Ashasembeko
JF-Expert Member
- Dec 14, 2017
- 226
- 914
Katika viongozi ambao wamepitia katika changamoto nyingi miaka mitano iliyopita ni Freeman Mbowe anashika nafasi ya pili baada ya Tundu Lissu.
Tukianza na kwamba ameharibiwa biashara zake. Wamemvunjia Club Bilcanas, Mashamba yake Hai na wamelifungia gazeti lake.
Tukumbuke mwaka 2018 yeye na Esther Matiko walikaa jela karibia miezi sita na kunyimwa dhamana.
Kuna kipindi walitaka hadi kumpora chama.
Mwaka huu, yeye na viongozi wengine wa Chadema, walihukumiwa kifungo cha miezi mitano au faini ya million 350. Tunajua lengo lilikua kukifilisi chama kuelekea uchaguzi lakini waliumbuka baada ya wananchi kwa ujumla wao kuwachangia na kulipa faini yote.
Wakaona haitoshi, wakamshambulia katika makazi yake Dodoma ili asiweze kufanya kampeni. Wakaenda mbali na kumdhalilisha bungeni na kwenye magazeti yao ya propaganda wakasema eti alikuwa amelewa.
Na yule DC wa Hai anaemfanyia unyama kila kukicha. Juzi tu nyumba yake ilivamiwa na fundi wake kupigwa risasi. Wakaona haitoshi wakaenda mvamia hadi Hoteli aliyokuwepo.
Wakati uchaguzi unaendelea vijana wa Sabaya walimuweka kizuizini na hakuweza hata kwenda kupiga kura.
Leo tunaskia amekamatwa na polisi kwa kuchochea maandamano.
Huyu mtu hata kama upo CCM, anastahili heshima yako. Mambo aliyoyapitia na aliyoyapoteza binadamu wa kawaida hawezi kustahimili.
Ni wazi kuwa watawala wanamchukia sana Mbowe, na bado nashindwa elewa hii chuki inatoka wapi. Kwanini Mbowe?
Zitto Kabwe aliwahi hadi andika barua kuomba mkopo wa WB usitishwe ili hatuoni akisumbuliwa sana kama Mbowe – japo na yeye kapitia magumu pia.
Kuna nini nyuma ya haya mashambulio ya bwana Mbowe?