Mbowe akosoa Maagizo ya kamatakamata ya Magufuli

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Dar es Salaam. Si wote wanaoweza kuunga mkono hotuba iliyojaa maagizo ya utendaji ya Rais John Magufuli, na mmoja wa wakosoaji ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye amemulika matumizi ya sheria ya kuweka watu mahabusu kwa saa 48.

Magufuli alitoa maagizo takriban sita kwa wakuu wapya wa mikoa aliowaapisha Jumanne, akiwataka wakomeshe ujambazi, kuzuia mchezo wa pool table nyakati za asubuhi, kuondoa wafanyakazi hewa, kutekeleza sera ya elimu bure, kusimamia ilani ya CCM, kuacha kupiga na kutimiza wajibu, na zaidi ya yote kuwataka kuwakamata na kuwaweka mahabusu watendaji wanaonyanyasa wananchi.

Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa upinzani bungeni, alisema maagizo ya mkuu huyo wa nchi, hasa ya kuwapa madaraka makubwa wakuu wa mikoa, yana kasoro na yanaweza kuchangia kuvuruga utendaji kazi na kuzua mgongano.

Mwenyekiti huyo wa chama hicho kikuu cha upinzani alianzia na suala la kuwapo kwa wakuu wa mikoa na wilaya, akisema ni kuendeleza mfumo wa kikoloni kwa kuwa wananchi hawakuwachagua wao kuwatumikia.

Alisema wananchi waliwachagua madiwani, wabunge na Rais ili wawatumikie, lakini wakuu wa mikoa na wilaya ni watu wanaopandikizwa kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa Malkia Elizabeth wa Uingereza aliyekuwa akipeleka magavana kutawala wazalendo.

Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997 inampa mkuu wa mkoa au wilaya madaraka ya kumuweka mahabusu mtu ambaye ataona kutolala rumande kunaweza kuhatarisha amani na utulivu na hakuna njia nyingine ya kumdhibiti zaidi ya kumlaza rumande.

Lakini sheria inataka mtu aliyelazwa mahabusu afikishwe mahakamani ndani ya saa 48 na kama haitafanyika, aachiwe huru na asikamatwe tena kwa kosa hilo.

Alisema kitendo cha kuwapa wakuu hao mamlaka ya kukamata watu, kinafanya polisi wasiwe na kazi ya kufanya.

“Polisi watafanya kazi gani, wanasheria watafanya kazi gani,” alisema.

Alifafanua kuwa Sheria Namba 10 ya Serikali za Mitaa inaeleza majukumu ya madiwani liwa ni pamoja na kuwasimamia wananchi katika kila jambo, huku kukiwa na kamati maalumu za kusimamia vitu muhimu kama elimu, afya na maji.

Mbowe alitoa mfano wa Jiji la Dar es Salaam, ambako wananchi wamewachagua viongozi kutoka Chadema na CUF katika ngazi ya udiwani, lakini mkuu wa mkoa ni CCM, kitu ambacho alisema kitasababisha malumbano kutokana na kila upande kujiona una haki.

Alisema watakaokuwa huru kutimiza majukumu yao bila kuingiliwa wala kubughudhiwa na watendaji wa halmashauri ni viongozi kutoka CCM.

“Majiji ya Mwanza, Arusha na Dar yamekuwa yakikumbana na migogoro hii ya mwingiliano wa utendaji mara nyingi kutokana na maelekezo wanayopewa na wakuu wa mikoa,” alisema.

“Kibaya zaidi mikoa mingi ina wakuu ambao ni wanajeshi. Hawakufundishwa kulinda raia bali kuumiza. Kwa rungu hili, hali itakuwa mbaya,” aliongeza.

Mbowe aliunga mkono agizo la Magufuli la kukomesha malipo ya wafanyakazi hewa, akisema jambo hilo linapaswa kukemewa na kumalizwa kwa kuwa kutumia Sh500 bilioni kuwalipa ni kupoteza fedha nyingi.

Hata hivyo, alisema wafanyakazi hewa wanaozungumzwa ni wale wadogo ambao malipo yao si makubwa.

“Haiwezekani mkurugenzi, mhasibu au mkuu wa idara fulani akafungwa halafu isigundulike na akaendelea kulipwa mshahara,” alisema na kuongeza: “Tatizo ni uanzishaji wa mikoa, wilaya, kata, mitaa na vijiji kila utawala mpya unapoingia madarakani.”

Alisema suala hilo la kuanzishwa maeneo hayo ya utawala linaweza kufurahiwa na wananchi, lakini linatumia fedha nyingi, hasa za mishahara, kuongeza idadi ya watumishi wa umma na kuhitajika fedha nyingi za kuhudumia ofisi mpya. Alisema licha ya baadhi ya mambo katika hotuba kuwa na tija, mengi yana usumbufu ikiwamo utaratibu wa kufanya kazi kwa kutoa maelekezo bila kuunda mfumo wa kusimamia.

“Upo wapi ufanyaji usafi aliouanzisha ambao uliungwa mkono na nchi nzima. Kama angeandaa mfumo bila shaka hadi leo kungekuwa na siku maalumu ya kufanya hivyo,” alisema wakati akizungumzia uamuzi wa kufuta sherehe za Uhuru ili siku hiyo itumike kufanya usafi.

Akizungumzia hotuba hiyo ya maagizo, mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba alisema hakuna shaka kila mtu anataka vijana wafanye kazi, lakini kwa bahati mbaya hakuna ajira wala viwanda.

Alisema wakati wa utawala wa Baba wa Taifa vijana wasiokuwa na kazi walikuwa wanarudi vijijini wakalime kwa sababu kulikuwa na mashamba, lakini kwa sasa wamepewa wawekezaji.

“Badala ya kupanga kuwakusanya na kuwaweka kwenye kambi, wawaandalie maeneo ya kufanya kazi kama kuwahakikishia wale waliopoteza fedha kwenda vyuo vya ufundi ambao hawana kazi,” alisema na kuongeza:

“Utendaji wa sasa utasababisha Magereza kujaa kwa sababu kila mtu atataka aonekane anafanya kazi kwa kuwawajibisha wa chini yake, hali hiyo itaondoa ushirikiano katika utendaji na kuleta visasi na chuki.
 

Attachments

  • imgres.jpg
    imgres.jpg
    5.1 KB · Views: 59
Wakurugenzi kwani huwa wanachaguliwa na wananchi? Kinachitakiwa hapa ni kufanya kazi kwa maslahi ya wananchi na si UCCM au UCHADEMA,vijijini mashamba yapo.

Tatizo mnakula chips mjini na kulegeza suruali tu. Njooni huku Ruvu tulime vitunguu.Ekari moja kukodi ni 150K tu.Sasa kaeni huko mwishowe mpigwe 48 ndani.
 
Utawala wa sheria ufuate mkondo wake na siyo kuswekana ndani bila utaratibu!!
 
Sjaona football ikichezwa saa nne asb labda kwa special case...ulaya wanacheza usiku hata huku wanaanza sa kumi baada ya masaa ya kazi
 
Anachofanya Magufuli ndicho upinzan walikitaka yaani wataumia awamu hii kusubiri Rais aongee na wao watoe tamko hawajui kuusoma upepo kila aongeacho Rais kwa watanzania wa chin kwao ni OK , hivyo upinzani jiangalieni jamaa akipewa na chama hali itakuwa hatarii sana kwenu
 
Anachofanya Magufuli ndicho upinzan walikitaka yaani wataumia awamu hii kusubiri Rais aongee na wao watoe tamko hawajui kuusoma upepo kila aongeacho Rais kwa watanzania wa chin kwao ni OK , hivyo upinzani jiangalieni jamaa akipewa na chama hali itakuwa hatarii sana kwenu[/QUOTE]
Wapinzani hawataki maigizo tu
 
Naona ujinga uliokaa kwa Mbowe. Wakurugenzi kwani huwa wanachaguliwa na wananchi? Kinachitakiwa hapa ni kufanya kazi kwa maslahi ya wananchi na si UCCM au UCHADEMA,vijijini mashamba yapo.

Tatizo mnakula chips mjini na kulegeza suruali tu. Njooni huku Ruvu tulime vitunguu.Ekari moja kukodi ni 150K tu.Sasa kaeni huko mwishowe mpigwe 48 ndani.

Umesema ardhi ipo halafu unasema kukodi.
Hii ina maana kijana atahitaji kianzio cha kukodi, kula, kununua pembejeo na kuhudumia shamba hadi litoe mazao.
Vijana wa mijini hasa Dar ndio wengi hawana ajira kwa sababu walizaliwa mjini. hawajawahi kuwa na ardhi na hawana mtaji. wengine ni wasomi wazuri tu lakini hawana ajira.

Ardhi iliyoko pembeni mwa mji wa Dar na mikoa ya jirani sehemu kubwa iko mikononi mwa wawekezaji na matajiri miongoni mwao wanasiasa. Kijana akitaka ardhi lazima anunue au akodi.

Kwa hivi wazo la kusema wakalime ni la kizamani sana enzi za mwalimu enzi ambazo ardhi ilikuwa huru. vijana wa mjini watalimaje wakati hawajafunzwa kilimo hata mababa zao na hata mababu zao walibobea mijini.

Ikiwa tunataka vijana walime hatuamuru tu bali tunaanzisha shule na vyuo na taasisi za kilimo na huko tunawapeleka vijana kujifunza kilimo na kisha kuwapa mitaji hata kwa kuwakopesha.

TATIZO WATANZANIA TUNAENDA ZAIDI KISHABIKI BILA HATA CHEMBE YA KUFIKIRI
 
Waandishi wa habari ni watu wa hatari sana na wanaweza wakasababisha tafaruku kwenye jamii.
Mh. raisi hakukataza pool, alicho kataza ni vijana wanao cheza pool kwanzia asubuhi badala ya kutafuta kazi, labda suala la kazi ni ngumu kidogo lakini inachotakiwa ni vijana kukazana kujitafutia mbinu za maendeleo.

Kama kazi ni ngumu kupatikana basi wajisomee, watafute elimu. siku hizi kila mtu ana smart phone, na anaweza kutumia internet na kuna masomo mengi tu yako kwenye internet. Si rahisi kupata degree kwa kutumia internet lakini kuna mambo mengi ya kujifunza. Ukitaka kufuga, kulima, kutengenza gari, computer, welding kila kitu kiko kwenye internet na ni bure.

Mh raisi ametoa mfano mzuri wa Philipine ambya alikua maskini kuliko Tanzania na walikua wananunua korosho hapa Tanzania sasa wanaongoza ku export dunia nzima. yote hayo imetoka na juhudi za wananchi wao.
Watu wanalalamika hakuna mashamba, mashamba yapo, si lazima ununue shamba, unaweza kukodisha.

Huko kijijini mwenyewe nina heka zangu kadhaa na kuna hao wazee wenye mashamba Yao makubwa tu, uwezo wao wa kulima ni heka 3 kwingine ni pori tu, na vijana wao ndio hao wanao hangaika na pool.
Mh raisi anacho taka ni kwamba kuzuia sula la njaa. kwanini tuwe na njaa wakati kuna ardhi, kuna vijana, na kuna hali ya hewa nzuri,

Cha muhimu ni kuomba sasa njia muafaka ya ukulima na ufugaji, mazao yapate ununuzi na bei nzuri. Na tujifunze njia ya kisasa ya ukulima na ufugaji.
Suala la maendeleo si la chama, ni la watanzania wote.
 
Umesema ardhi ipo halafu unasema kukodi.
Hii ina maana kijana atahitaji kianzio cha kukodi, kula, kununua pembejeo na kuhudumia shamba hadi litoe mazao.
Vijana wa mijini hasa Dar ndio wengi hawana ajira kwa sababu walizaliwa mjini. hawajawahi kuwa na ardhi na hawana mtaji. wengine ni wasomi wazuri tu lakini hawana ajira.
Ardhi iliyoko pembeni mwa mji wa Dar na mikoa ya jirani sehemu kubwa iko mikononi mwa wawekezaji na matajiri miongoni mwao wanasiasa. Kijana akitaka ardhi lazima anunue au akodi.
kwa hivi wazo la kusema wakalime ni la kizamani sana enzi za mwalimu enzi ambazo ardhi ilikuwa huru. vijana wa mjini watalimaje wakati hawajafunzwa kilimo hata mababa zao na hata mababu zao walibobea mijini
Ikwa tunataka vijana walime hatuamuru tu bali tunaanzisha shule na vyuo na taasisi za kilimo na huko tunawapeleka vijana kujifunza kilimo na kisha kuwapa mitaji hata kwa kuwakopesha.
TATIZO WATANZANIA TUNAENDA ZAIDI KISHABIKI BILA HATA CHEMBE YA KUFIKIRI
Basi kacheze pool …!! Maana unalialia mpaka huruma…!!
 
Taifa ombaomba lakini vijana ambao ni nguvu kazi wanacheza pool asubuhi! Nchi nyingi wameweka sheria muda wa kufungua bar na muda wa kuuza pombe, hata hapo Kenya wamepitisha sheria kuhusu muda wa kuuza pombe. Sisi tunabishana kuhusu vijana kushinda kwenye vilabu wakicheza pool!

Na mkitaka kujua unafiki wa Mbowe, nendeni Kijijini kwake Machame mtafute hata bar moja yenye vijana wanaocheza Pool asubuhi.
 
Brown73
umetumia lugha nzuri na ya upole kufafanua kauli ya rais

nilivyoelewa, nikwamba watakamata kwa nguvu vijana na kupeleka makambini kufanya kazi...

hapo hiari ya kijana itakuwa haipo, na utakuwa utumwa mpya...
 
Taifa ombaomba lakini vijana ambao ni nguvu kazi wanacheza pool asubuhi! Nchi nyingi wameweka sheria muda wa kufungua bar na muda wa kuuza pombe, hata hapo Kenya wamepitisha sheria kuhusu muda wa kuuza pombe. Sisi tunabishana kuhusu vijana kushinda kwenye vilabu wakicheza pool!

Na mkitaka kujua unafiki wa Mbowe, nendeni Kijijini kwake Machame mtafute hata bar moja yenye vijana wanaocheza Pool asubuhi.
Kabla ujamwita Mbowe ni mnafki acheni kwanza maigizo kwa Watanzania
 
Back
Top Bottom