Mbona Zanzibar mafuta hayashuki bei?

Mbona Zanzibar mafuta hayashuki bei?

farooq2013

Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
98
Reaction score
16
Kinachonishangaza EWURA walitangaza ushukaji wa mafuta nchi nzima tangu Disemba na hadi jana mafuta ya petroli bara yanauzwa 1623 lkn huku kwetu zanzibar bei bado ni 1965.

Sijui wenzetu wa Zanzibar mafuta wanayachukua nchi gani au sie tupo nchi tofauti na Tanganyika.Kibaya zaidi hali ya uchumi ya Zanzibar ipo chini ukilinganisha na wenzetu kwa hiyo bei hiyo ya mafuta inazidi kutukwamisha kimaisha na kimaendeleo.
 
Nafikiri Maalim Seif ana majibu mazuri zaidi.
 
EWURA sio chombo cha Muungano wala kwenye zile hati za waasisi EWURA haimo. Undeni chombo chenu cha kushughulikia mambo kama hayo. By the way, si mlisema mafuta ya Zanzibar ni ya wazanzibar?
 
Vipi tena mafuta hayashuki bei kwenye koloni letu la zanzibar?
 
nyie wazanzibari si mlitaka mafuta na gesi yaondoshwe kwenye masuala ya muungano? kwani mmeona Tanganyika inajihusisha na kushusha bei ya mafuta zanzibari?
huko muendelee na baraza la mapinduzi kushusha hiyo bei kwa utaratibu mliojipangia
 
nyie wazanzibari si mlitaka mafuta na gesi yaondoshwe kwenye masuala ya muungano? kwani mmeona Tanganyika inajihusisha na kushusha bei ya mafuta zanzibari?
huko muendelee na baraza la mapinduzi kushusha hiyo bei kwa utaratibu mliojipangia
 
Wazanzibar wakitingwa ndio wakakumbuka kuwa kumbe kunatanganyika.
 
Kwa kumbukumbu zangu, mafuta si suala la muungano.
 
ZANZIBAR ni nchi au siyo nchi?:A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:

Mkuu mamlaka ya EWURA hayavuki bahari....mwisho wake ni katika mipaka ya TANGANYIKA
 
Nafikiri Maalim Seif ana majibu mazuri zaidi.

Hawezi jibu hili sababu mapato ya kodi ya serikali ya umoja wa kitaifa yatapungua bei ikishuka.Na yeye anategemea maruprupu kutokana na hiyo kodi.Mnataka mabenzi yake yakose pesa za kuyaendesha maruhuni nyie.

Bei haishuki.Heri magari yenu yasimame lakini sio ya maalim seif makamu raisi wa serikali ya Zanzibar
 
Back
Top Bottom