Mbowe amshangaa Selasini kujiuzulu nafasi ya Mnadhimu wa Upinzani Bungeni, asema sababu alizotoa hazina mashiko

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe amesikitishwa na uamuzi wa Mbunge wa Rombo Joseph Selasini wa kujiuzulu nafasi ya mnadhimu wa upinzani bungeni na kusema wazi sababu alizotoa hazina mashiko.

Mwenyekiti huyo wa CHADEMA ameshangazwa na taarifa ya Selasini kwamba hakuwahi kupewa barua ya uteuzi.Ameuliza kama hakupewa barua ya uteuzi imekuwaje aandike barua ya kujiuzulu?

Mbowe amesema Selasini ametumikia nafasi hiyo kwa miaka miwili kwa uaminifu na anaheshimiwa na wabunge wote wa upinzani huku akipewa ushirikiano wote na Ofisi ya Bunge. Amekuwa akihudhuria vikao vyote vya Kamati za uongozi na kulipwa posho.

Mbowe ameendelea kusema na kuuliza kama Selasini amefanya yote hayo ndani ya miaka miwili imekuwaje ashindwe kumalizia miezi minne iliyobaki kabla ya Bunge kuvunjwa?

Kiongozi huyo mkuu wa upinzani nchini ameonyesha wazi kutofurahishwa na uamuzi huo wa Mbunge Selasini na kusema labda kama ana mambo yake ya siri ndiyo maana ameamua kufanya hivyo.

Mwezi uliopita katika uchaguzi mkuu ndani ya chama Selasini alikuwa anagombea nafasi ya Mwenyekiti Kanda ya Kaskazini Lakini alipoteza nafasi hiyo kwa mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema.

Pia soma
i. News Alert: - Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ajiuzulu nafasi ya Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni
 
Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe amesikitishwa na uamuzi wa Mbunge wa Rombo Joseph Selasini wa kujiuzulu nafasi ya mnadhimu wa upinzani bungeni na kusema wazi sababu alizotoa hazina mashiko.

Kiongozi huyo mkuu wa upinzani nchini ameonyesha wazi kutofurahishwa na uamuzi huo wa Mbunge Selasini na kusema labda kama ana mambo yake ya siri ndiyo maana ameamua kufanya hivyo.
Naunga mkono hoja ya Mwenyekiti kuwa kuna baadhi ya wanachama na viongozi wengi tuu wa CHADEMA sio tu wana mambo yao, bali kuna baadhi wameisha jitambua, hivyo wanasubiri tuu muda muafaka ufike baada ya kuvunjwa Bunge wafanye yao!.

P
 
Mheshimiwa Selasini, amejiuzulu kwa heshima na kwa bustara. Sidhani sababu zilizo mfanya ajiuzulu ni kutopewa barua ya uwakilishi, bali kuna jambo kubwa na ameliona sio kuliweka hadharani.

Wengi wanajua lilitokea Arusha kwenye uchaguzi wa ndani chadema, selasini ilikuwa achukue jimbo na alishauriwa na viongozi wengi na wazee wengi wa kanda, lakini team Mbowe hawakutaka hilo, palikuwa na vuta ni kuvute nyingi sana, vitisho na hongo nyingi zilitepenbea, ili selasini asishinde.

Maoni yangu ni kuwa Selasini na busara zake hazitakiwi na baadhi ya viongozi chadema.

Lakini mbona kiongozi yoyote chadema akiwa na mawazo tofauti na akifanya uamuzi wake , ataitwa msaliti,mwizi, hajielewi . Hakuna kumsikiliza, kushauriana au hata kufanya kikao cha kumsikiliza. Ni wakati muafaka ikaundwa kundi la wazee wastaafu wenye busara, wakapewa jukumu la kusikiliza matatizo ya viongozi na wanachama, na kutoa ushauri kwa kamati kuu ya chama, badala ya udikteta na kutukanwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu leo umemuunga mkono Mwenyekiti? Tupe sababu za kuunga mkono
No sio mara ya kwanza kuunga mkono hoja za Mwenyekiti Mbowe, akifanya vizuri huwa nampongeza.

As of now tunavyoandika humu, kuna wengi Chadema wameisha amua to do the right thing ila wanalazimika kuendelea kuwepo Chadema wakiwa wapo wapo tuu, mwili Chadema, roho au moyo elsewhere wakisubiri muda muafaka!.

Ili waweze kufanya yao ule wakati muafaka utakapo wadia, wanatafuta vijisababu ili kutengeneza bifu fulani ili wakiamua ionekane ndio sababu, kumbe Mwenyekiti tayari ameisha washtukia kabla.

NB kumuunga mkono Mwenyekiti sikuanza leo

P
 
"Molemo, post: 34090922, member: 65674"]
Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe amesikitishwa na uamuzi wa Mbunge wa Rombo Joseph Selasini wa kujiuzulu nafasi ya mnadhimu wa upinzani bungeni na kusema wazi sababu alizotoa hazina mashiko.
Kwanza, naamini taarifa labda kama kutakuwa na Molemo mwingine.
Pili, suala hapa si mashiko ya sababu, ni je sababu alizoeleza ni za kweli au la
Mwenyekiti huyo wa Chadema ameshangazwa na taarifa ya Selasini kwamba hakuwahi kupewa barua ya uteuzi.Ameuliza kama hakupewa barua ya uteuzi imekuwaje aandike barua ya kujiuzulu?
Mnaona hapa! haya ndiyo tunayosema kuwa Mbowe ana matatizo ya uongozi.

Mwenyekiti ana fursa ya kueleza nini kimetokea si kuuliza maswali.
Swali asilojibu Mbowe: Je, alimpa barua ya uteuzi?
Je, alimtambulisha kwa barua katika uongozi wa Bunge?
Mbowe anatakiwa aeleze siyo aulize maswali. Hakuna mwenyekiti mwingine wa kujibu hoja za Selasini isipokuwa yeye na yeye tu
Mbowe amesema Selasini ametumikia nafasi hiyo kwa miaka miwili kwa uaminifu na anaheshimiwa na wabunge wote wa upinzani huku akipewa ushirikiano wote na Ofisi ya Bunge. Amekuwa akihudhuria vikao vyote vya Kamati za uongozi na kulipwa posho.
Selasini kasema hayo.

Hoja si posho, je, alitambulishwa rasmi? Je, Mbowe alimpa barua ya maandishi kuhusu uteuzi? Posho anaweza kupewa mwakilishi yoyote, haijibu hoja za Selasini.
Mbowe ameendelea kusema na kuuliza kama Selasini amefanya yote hayo ndani ya miaka miwili imekuwaje ashindwe kumalizia miezi minne iliyobaki kabla ya Bunge kuvunjwa?
Mbowe, ajibu hoja za Selasini kwa mistari si kuuliza maswali.

Selasini kushindwa kuendelea haijibu hoja alizotoa.

Kwa hili unawezaa kuona jinsi Mbowe anavyobabaika.
Mwenyekiti anauliza wanachama maswali badala ya kuwapa majibu!
Kiongozi huyo mkuu wa upinzani nchini ameonyesha wazi kutofurahishwa na uamuzi huo wa Mbunge Selasini na kusema labda kama ana mambo yake ya siri ndiyo maana ameamua kufanya hivyo.
Kama ana mambo yake binafsi ya siri au ya wazi hayo si majibu ya hoja zake. Mbowe anatakiwa aeleza, je alimkaimisha nafasi hiyo kwa maandishi?
Je, alimtambulisha kwa maandishi katika uongozi wa Bunge?Je, anachosema Selasini ni uongo?
Mwezi uliopita katika uchaguzi mkuu ndani ya chama Selasini alikuwa anagombea nafasi ya Mwenyekiti Kanda ya Kaskazini Lakini alipoteza nafasi hiyo kwa mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema.
Angalia kauli hizi za Mwenyekiti.

Yaani badala ya kutolea ufafanuzi sintofahamu yeye anachomeka hoja nyingine.

Mambo ya uchaguzi hayajibu hoja za Selasini.
Mbowe anakigawa chama badala ya kuwaunganisha wananchi.

Kama hayo na uzi huu ni kauli za Mbowe, hii ni fedheha kubwa sana kwa Chadema!

Mwenyekiti anauliza maswali badala ya kutoa ufafanunuzi!

Kama uzi ni sahihi, Selasini ana hoja, Mbowe hana majibu.
 
Mkuu leo umeunga mkono M/kiti?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi ni mkweli daima, ukiwa mkweli, utasimama kwenye kweli wakati wote. Mwenyekiti Mbowe akifanya mazuri, nampongeza na hii sii mara ya kwanza kumpongeza Mbowe, tena kuna wakati hadi nilimuanzishia thread ya pongezi humu.

P
 
Back
Top Bottom