaguzi, Rais Kikwete alisema kuwa ni vigumu kuepuka suala la takrima katika uchaguzi, kauli ambayo inaonekana kupingana na uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa mwaka 2006.

  Bw. Mbowe alisema kuwa suala la takrima katika uchaguzi ni utamaduni ulioletwa na CCM baada ya kuruhusiwa kwa mfumo wa vyama vingi, ikitumia kama kigezo cha kuwahonga na kuwarubuni wapiga kura.

  "Hivi mbona sasa hatumwelewi Rais Kikwete, leo anasaini kwa mbwembwe sheria ya uongo ya kupunguza matumizi katika uchaguzi, mara chama chake kinatangaza kutumia bilioni 50 kwenye uchaguzi, kesho anatoa kauli ya kuunga mkono takrima, haeleweki sasa, analivuruga taifa, hana dhamira ya dhati katika mapambano haya.

  "Rais anaonesha udhaifu katika vita dhidi ya rushwa kama hizo za takrima na uchaguzi umekaribia... mpaka sasa bado miezi kadhaa kufanyika uchaguzi hatujui tunaingia kwa kutumia sheria ipi, Sheria ya NEC? Sheria ya Msajili wa Vyama vya Siasa? Au sheria hii mpya, ambayo mpaka sasa kanuni zake hatuzijui, maana mwanzo walileta kanuni ambazo hazitekelezeki," alisema Bw. Mbowe.

  Huku akitetea wapinzani wa kweli kuwa hawana uwezo, nia wala sababu ya kutumia takrima, Bw. Mbowe pia alipinga mfano alioutumia Rais Kikwete kutetea rushwa ya takrima katika uchaguzi.

  Wakati akizungumza na viongozi hao wa dini, Rais Kikwete alitumia mfano wa watu wa Kilimanjaro ambapo alisema kuwa ni vigumu kuwaita wazee na kuzungumza nao bila kuwapatia Kitochi (kipimo cha Mbege chenye ujazo wa lita moja) wanywe.

  "Si kweli. Nasema si kweli, tena hayo ni matusi kwa Wachagga, hakuna mila yoyote duniani inayosema kuwa eti ili uwaite wazee wa Kichagga na uzungumze nao na wakusikilize lazima uwapatie hicho Kitochi anachosema Bwana Mkubwa, mimi ni mtoto wa nyumbani, nimekuwa Mbunge wa Hai, tunafanya siasa kila siku, tunaitisha mikutano na vikao, hakuna kitu kama hicho.

  "Kwanza hakuna wapinzani wa kweli wanaweza kutoa takrima, hawana nia hiyo, wala sababu ya kutoa rushwa, huu ni utamaduni wa CCM, haya mambo ya takrima, kofia, pombe, hela, yaliletwa na CCM baada ya vyama vingi ili kuwahonga wapiga kura, ni vyema Rais akatumia mifano 'relevant' (halisia) anapozungumza," alisema Bw. Mbowe na kuongeza;

  "Tulimuunga mkono Rais aliposema kuwa wanatunga sheria ya kudhibiti matumizi katika uchaguzi, lakini sheria yenyewe mara ikakosewa, mara wakaleta kanuni ambazo hazitekelezeki tukazipinga, mpaka sasa hazijatolewa zingine na uchaguzi unakaribia...ghafla tunamsikia anawashawishi viongozi wa dini na Watanzania kuwa takrima haizuiliki, huko ni kuhalalisha rushwa katika chaguzi.

  Aliongeza kuwa tafsiri ya kauli ya Rais Kikwete ni kuwa Watanzania sasa wanaweza kushuhudia sheria ikitungwa lakini wakaweza kuivunja kwa kufuata maelezo ya viongozi wao.
   
 2. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #2
  May 17, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Yeah,Its true.kwanza kikwete naona sasa hana hafuati hata Itifaki za kuongea kama mkuu wa nchi.Huyu jamaa ni bora angepumzika tu,tunamwonea bure.Tanzania sasa tuongozwe na mtu mwenye IQ ya wastani kwenda juu,hizi IQ below average zitatuongoza hovyo hovyo,na kutupeleka kusikotakiwa.Mr.President hana courtesy na hayuko sensitive ktk kuongea.Oflate amekua mkurupukaji tu,na rangi zake halisi zinaonekana
   
 3. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  You are right man, jamaa itifaki imemshinda kabisa, RAISI huwa ana ulimi usio leta ukinzani na sheria zilizopo, kama yeye ametunga sheria ya kudhibiti rushwa halafu at the same time anasema ni vigumu kudhibiti rushwa, sasa tumuelewe vipi jamani, huyu jamaa kama ni type za mirror basi yeye is convex type--------taswira yake haieleweki, make you find it distorted and just a minute on normal looking-------he has got two faces
   
 4. Mpelijr

  Mpelijr Member

  #4
  May 18, 2010
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Ni kweli kabisa.....
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Face yake ya kweli ni bado amesoma mpaka digrii ya kwanza lakini bado hajaelimika, hivyo anaendesha mambo kama sio msomi, yawezekana haya yanatokea hata kwenye kuongoza familia yake, wewe ona mkewe navyojitwalia madaraka kinyume na katiba nae asemi kitu. Kwa kifupi sura ya huyu bwana ni bora liende na kujaribisha mambo - fanya hivi, wakikaa kimya tekeleza, wakipinga sema sawa au danganya. Sasa watanzania wote tumekuwa shemeji zake? Ukoo wake mwiko kuoa au kuolewa na ukoo wangu!
   
Loading...