labda alikua anaongea kwa mafumbo.Jamani si nimemsikia mbowe mwenyewe akisema kuwa hata ikibidi ngumi zitapigwa!
Mbowe hana vilipulio kile kichwa hakina kitu haiwezekani uishie kidato cha nne uje umlipue msomi kama jk sijui ataanzia wapi yeye ishu zake ni muziki tu.
vya kujifunia mbona vingi,piga picha Tanzania ya miaka ya 60 kisha fastforward Tanzania ya miaka ya 2000,uone tofauti.Hao wanaojiita wasomi tz wanawezakujivunia nini kwa wananchi wao? na wananchi wanakuonaje na usomi wako fanya uchunguzi wa elimu yako usije ukawa watu wanakucheka kila ukigeuka.
Unapotea ndugu mbowe alikimbia shule mapema c yupo kimaslah zaid? CCM bado ina miaka 100 ya kutawala
Kwa mbowe kuheshimu maoni ya wananchi ni kukubaliwa serikali tatu kama anavyotaka yeye na wakati huohuo hakuna ushahidi kuwa wananchi wote wanataka serikali tatu.
Yeye ndo anaforce anachotaka kiwe,wakati jk ashasema hata yeye hajui mwisho kutakubalika serikali ngapi.
Suala la mbowe kurudi kwa wananchi kama matokeo anayotaka yeye hayatapita halina impact kwani limeshazoeleka wao kwenda kuuza sura kwa chopa.
Huyu ana div 1 point 7Chanzo: Tanzania Daima.
Mmiliki wa gazeti: DIV Zero
Aliyeipua: DIV Zero
Mwenye CV ya mbowe atuwekee hapa, naona anongea kama mtu alieishia std 7.
Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
Ila anaongoza Chama Kikuu cha upinzani na ana pesa kuliko wewe!Mbowe ni mgumu sana wa kuelewa ndio maana ilikuwa ngumu kuendelea na shule
Asingeweza kuendelea na shule kwa sababu akili yake siyo ya shule ni ya mziki zaidi shule haiko upande wake.
[h=2]
[/h]JUMANNE, FEBRUARI 04, 2014 06:52 NA KULWA KAREDIA
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amemjibu Rais Jakaya Kikwete kwamba asiingize utani katika masuala mazito ya taifa. Mbowe alisema Katiba ya Tanzania, itaamuriwa na wananchi wenyewe na si Chama Cha Mapinduzi (CM) ambacho kimekuwa na mkakati mkali wa kutaka kuua maoni ya wananchi.
Mbowe ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tu baada ya Rais Kikwete kudai amesikia kiongozi huyo wa upinzani akitangaza kutumia nguvu kupata Katiba mpya.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo juzi kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, wakati akihutubia sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa CCM. Alisema amesikitishwa na kauli hiyo na kuwataka Watanzania kutobabaishwa.
Kikwete alisema Katiba mpya itapatikana kwa hoja za kila upande kulingana na mapendekezo yake.
Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Mbowe alisema Rais Kikwete hapaswi kuchukulia utani katika mambo mazito ya taifa.
Namuomba Rais Kikwete asichukulie utani mambo ya taifa suala la Katiba mpya. Anapaswa kuzungumza mambo ya msingi ambayo yanaleta tija.
Siku zote Katiba ya nchi inapatikana kwa dhamira nzuri lakini tumebaini wenzetu hawa CCM hawaheshimu hoja za wananchi.
Hebu tujiulize jinsi Jaji Joseph Warioba alivyotumia fedha nyingi kukusanya maoni ya Watanzania, leo CCM hao hao wanayakataa tuwaeleweje? alihoji Mbowe.
Alisema Jaji Warioba ametoa hoja za msingi lakini kwa sababu ya uoga wa CCM wanataka kupindisha ukweli wa mambo.
Mzee wa watu huyu amezunguka taifa zima kwa fedha za walipa kodi wa nchi hii, sasa wanataka watumie wabunge wao kukwamisha mchakato huu,alisema Mbowe.
Alisema kama utawala wa Rais Kikwete utashindwa kuleta Katiba mpya ambayo inakidhi matakwa ya Watanzania, wao wataendelea kudai utawala mpya utakapoingia madarakani uwe ni wa Chadema au CCM.
Nawahakikisha Watanzania, ikija Katiba mbaya tutaendelea kuidai kwa nguvu zote iwe CCM imeingia madarakani au sisi, Kikwete awe madarakani au asiwepo hatulali kamwe.
Katiba ni maridhiano ambayo yanabeba maoni ya Watanzania sasa kwa nini CCM hawataki kuyafuata? alihoji Mbowe.
Alisema CCM haina hatimiliki ya Katiba mpya na kwamba wakati wa kufanya uamuzi mgumu wa kupindisha maoni ya Watanzania umefika.
Hawa watu hawana hatimiliki ya Katiba mpya, kwa nini wanajawa uoga kiasi hiki? Wanaogopa serikali tatu, nakwambia sitaki utani kwenye ya msingi,alisema Mbowe.
NJE YA BUNGE
Mbowe alisema atahakikisha wanajadiliana vya kutosha ndani ya Bunge kuona haki inatendeka.
Tutabishana kwa kila namna ndani ya Bunge,wakituzidi kete kwa rafu zao bungeni tutarudi kwa wananchi kuwashitaki maana hawa ndiyo walengwa hatutaki kufika huko kama kila mtu ataweka busara zake chini.
Dhamira ya CCM ndiyo inatufanya tutoe kauli hizi lakini nakwambia hapa hakuna mcheza ngumi hoja ndiyo jambo la msingi tu,tutatumia maandamano nchi nzima maana haya ni haki ya msingi ya kila mtu,alisema Mbowe.