Mbowe awatuhumu Rais na Waziri Mkuu kukataliwa kwa wagombea wa CHADEMA Bunge la EALA

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Baada ya matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki kutangazwa, huku wagombea wa Chadema wakipigiwa kura nyingi za hapana na hivyo kukosa nafasi, Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge alisema kuwa, hawayakubali matokeo hayo na kuwa watakwenda mahakamani.

Mbowe pia amemtuhumu Rais Dkt Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusika katika mchakato wa kuwakataa wagombea wa CHADEMA na kusema kuwa, wao hawatakubaliana na hilo kwa sababu Spika wa Bunge amekiuka kanuni za bunge, na uchaguzi wote ulikuwa wa kasoro.
3c5dc242d105c73f5a69907e22379e7f.jpg

My Take
Bunge linatakiwa liweke uzalendo mbele na liweke pembeni swala la itikadi zao inapofikia kwenye maswala ya kitaifa. Vinginevo tutaendelea kuwa wasindikizaji tu ndani ya EAC. Serikali iache utawala wa visasi. Ijikite kwenye maswala ya msingi kwa matakabali wa Taifa.
 
Baada ya matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki kutangazwa, huku wagombea wa Chadema wakipigiwa kura nyingi za hapana na hivyo kukosa nafasi, Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge alisema kuwa, hawayakubali matokeo hayo na kuwa watakwenda mahakamani.

Mbowe pia amemtuhumu Rais Dkt Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusika katika mchakato wa kuwakataa wagombea wa CHADEMA na kusema kuwa, wao hawatakubaliana na hilo kwa sababu Spika wa Bunge amekiuka kanuni za bunge, na uchaguzi wote ulikuwa wa kasoro.
Kura za hapana ni kupinga ukosefu wa machaguo na kutokukubalika kwa wagombea husika aache visingizio
 
MAMBO YA KUSHANGAZA

1. CHADEMA Hawajawahi kushindwa UCHAGUZI na HAWATASHINDWA MILELE bali huwa WANAIBIWA KURA tu

2.WANASHERIA wa CHADEMA hawajawahi KUSHINDWA KESI na WALA HAWATASHINDWA bali pale wanapo SHINDWA MAHAKAMA huwa ZIMETUMIKA na ZIMEKUWA za CCM na RAIS Ameziingilia

3.Siku ZOTE Haki itakuwa imetendeka pale tu Wanapokuwa wao CHADEMA Wameshinda KESI
 
Mbowe anatafuta pa kutokea ili asilaumiwe na wafipa.. Amefanya fyongo mwenyewe kama mwenyekiti as if hana washauri kisheria kuwa walilolifanya ni technical mistake
 
Back
Top Bottom