SI KWELI PreGE2025 Mbowe achukua jengo la ofisi kuu ya CHADEMA

SI KWELI PreGE2025 Mbowe achukua jengo la ofisi kuu ya CHADEMA

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wakuu nimekutana na hiki kipeperushi hapa kinadai kuwa aliyekua Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amechukuwa jengo la ofisi kuu za chama hicho.

photo_2025-07-29_08-59-58.jpg
 
Tunachokijua
Freeman Mbowe alikuwa ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuanzia mwaka 2004 hadi 2025 ambapo alishindwa uchaguzi na Mwenyekiti wa sasa Tundu Lissu.

Madai

Julai 28, 2025 kumeibuka taarifa ikidai kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amechukua jengo la ofisi kuu za chama hicho lililopo Mikocheni jijini Dar es salaam.

Taarifa hiyo inaendelea kwa kueleza kuwa Mbowe amewapa mwezi mmoja viongozi wa chama hicho kuhama na kama hawatofanya hivyo atazitupa nje nyaraka hizo.

Uhalisia wa taarifa hiyo

Ufuatilaiji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

Taarifa hiyo haijatolewa na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kama gazeti hilo linavyodai. Jengo ambalo kwa sasa ni ofisi za CHADEMA iliripotiwa na chombo cha habari cha Mwananchi kuwa ofisi hizo zililinunuliwa na kukarabatiwa kwa gharama ya Sh1.5 bilioni mwaka 2023

JamiiCheck imewasilia na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia ambaye amekanusha taarifa hizo na kueleza kuwa:

"Hizo taarifa hazina ukweli, Mbowe hajachukua jengo lolote la chama kwa kuwa hilo wanalilozungumzia lina nyaraka halali za chama na zipo kwenye Sekretarieti ya Chama, nyaraka zinasoma jina la chama na sio za Mbowe".
tatizo umekosa ubunifu wa kudanganya muandishi makini hawezi mwita yeyote mlevi bila kuwa na uthibitisho ni ishara kuwa muandishi hana elimu dunia ya kutosha celix @555fier BlackBold viongozi mnaachaje uzi wa hivi umalize lisaa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom