Mbowe: CCM bila Polisi ni wepesi

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Mbowe.jpg

Mwenyekiti Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa katika uchaguzi huu mdogo wa marudio katika majimbo mawili ya Kinondoni na Siha jeshi la polisi liandae magereza ya kutosha kwani watawafunga wote na kudai hawawezi kukubali kura kuibiwa.

Ameyasema hayo kwenye kampeni za CHADEMA Magomeni jijini Dar es salaam ambapo amedai Chama Cha Mapinduzi (CCM) bila polisi ni wepesi na hawawezi chochote sababu chama hicho kimeshapoteza mvuto kwa wananchi.

“Yaani nyinyi polisi muachie CCM dakika tano tu wacheze ngoma siku ya tarehe 17 hawa jamaa ni weupe, na polisi ndugu zangu safari hii mtuandalie magereza mtatufunga wote haki ya Mungu, safari hii haibiwi mtu kura hiyo nawaambia mtatuua. Kama tumeweza kupona risasi 38 sasa tupo tayari kwa lolote, Wabunge wetu wanafungwa, wanafukuzwa Bungeni, madiwani wanalazimishwa kuhama chama, kila siku viongozi wa upinzani ni polisi na mahakamani,”amesema Mbowe

Hata hivyo, Mbowe amesema kuwa endapo watafanyiwa mambo ambayo walifanyiwa kwenye uchaguzi wa Kata 43 basi mambo hayawezi kuwa mazuri

Chanzo: Dar24
 
Kila mtu anajua hata sisonje anajua na dawa ya polisi ccm tunaishi nao mtaani dawa yao ndogo

Swissme
 
Chaguzi hizi ndogo zinazoendelea hapa nchini zinathibitisha kwamba hali ya Chama Cha Mapinduzi ni mbaya sana licha ya Mwenyekiti wake wa Taifa kujitahidi kuwaaminisha watanzania kuwa yeye ni Rais bora na Rais pendwa.
Nguvu inayotumiwa na vyombo vya dola kuibeba CCM ni kubwa Sana, kwa bahati mbaya sana CCM wanadhani kuwa watanzania ni wajinga na malimbukeni lakini kimsingi watu wanajua na wanatambua kila linaloendelea. Mambo haya Yana mwisho wake
 
kwani ukiambiwa umeshika dola maana yake nini? unashika dola bila polisi au jeshi au? kushika dola huko chadema tafsiri yenu huwa nini?
 
Siku Mungu akiwaamua kuwalipa mabaya yao hata huyo wanaemtegea asiyepingwa na kupangiwa atatangulia yeye....maana Mungu hudili na mzizi na kisha kuangusha mbuyu kabisa....siku itakuja, watatafuta msaada hautapatikana.
 
kwani ukiambiwa umeshika dola maana yake nini? unashika dola bila polisi au jeshi au? kushika dola huko chadema tafsiri yenu huwa nini?
we jamaa mweupe sana kichwani. Kwani Gadafi si na yeye alikuwa umeshika dola kama unavyosema.
 
Chaguzi hizi ndogo zinazoendelea hapa nchini zinathibitisha kwamba hali ya Chama Cha Mapinduzi ni mbaya sana licha ya Mwenyekiti wake wa Taifa kujitahidi kuwaaminisha watanzania kuwa yeye ni Rais bora na Rais pendwa.
Nguvu inayotumiwa na vyombo vya dola kuibeba CCM ni kubwa Sana, kwa bahati mbaya sana CCM wanadhani kuwa watanzania ni wajinga na malimbukeni lakini kimsingi watu wanajua na wanatambua kila linaloendelea. Mambo haya Yana mwisho wake
Uchaguzi kinondoni magu ajipime kutokurusha bunge uongozi wake kwa jumla yupo sahihi au afikirie upya ili watu wamuelewe
 
Mwenyekiti Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa katika uchaguzi huu mdogo wa marudio katika majimbo mawili ya Kinondoni na Siha jeshi la polisi liandae magereza ya kutosha kwani watawafunga wote na kudai hawawezi kukubali kura kuibiwa.

Ameyasema hayo kwenye kampeni za CHADEMA Magomeni jijini Dar es salaam ambapo amedai Chama Cha Mapinduzi (CCM) bila polisi ni wepesi na hawawezi chochote sababu chama hicho kimeshapoteza mvuto kwa wananchi.

“Yaani nyinyi polisi muachie CCM dakika tano tu wacheze ngoma siku ya tarehe 17 hawa jamaa ni weupe, na polisi ndugu zangu safari hii mtuandalie magereza mtatufunga wote haki ya Mungu, safari hii haibiwi mtu kura hiyo nawaambia mtatuua. Kama tumeweza kupona risasi 38 sasa tupo tayari kwa lolote, Wabunge wetu wanafungwa, wanafukuzwa Bungeni, madiwani wanalazimishwa kuhama chama, kila siku viongozi wa upinzani ni polisi na mahakamani,”amesema Mbowe

Hata hivyo, Mbowe amesema kuwa endapo watafanyiwa mambo ambayo walifanyiwa kwenye uchaguzi wa Kata 43 basi mambo hayawezi kuwa mazuri

Chanzo: Dar24
Timiza ahadi yako mwenyekiti.
 
Back
Top Bottom