Mbowe, Dr. Slaa SOMENI Hapa ni Muhimu Sana!

Mbowe, Dr. Slaa SOMENI Hapa ni Muhimu Sana!

masalapa

Senior Member
Joined
Oct 29, 2012
Posts
139
Reaction score
68
Shikamooni?

Mimi ni mwanachama wa Chadema niko mkoa wa Simiyu wilayani Bariadi. Kama mnavyokumbuka, mwaka 2010 tuliweka mgombea ubunge aitwaye Zacharia Thomas kwenye jimbo la Bariadi Magharibi. Hata hivyo hakufanya vizuri kwani hakuwa amejiandaa vya kutosha na ilikuwa ghafla mno. Matokeo yake alishindwa vibaya na Chenge huku Isaac Cheyo wa UDP akifuatia kwa karibu.

Dhumuni langu ni kuwaambia kuwa inabidi sasa tuanze kampeni za kukiimarisha chama hasa hasa katika mkoa huu mpya. Kumbukeni pia hata chama cha Republican baada ya kushindwa uchaguzi wiki iliyopita tayari kimeshaanza mikakati ya kujipanga kuelekea uchaguzi wa 2016. Sasa sisi ambao ni wachanga katika mkoa huu ilibidi tuwe tumeshaanza mikakati hiyo 01 Novemba, 2010 mara tu baada ya uchaguzi. Tathmini yangu baada ya kuzunguka maeneo mengi ya jimbo la Bariadi Magharibi na maeneo mengine ya mkoa huu mpya ni kuwa:
  1. sasa kuna vijana wengi walio na upeo wa ku-analyse mambo (hasa wale wahitimu wa sekondari za kata) na wanavutiwa sana na siasa za Chadema.
  2. Magamba wamewaudhi sana wananchi hasa wakulima kwa kutosimamia wapate bei nzuri ya pamba waliyoahidi (Tshs. 1,200/= kwa kilo) na badala yake bei ikawa Tshs. 600/= tu kwa kilo. Nawaambieni hii ni nafasi nzuri ya kuhubiri utapeli wa Magamba baada ya kuwa-disappoint wakulima wengi ambao wanategemea pamba. Ikumbukwe kuwa, umaarufu wa Mzee Cheyo kule Bariadi Mashariki ni kwakuwa yeye kila akisimama bungeni huongelea maswala ya pamba tu. Hii inamfanya kubaki hana mpinzani jimbonu kwake. Hata Magamba walipomtuma Makondo wa TRA kwenda kugombea jimboni kwake aliambulia aibu kubwa hata baada ya kutumia zaidi ya bilioni 1!
  3. Udhaifu wa Mzee wa Vijisenti ambaye ndiye mbunge wa sasa. Huyu jamaa alimwaga pesa nyingi sana, hata kufikia kutoa milioni 30 kwa kijiji cha Ikinabushu lakini akaambulia kura tatu tu, wastani wa Milioni 10 kwa kura 1! Mzee wa Vijisenti baadaye alikataa kufanyiwa sherehe na wanamagamba wenzake baada ya kushinda uchaguzi kwa madai kuwa ni hela zake tu ndio zimempitisha na wala sio wanaccm. Alifikia hata kusema Bariadi kuna michwa, wamekula hela zake nyingi lakini akaambulia mavuno kiduchu! Hii ilichangiwa sana na kutokukubalika kwa Magamba na udhaifu wa Mzee wa Vijisenti katika kuelezea na kusimamia sera za chama chao.
  4. Wananchi wengi wako tayari kwa mabadiliko ya kimfumo. Magamba hawana jipya tena katika kutetea wanachi. Hata nyie ni mashahidi Mzee wa Vijisenti ni vigumu sana kumsikia akitetea wananchi wake mjengoni. Yupo kama hayupo vile!
  5. Wana Chadema wengi hawajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura. Hili liko wazi, na naamini na nyie mnalifahamu. Changamoto hapa ni kueneze elimu ya uraia ili wananchi wengi, hasa vijana, wajiandikishe na pia wajitokeze kupiga kura. Mbinu hii ndiyo hasa iliyotumiwa na Obama kumbwaga Romney. Ikumbukwe kuwa, vijana wengi ni kama minorities katika nchi yetu, Magamba wamekumbatia wazee na akina mama waliochoka kimaisha na ambao muda wao wa kuwa active kwenye siasa umekwisha! Oneni hata sekretarieti yao ilivyo, unadhani Mukama, Msekwa, Chiligati, n.k. wanaweza kuongea lugha za vijana wakaeleweka? Sasa sisi tunao vijana, na vijana wako na sisi. Hii ni Asset katika siasa, tafadhalini sana tusiipoteze kizembe.
  6. Hakuna matawi na mashina mengi vijijini. Inabidi kampeni ya elimu ya uraia isiishie mikoa fulani fulani tu, ajirini makamanda wengi muwasambaze nchi nzima na hasa vijijini ambako kuna zaidi ya 70% ya wapiga kura. Mimi ni mmoja wao, niko kazini tangu mwanzo wa mwaka huu. Sisi ni kama Yohana Mbatizaji, tunaandaa njia ili Mgombea wetu akija 2015 apite kirahisi. Sasa tupeni support, iwe kwa ushauri ama mikakati. Acheni urasimu au kupuuzia kusambaza kadi na bendera za chama chetu. Hiyo ndio publicity ya chama. Bado si zaidi ya mwaka na nusu tuingie kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, tukifanya vizuri kwenye uchaguzi huo itakuwa ni ishara ya kushinda 2015. Lakini hatutaweza kama tutakaa tu na kuibuka 2014. Maandalizi, kama nilivyosema, yalipaswa kuanza 2010. Kumbukeni sisi bado hatuna rasilimali fedha za kutosha, hivyo inabidi kuanza maandalizi ya kukieneza chama hasa mikoa yote mipya (Geita, Katavi, Njombe na Simiyu) mapema iwezekanavyo ili kuwa na database kubwa ya wapiga kura.
Huo ni ushauri wangu, kama ikiwapendeza uchukueni na tushirikiane kuufanyia kazi. Mimi ni mwanachama wa kawaida tu. Baada ya masomo yangu UDSM, nimeamua kushiriki katika Vuguvugu la Mabadiliko huku kwenye grassroot, and charity begins at home. Kwa mawasiliano zaidi napatikana kwenye pemakono@gmail.com au 0719077297. Nawasilisha!
 
Ni makala nzuri sana yenye mwongozo mzuri. Ila sisi wananchi tumekuwa tukitegemea sana viongozi wetu watusaidia hata kazi za maandalizi ya shamba. Cha msingi wanachama wajipange na kutumia nguvu yao kukiimarisha chama, then viongozi wa juu wanakuja kukisimamisha sawasawa kwenye misingi tuliyoiweka vizuri.

Mfano kazi ya kufungua matawi isisubiri viongozi wakuu wa kitaifa tu, watazunguka kwa kazi hiyo tu mpaka 2020 na hawatafanikisha hiyo kazi. Cha msingi tuwatumie vizuri viongozi wetu wa wilaya na mkoa, hawa wa kitaifa wanakuja kwa maswala ya kukiimarisha chama katika wilaya kwa ujumla na kutoa ushauri kutokana na ripoti mnazozituma kwenye chama.

Kama kweli tunataka kukijenga chama, ni muhimu tujitoe wote kwa moyo wa kizalendo na si kutegemea/kuwatwisha mzigo mzito wale wachache waliojitoa kisawasawa.
 
Kwanini usiwaandikie barua ya kiofisi? Nadhani ni njia sahihi zaidi kuliko hii...
Mkuu, tumeandika barua mara nyingi sana, sasa sijui haziwafikii walengwa au ndio mambo mengi. Ndio maana nikaona kwa njia hii huenda ujumbe utawafikia haraka zaidi, au kama kuna mtu aliye na mawasiliano yao ya karibu basi anaweza kutusaidia kuwafikishia ujumbe huu.
 
mpe contacts za CDM ikiwamo email ya mtu muhusika na wengineo....pia hapa alipoweka hii issue ni mahala stahiki kwakuwa wapo wachambuzi ambao wanaweza juiboresha mada na kukisaidia chama katika wigo mpana wa siasa.

pia hapa napo ni kati ya maeneo machache ambayo viongozi wa cdm wote kwa nafasi zao hufika na kupata habari na kuchangia pia mijadala ijengayo kama hii.
 
Mtizamo wako ni mzuri.Ila kwa mbinu zinazohitaji kukisaidia chama ni vema zisiwe public.
 
Umeandika vizuri sana, ingeleta tija zaidi kama ungewaandikia kiofisi nao wangeweza kulichukulia suala kwa umuhimu uliotukuka. Hata hivyo mbinu ya kutumia udhaifu wa mwenzio kuwa ndio mtaji muda mwingine huwa haufanyi kazi sana hasa pale mwenye udhaifu huo akijitambua. Cha msingi ni kuwa na sera zenye tija kwa wananchi ambazo zinaleta uahueni wa maisha kwao. Nakupongeza kwa makala nzuri.
 
NtakuPM number ya jamaa anayejiandaa kuja hapo kumng'oa cheyo muangalie mtashirikiana vipi. au na wewe unataka kugombea?
 
kaka umeongea kitu cha msingi,na mi pia nipo bariadi sina muda mrefu lakini nimegundua CDM kipo chini sana pamoja na fursa zilizopo za kuiwezesha kulichukua hili jimbo,kuna hawa sisi tuliopo sisi tufanye kitu kwanza.tunaweza kutafutana kwa mkakati.
 
kaka umeongea kitu cha msingi,na mi pia nipo bariadi sina muda mrefu lakini nimegundua CDM kipo chini sana pamoja na fursa zilizopo za kuiwezesha kulichukua hili jimbo,kuna hawa sisi tuliopo sisi tufanye kitu kwanza.tunaweza kutafutana kwa mkakati
Mawasiliano yangu nimeyatoa, sasa nitafute tuweze kuingia kazini na mikakati zaidi.
 
It's well analysed input worthy appreciation. Na channel ya mawasiliano uliyoitumia ni sahii na kwa wakati sahii.

Wanaokumbuka uzi wa Ta Muganyizi kuhusu kutokuwepo au presence but on limited coverage kwa CDM Wilaya nzima ya Bukoba Vijijini.

Ukisoma threads zote ni kama zinarandana na kama hazirandani sana lakini muktadha ni ule kwamba CDM inahitaji kwenda na mikakati yake vijijini kule ili iamshe mioyo ya watu waliosononeka.

Na kazi hiyo ifanywe bila kuangalia udhaifu wa mpinzani-CCM maana imeonyesha vyama vyote ni dhaifu. Kimoja kina miundo mbinu ya kufika kwa Watanzania lakini kingine-CDM hakina. Chenye miundo mbinu kimeamua kulala. Mchangiaji mmoja amesema kinaweza kikaja kikatambua udhaifu wake. Hiyo sio ajabu maana wakati unaweza ukafika CCM kikaamua kutumia udhaifu wake (weakness) kuelekea kwenye nguvu (strength).

Hivyo basi CDM kinatakiwa kiwafikie watu na wanachama wake na kihakikisha are voting worthy-wana vitambulisho vya kupigia kura na takwimu zao ziko updated kwenye daftari la wapiga kura. Kazi hii si ndogo kama wanavyofikiri. Huwezi mtu kuifanya bila support and authority of party hierachy. Hivyo pamoja na uzalendo na kujitoa kwa wanachama bado uongozi wa juu wanahitaji kuwa regularist kwenye kueneza sera na mikakati ya CDM.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
kwakweli huu ni ushauri mzuri sana na ni vizuri kijana huyu akaungwa mkono ili kuleta mageuzi tarajiwa sehemu husika. Wanaohusika wasiupuuze.
 
Ushauri mzuri.lakini je kesi ya pingamizi kuzuia shughuli za siasa ilishaisha?nimechukua contact zako nitaku-connect na mtu ambae ameshaanza kupiganisha huko Old Maswa,mnaweza kuunganisha nguvu mkajipanga kwa mapambano ya ukombozi.
 
Mkuu, tumeandika barua mara nyingi sana, sasa sijui haziwafikii walengwa au ndio mambo mengi. Ndio maana nikaona kwa njia hii huenda ujumbe utawafikia haraka zaidi, au kama kuna mtu aliye na mawasiliano yao ya karibu basi anaweza kutusaidia kuwafikishia ujumbe huu.

Kuna ombwe la uongozi hapo katikati. Kuna watu wako CDM na ni viongozi lakini wapo kama hawapo kwani lengo lao ni maslahi kutoka chama sio kukiendeleza chama.
Kijana umejieleza vizuri sana. Na viongozi wa mkoa na wilaya wanatakiwa wakusikie na wakuelewe vilivyo. Wapambane kueneza sera kwa sasa. Bendera, vipeperushi na Tshirt ni michango yenu wenyewe mnatengeneza mnauziana wenyewe ila kadi hutoka makao makuu. Amkeni wananchi mabadiliko yaja.
 
safi sana...2015 kitaeleweka tu, nimeipenda hiyo Movement... eti JF ni CHADEMA na CDM ni JF?
 
Ushauri mzuri.lakini je kesi ya pingamizi kuzuia shughuli za siasa ilishaisha?nimechukua contact zako nitaku-connect na mtu ambae ameshaanza kupiganisha huko Old Maswa,mnaweza kuunganisha nguvu mkajipanga kwa mapambano ya ukombozi.
Hakuna kesi ya namna hiyo huku. Nitashukuru, niunganishe na huyo ndugu yangu maana wanasema "pamoja tutasimama ila kwa mmoja mmoja tutaanguka"! Ahsante.
 
Kwanini usiwaandikie barua ya kiofisi? Nadhani ni njia sahihi zaidi kuliko hii...

Huwa hawajibu.

Hata kwenye website yao inaelekea admin alichukua likizo ya muda mrefu -au account ya info@ haina mtunzaji.
 
Back
Top Bottom