Mbowe acha siasa za maigizo, UKAWA hamna akidi ya kumng'oa Naibu Spika

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,285
38,363
Acha kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa vitu ambavyo vipo wazi kabisa kuwa huwezi kushinda.Inajulikana kabisa kuwa kambi rasmi ya Upinzani haifiki hata nusu ya wabunge wa CCM, lakini unaleta hoja zinazohitaji akidi kuamuliwa. Na unaeneza propaganda kuwa kuna wabunge wa CCM hawana Imani Na Naibu Spika hivyo watakuunga mkono kumng'oa Naibu Spika.

Hivi lini wabunge wa CCM wamewai kusaliti chama chao kwa maslai ya Wapinzani.? Mh.Mbowe umepwaya sana, unatakiwa kubadili aina Na muelekeo wa siasa za Upinzani Bungeni Na nje ya Bunge kwa ujumla. Utawala huu unamapungufu mengi tu pamoja Na mazuri Yake...ni jukumu la kambi yako kujenga hoja zenye mshiko mtaeleweka tu.

Acha siasa za matukio, la sivyo utacheza CD zote za CCM. Sasa hivi CCM wanaenda kukabidhiana madaraka.... Naibu Spika, Bunge live,Lugumi,Udom zitachuja mtakurupikia uchaguzi wa ndani wa CCM Na kusahau haya mengine.

Ni mtazamo tu..!
 
Hivi unakumbuka kwamba katika ile petition ya kumtoa Pinda hata wabunge wa CCM waliisaini? Idadi ya wabunge wa upinzani ilikuwa ndogo lakini akidi ilipatikana na azimio likavurugwa tu.kwa matumizi mabaya ya kanuni
 
Acha kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa vitu ambavyo vipo wazi kabisa kuwa huwezi kushinda.

Inajulikana kabisa kuwa kambi rasmi ya Upinzani haifiki hata nusu ya wabunge wa CCM, lakini unaleta hoja zinazohitaji akidi kuamuliwa.

Na unaeneza propaganda kuwa kuna wabunge wa CCM hawana Imani Na Naibu Spika hivyo watakuunga mkono kumng'oa Naibu Spika.

Hivi lini wabunge wa CCM wamewai kusaliti chama chao kwa maslai ya Wapinzani.?

Mh.Mbowe umepwaya sana, unatakiwa kubadili aina Na muelekeo wa siasa za Upinzani Bungeni Na nje ya Bunge kwa ujumla.

Utawala huu unamapungufu mengi tu pamoja Na mazuri Yake...ni jukumu la kambi yako kujenga hoja zenye mshiko mtaeleweka tu.

Acha siasa za matukio, la sivyo utacheza CD zote za CCM.

Sasa hivi CCM wanaenda kukabidhiana madaraka.... Naibu Spika, Bunge live,Lugumi,Udom zitachuja mtakurupikia uchaguzi wa ndani wa CCM Na kusahau haya mengine.

Ni mtazamo tu..!
Hang on please. Mr Mbowe has a point.

Do you remember that Mr Lowassa joined UKAWA with a promise to bring 50 MPs from CCM, plus 20 CCM Chairmen? He has yet to land his promise and deliver; maybe this is where he is now going to deliver and kick the Deputy Speaker out.
 
Naona huzijui hesabu za siasa, kwenye siasa sio lazima upate wanachokitegemea wengine bali upate unachokitaka wewe.

Kwenye siasa 2 + 2 = 22.

Kama unategemea hadi uone NS aking'olewa utasubiri sana.
 
Umemsikia Zitto alivyomchana Baba yake na Jesca (yule KILAZA wa UDOM)? Anasema anaokoteza maneno ya mitaani halafu anafanya maamuzi ya kukurupuka na mbaya zaidi ni MROPOKAJI. Teh! Teh! Teh! Kumbe Shetani amejivika ngozi ya Malaika.

Mkuu humu ndani kuna mada nyingi za kimhusu "Baba Jesca" , mada iliyo mbele yako ni siasa za Upinzani Bungeni Na nchi nzima kwa ujumla.!
 
Naomba nieleweshwe kanuni zinasemaje inapobidi kura ya kutokuwa na imani kupigwa. Jee ni siri au wazi?
Kama ni wazi NS hang'oki ila atapata fedheha kupigiwa kura ya kutokuwa na imani. Lakini kama ni kura ya siri anaondoka Mara moja
 
Hakuna Kura ya wazi wala ya siri, kinachohitajika ni saini tu.!
 
Naona huzijui hesabu za siasa, kwenye siasa sio lazima upate wanachokitegemea wengine bali upate unachokitaka wewe.

Kwenye siasa 2 + 2 = 22.

Kama unategemea hadi uone NS aking'olewa utasubiri sana.

Haya bwana naendelea kusubiri hiyo ya 2+2=22. Itawezekana vipi.!
 
Hivi unakumbuka kwamba katika ile petition ya kumtoa Pinda hata wabunge wa CCM waliisaini? Idadi ya wabunge wa upinzani ilikuwa ndogo lakini akidi ilipatikana na azimio likavurugwa tu.kwa matumizi mabaya ya kanuni
FYI lile lilikuwa igizo tu ....kama serikali haitaki naibu spika atoke HATOKI! Chukua hiyo chungu kwelikweli ...maigizo ya kisiasa yanachosha sasa ...
 
wangebaki kipindi ambacho nasari alipotoa hoja yake ya wale wanafunz vilaza according to magufuli ningekwambia sina waswas hawawez kumtoa naibu spika ila kana walitoka jinoe upya na hii post yako na chanzo cha kutoka hao wabunge wa CCM chanzo ni nani? moyo wa mtu ni kichaka.....wengi walimpenda zungu.
 
Naona huzijui hesabu za siasa, kwenye siasa sio lazima upate wanachokitegemea wengine bali upate unachokitaka wewe.

Kwenye siasa 2 + 2 = 22.

Kama unategemea hadi uone NS aking'olewa utasubiri sana.
Umemjibu vizuri sana.Huyu siasa haijui.Hatua ya UKAWA kwa hapo ilipofikia ni pigo kubwa kwa Naibu Spika bila kujali nini kitafuata.

Kwa maneno mengine,CV yake tayari imeingia doa hasa kama ana lengo la kuja kugombea ubunge siku za baadae.Kaingia doa la kumpunguzia kura.
 
wangebaki kipindi ambacho nasari alipotoa hoja yake ya wale wanafunz vilaza according to magufuli ningekwambia sina waswas hawawez kumtoa naibu spika ila kana walitoka jinoe upya na hii post yako na chanzo cha kutoka hao wabunge wa ccm chanzo ni nani? moyo wa mtu ni kichaka.....wengi walimpenda zungu.

Mkuu siasa ni hesabu sio kudra!
 
Umemjibu vizuri sana.Huyu siasa haijui.Hatua ya UKAWA kwa hapo ilipofikia ni pigo kubwa kwa Naibu Spika bila kujali nini kitafuata.

Kwa maneno mengine,CV yake tayari imeingia doa hasa kama ana lengo la kuja kugombea ubunge siku za baadae.Kaingia doa la kumpunguzia kura.

Mkuu kama doa alipewa Lowasa ndani ya miaka nane lakini mwisho wa siku akaishia kuabudiwa Na wale wale.

Hivyo sitashangaa kesho kusikia Tulia ni shujaa wa CHADEMA.!
 
Mkuu humu ndani kuna mada nyingi za kimhusu "Baba Jesca" , mada iliyo mbele yako ni siasa za Upinzani Bungeni Na nchi nzima kwa ujumla.!

Namkumbuka Marehemu Mbunge Filikunjombe! Ndiyo mbunge pekee wa ccm aliyeipenda Tanzania... wengine wote ni wachumia tumbo tu. Kwenye upuuzi huu wa naibu speaker ... Deo angekuwa kwa wapinzani (kudai ang'olewe)!
 
Mkuu kama doa alipewa Lowasa ndani ya miaka nane lakini mwisho wa siku akaishia kuabudiwa Na wale wale.

Hivyo sitashangaa kesho kusikia Tulia ni shujaa wa Chadema.!

mkuu naona unahamisha magoli taratibu inshu ni naibu spika hapa jikite hapo kumtetea atachomoka vipi na huu msala mana hata raia huku wanahoji uwezo wake.
 
Back
Top Bottom