Mbowe akana kuwapo kwenye maandamano

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
613
1,776
MWENYEKITI Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amedai mahakamani siku ya tukio hakushiriki na hakuwapo kwenye maandamano ya wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakielekea kwenye ofisi za msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni.

Mbowe anaendelea siku ya pili na ushahidi wa utetezi katika kesi inayomkabili na vigogo wenzake wanane wa CHADEMA dhidi ya mashtaka 13 ikiwamo uchochezi.

Ushahidi huo unasikilizwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Akiongozwa na wakili wa utetezi, Peter Kibatala, Mbowe alidai kuwa pamoja na kutajwa na kuhusishwa na maandamano hayo, lakini hakuwapo eneo la tukio na kwamba ilikuwa na hisia tu.

Alidai kuwa baada ya kumaliza mkutano wa kufunga kampeni katika viwanja wa Buibui, Mwanyamala aliindoka uwanjani hapo akiongozwa na askari polisi kuelekea Makao Makuu ya CHADEMA, Kinondoni.

Alidai siku hiyo wafuasi wa CHADEMA wakiwa njiani walikutana na wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), katika makutano ya Barabara ya Morocco na Mwananyamala wakiwa na mgombea wao wakisindikizwa na ngoma aina ya mdundiko.

Mbowe alidai kuwa wanachama hao walikuwa wakiongozwa na polisi kuelekea Barabara ya Morocco na hakujua kilichoendelea nyuma kwa kuwa aliendelea na safari yake ya kuelekea Makao Makuu ya CHADEMA.

Akizungumzia kufikishwa kwake mahakamani, Mbowe alidai kwa mara ya kwanza alipokea wito wa kuitwa polisi kupitia mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Pia, alidai kuwa Kamanda huyo alitoa wito kwa viongozi wa CHADEMA kuripoti polisi kuhusu tukio hilo la maandamano.

Vile vile, alidai kupata taarifa kuhusu kifo cha Akwilina Akwiline, aliyepigwa risasi katika maandamano hayo kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari na kwamba polisi inawashilikia askari kuhusu tukio hilo.

Alidai kuwa hajawahi kula njama na washtakiwa wenzake bali waliitwa kwa nyakati tofauti kwenda polisi.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.

Wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji jinai kati ya Februari Mosi na 16, 2018, Dar es Salaam.

======

*Maswali na majibu, Kisutu, Tue. 5th Nov. 2019*

*Kesi namba 112/2018 inayowakabili Viongozi Wakuu wa Chadema, katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam, iko katika hatua ya washtakiwa kujitetea kwa kutoa ushahidi wao. Shahidi wa kwanza ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe Freeman Mbowe.*

Kibatala - Hali ilikuwaje Kinondoni siku ya kufunga mkutano?

Mbowe - Kulikuwa na movement nyingi za wananchi wengi, mashabiki, wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa ikiwa ni siku ya kufunga kampeni za uchaguzi

Kibatala - Kuna uhusiano gani kati ya Barabara ya Mwanyamala na Kawawa?

Mbowe - Barabara ya Mwananyamala imekutana na Kawawa road kwenye junction ambayo Kaskazini inaelekea kukutana na Ali Hassan Mwinyi Road na Kusini inaenda Magomeni junction inapokutana na Morogoro road na pembeni ya Barabara ya Kawawa kuna uwanja wa Biafra ulipokuwa ukifanyika mkutano wa kufunga kampeni za Ccm siku hiyo.

Kibatala - Inaanzia wapi barabara ya Kawawa?

Mbowe - Inaanzia Ali Hassan Mwinyi upande wa Kaskazini inaungana na Morogoro road Magomeni junction.

Kibatala - Kwa ufahamu wako, mtu aliyetoka mkutano wa CCM Biafra, akitaka kwenda labda Posta au Mbezi Luis anapitia wapi?

Mbowe - atapita barabara hiyo hiyo ya Morocco au Kawawa road

Kibatala - Mtu ambae alihudguria mkutano wa Chadema Uwanja wa Buibui yeye atapita wapi?

Mbowe - Atapita barabara hiyo hiyo ya Morocco au Kawawa road

Kibatala - Mawakala idadi yao 600 wakitoka ngome au sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili ya kuratibu uchaguzi wanapita wapi?

Mbowe - barabara hiyo ya Morocco au Kawawa road

Kibatala - Mawakala walipita wapi kwenda ngome?

Mbowe - Kawawa road

Kibatala - kwa ufahamu wako uondokaji wananchi waliohudhuria mkutano wa Chadema ulikuwaje?

Mbowe - Kwenye mikutano ya siasa, wengine wanaondoka kwa miguu, wengine kwa magari wakielekea pande za mashariki, magharibi.

Kibatala - Neno moja tu inakuwaje?

Mbowe - Mikutano ya kufunga kampeni inakuwa na hamasa kubwa shamra shamra, watu wanaimba, wengine wakicheza vigoma

Kibatala - Hii inakuwa ni Chadema tu?

Mbowe - Hapana hii inakuwa kwa vyama vyote kwenye mikutano ya hadhara

Kibatala - Unasema nini kuhusu uondokaji wa wafuasi wa CCM kwenye mkutano?

Mbowe - Jambo pekee ninaloweza kukumbuka, katika junction ya Mwananyamala na Kawawa walikutana wafuasi wa CCM wakiwa na mgombea wa Ccm

Kibatala - Hali ya uondokaji wa wanaCCM ilikuwaje?

Mbowe - walikuwa na shamra shamra wakiwa kwenye gari akishangiliwa na wafuasi wao kwa ngoma almaarufu mdundiko

Kibatala - Uwepo wa polisi ulikuwaje?

Mbowe - Kuna polisi waliongoza watu wetu mpaka Mwananyamala junction, hapo ndipo tulikutana na mgombea wa CCM, baada ya hapo polisi waliendelea kudeal na watu wengine.

Kibatala - wali-deal na watu gani?

Mbowe - Polisi waliendelea kuongoza msafara wa CCM, wakielekea Mwananyamala

Kibatala - Sasa ieleze Mahakama ni kwa namna gani Polisi wali-deal na CCM?

Mbowe - Sina uhakika sana walifanya nini sababu I was in movement

Kibatala - Ulitokaje jukwaani baada ya mkutano?

Mbowe - Viongozi tulitoka jukwaani, mimi binafsi nilitoka nikaelekea Makao Makuu ya Chama kwa kutumia gari.

Kibatala - Makao Makuu ya Chadema yapo wapi?

Mbowe - Kata ya Kinondoni nyumba namba 169 na 170 Mtaa wa Ufipa, ili kufika Mtaa wa Ufipa kutokea uwanja wa Buibui unapita Mwananyamala road kwa upande wa Mashariki alafu unakuta junction ya Mwananyamala, kisha unaenda Kaskazini unakuta junction ya Morocco na Kawawa unakata kulia kama mita 150 then kushoto.

Kibatala - Mara ya kwanza polisi ku-deal na wewe ulitokea wapi, ulifikaje polisi?

Mbowe - niliitwa na polisi siku 2 au 3 baada ya tukio lile la tarehe 16

Kibatala - Uliitwa wapi?

Mbowe - Makao Makuu ya Polisi Kanda ya Dar es salaam

Kibatala - Uliitwa polisi kwa njia gani au ulijuaje unaitwa?

Mbowe - Kupitia mkutano na waandishi wa habari

Kibatala - Nani alizungumza kwenye mkutano huo?

Mbowe - Kamanda Mambosasa

Kibatala - alisemaje?

Mbowe - aliongea mambo mengi, kati ya hayo ni kupigwa risasi Akwilina

Kibatala - Kamanda Mambosasa alisema ni nani alimpiga risasi Akwilina?

Mbowe - Hakusema ni nani, lakini alisema, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi

Kibatala - Mambo mengine ni yapi alisema?

Mbowe - alitoa wito kwa viongozi wengine Chadema kuripoti Polisi Makao Makuu ya Polisi Kanda ya Dar es salaam 2nd floor Wilaya ya Ilala.

Kibatala - Alitaja Viongozi wa Chadema ?

Mbowe - Alinitaja mimi specific

Kibatala - Kabla ya press conference ya Mambosasa ni afisa gani wa polisi wa cheo chohote alitaka uripoti polisi

Mbowe - Sikuwahi kuitwa

Kibatala - Kati ya kipindi cha mkutano na tukio lile ulikuwa wapi?

Mbowe - Nilikuwa Dar nikiendela na shughuli zangu ikiwemo kuratibu uchaguzi kama Kiongozi wa Chama.

Kibatala - Uratibu huo unakuwaje ?

Mbowe - Uratibu huo unahusisha mambo mengine, kujua idadi ya mawakala wetu ni wangapi katika vituo.

Kibatala - Uliratibu kutoka wapi?

Mbowe - Makao Makuu ya Chadema

Kibatala - Malalamiko mengine uliyopokea?

Mbowe - Malalamiko mengi ya mawakala wetu

Kibatala - malalamiko gani?

Mbowe - Kunyimwa barua za utambulisho

Kibatala - Ulishughulikiwaje?

Mbowe - Kuwasiliana na Msimamizi wa Uchaguzi, huku polisi wakiwazuia kuingia kwenye vituo vya kupigia kura.

Kibatala - Mawakala hawa walienda wapi?

Mbowe - kwa Mkurugenzi kufuata barua.

Kibatala - Waliendaje?

Mbowe - Walienda kwa miguu

Kibatala - kulikuwa na kiongozi wa mawakala

Mbowe - ndio

Kibatala - alikuwa nani?

Mbowe - Boniface Jacob ambaye ni Meya wa Ubungo

Kibatala - Mawakala hawa kutoka Uwanja wa Buibui suala gani kubwa liliwapeleka kwa Mkurugenzi alideal nao vipi?

Mbowe - Kuna baadhi walikuwa kwa Mkurugenzi, wengine Uwanja wa Buibui na wale walikuwa uwanja wa Buibui baada ya mkutano walienda kwa Mkurugenzi.

Kibatala - Walipokelewaje?

Mbowe - Baadhi walipewa barua, wengine walipewa usiku

Kibatala - Nani pekee alikwenda kwa Mkurugenzi?

Mbowe - mawakala

Kibatala - Kamati ya Maadili inakuwa na kazi gani kipindi cha kampeni uchaguzi?

Mbowe - Kampeni zinasimamiwa na sheria, shughuli zote za Uchaguzi zinaratibiwa na Kamati ya Maadili, Matukio yote kuanzia siku ya kwanza hadi siku ya mwisho.

Kibatala - kwa ufahamu wako ni nani alienda ngome baada ya kufunga Kampeni

Mbowe - Tulipoachana na M/kiti wa kampeni ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na M/kiti wa Chadema Kanda ya Pwani Mhe. Frederick Sumaye na Boniface Jacob walielekea ilipo ngome yaliyopo Magomeni wakiwa na viongozi wengine.

Kibatala - Walitumia nini kwenda huko?

Mbowe - To my knowledge walitumia magari

Kibatala - Vipi kuhusu washtakiwa hapa?

Mbowe - nakumbuka walitawanyika kurudi maeneo yao kwa sababu wengine sio wakazi wa Dar es salaam.

Kibatala - Kuwa specific?

Mbowe - Mhe Heche na Msigwa hufikia Baobab Apartments

Kibatala - Kwa ufahamu wako ni nani alimpiga risasi Akwilina?

Mbowe - Kwa ufahamu wangu unaegemea kutokana na taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi kwa tamko la Mambosasa kwamba Jeshi la Polisi, wanawashikilia askari ambao walimpiga risasi.

Kibatala - sababu nyingine?

Mbowe - Kuna watu wengine walidai walipigwa risasi na askari polisi.

Kibatala - Sababu nyingine kama ipo?

Mbowe - hizo zinatosha.

Kibatala - Unasema wakati unaenda Makao Makuu ya Chadema ukisindikizwa na polisi hali ilikuwaje baada ya kukutana na Polisi CCM?

Mbowe - Hivi ni vyama vinavyoshindana, kulikuwa na hali ya kuzomeana na shamrashamra kwa pande zote za wafuasia wa vyama.

Kibatala - Ni Kiongozi gani alikamatwa Mkwajuni na polisi katika maandamano kama inavyodaiwa kulikuwa na maandamano?

Mbowe - Hakuna aliyekamatwa.

Kibatala - Walifikaje polisi na kufunguliwa mashtaka yanayowakabili hapa?

Mbowe - Wote kwa wito.

 
Naona baada ya kubanwa vilivyo huko mahakamani Mwenyekiti kaamua kukana kuwepo kwenye maandamano pale kinondoni.
1-Kama ni kweli hakuwepo wafuasi wa Chadema mnaopenda kuwa kimbelembele kwenye maandamano mnajisikiaje?

2-Kama alikuwepo anaigopa nini?

Source :Magazeti ya leo asubuhi
 
anawaruka wenzie wale kitanzi pekeyao watakoma yule dj msanii kinoma kazi kwako mashinji
 
Naona baada ya kubanwa vilivyo huko mahakamani Mwenyekiti kaamua kukana kuwepo kwenye maandamano pale kinondoni.
1-Kama ni kweli hakuwepo wafuasi wa Chadema mnaopenda kuwa kimbelembele kwenye maandamano mnajisikiaje?

2-Kama alikuwepo anaigopa nini?

Source :Magazeti ya leo asubuhi
Weka ushahidi kama ulimuona.
 
Naona baada ya kubanwa vilivyo huko mahakamani Mwenyekiti kaamua kukana kuwepo kwenye maandamano pale kinondoni.
1-Kama ni kweli hakuwepo wafuasi wa Chadema mnaopenda kuwa kimbelembele kwenye maandamano mnajisikiaje?

2-Kama alikuwepo anaigopa nini?

Source :Magazeti ya leo asubuhi

Unahitaji kuwa na akili kubwa kufahamu alichokifanya Mhe. Mbowe. Si ushabiki wa kitoto. Yale ya Kinondoni hayakuwa maandamano. Kama Mwenyekiti mwenye uweredi mkubwa hawezi kujitia kutanzani kwa kukiri eti yale yalikuwa maandamano.
 
Naona baada ya kubanwa vilivyo huko mahakamani Mwenyekiti kaamua kukana kuwepo kwenye maandamano pale kinondoni.
1-Kama ni kweli hakuwepo wafuasi wa Chadema mnaopenda kuwa kimbelembele kwenye maandamano mnajisikiaje?

2-Kama alikuwepo anaigopa nini?

Source :Magazeti ya leo asubuhi
Hahahaaaa..........hakuwepo mbele ya jicho la " sheria"

Umenikumbusha kesi ya Kachero nguli aliyebobea katika sheria kamanda mstaafu Zombe!
 
Naona baada ya kubanwa vilivyo huko mahakamani Mwenyekiti kaamua kukana kuwepo kwenye maandamano pale kinondoni.
1-Kama ni kweli hakuwepo wafuasi wa Chadema mnaopenda kuwa kimbelembele kwenye maandamano mnajisikiaje?

2-Kama alikuwepo anaigopa nini?

Source :Magazeti ya leo asubuhi
Nani alimuona? Ushahidi hautoshi
 
Maswala ya mahakama ni utata kidogo.

Kukataa kua kwenye maandamano. Inamaanisha ule umati uliotupiwa mabomu kwa kudhani ni maandamano ulitupiwa mabomu kimakosa.

Kama itathibitishwa yale hayakua maandamano na wale askari waliachiwa kwakua kuua na au kujeruhi wakati wa maandamano siyo kosa basi itabidi wakamatwe upya na mashtaka mapya juu ya Akwilina.

Hiyo ni kama hatosema hakuwepo ila hakuwepo kwenye maandamano. So atakua alikuepo ila siyo kwenye maandamano.

Binafsi naona hivyo. So siyo dili ya kumuona Mboewe muoga ila ni dili ya kisheria zaidi ndiyo maana amekataa.
 
Naona baada ya kubanwa vilivyo huko mahakamani Mwenyekiti kaamua kukana kuwepo kwenye maandamano pale kinondoni.
1-Kama ni kweli hakuwepo wafuasi wa Chadema mnaopenda kuwa kimbelembele kwenye maandamano mnajisikiaje?

2-Kama alikuwepo anaigopa nini?

Source :Magazeti ya leo asubuhi

Kutokuwepo kwa mbowe ktk maandamano ni vizuri sana dunia nzima hakuna kiongozi wa juu anaongoza maandamano ya kudai haki hata vitani kamanda hawi front wadanganye wa saizi yako
 
Naona baada ya kubanwa vilivyo huko mahakamani Mwenyekiti kaamua kukana kuwepo kwenye maandamano pale kinondoni.
1-Kama ni kweli hakuwepo wafuasi wa Chadema mnaopenda kuwa kimbelembele kwenye maandamano mnajisikiaje?

2-Kama alikuwepo anaigopa nini?

Source :Magazeti ya leo asubuhi
Ujïnga mtupu
 
Unahitaji kuwa na akili kubwa kufahamu alichokifanya Mhe. Mbowe. Si ushabiki wa kitoto. Yale ya Kinondoni hayakuwa maandamano. Kama Mwenyekiti mwenye uweredi mkubwa hawezi kujitia kutanzani kwa kukiri eti yale yalikuwa maandamano.
Mtoa mada hajasikiliza hoja za kibatara tangia awali,alimuuliza shahidi kwamba akiona watu wanaelekea sehemu basi ni maandamano? Baada ya mkutano kuisha je watu wangerudi vipi kwenda majumbani kwao? Wangepaa ili isionekane wanaandamana?
 
Mkuu huu ndio utamu wa sheria..mtu anakuruka unamuangalia mchana kweupe na anakushinda
Kweli bwana. Nakumbuka zamani bado niko mdogo, kuna baba yangu mdogo alimkata mzee mmoja hivi na panga lakini yule mzee bahati nzuri mwili haukupata jeraha ila shati lilichanika. Basi lile shati likapelekwa mahakamani kama kielelezo. Na shitaka lilifunguliwa kuwa baba mdogo alimkata mzee Laurent.
Ba' mdogo wangu siku ya kesi akauliza mahakama, "NASHITAKIWA KUMKATA LAURENT AU KUKATA SHATI LA LAURENT?"
Huwezi kuamini alishinda ile kesi.
Ila unajua mambo ya kinyumbani nyumbani kama sio kikijijini, babu alikwenda kwa yule mzee akamuomba msamaha, ili kuepusha kuvuruga mahusiano pale kijijini.
 
Huyo jingalao ni wa kumpuuza. Huyo hata akisikia kitu huwa haelewi. Ni aheri mjinga mwerevu kuliko huyu. Tuupuuze ujinga wake.
 
Back
Top Bottom